Mayai ya kanga

Mayai ya kanga

Black Sniper

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Posts
34,434
Reaction score
59,289
Ndugu zangu naomba msaada nimefuga kanga na kuku upande wa kuku hakuna tatizo ndipo nikaona nijiongeze kufuga kanga. Ni eneo kubwa sana wanapata chakula cha kutosha tatizo wanataga vichakani bila mimi kujua na kupata mayai ni shida, baada ya kufatilia sana nimepata sehemu wanayotagia na kufanikisha kupata mayai 60 lakini wanyama wamepitia mayai 35.

Hayo mayai nimeyauza maana nikiwawekea kuku wanatotoa mawili tu, msaada tafadhali kama kuna njia ya wao kutagia bandani
 
Yai la kanga ni shilingi ngapi? Na vp wadau unaweza kufuga kanga na kuku kwenye banda moja? Na soko la kanga likoje? Kanga mkubwa anauzwa shilingi ngapi? Naomba kujuzwa na bei ya mayai ya bata bukini. Natanguliza shukrani
 
Nafuga kanga. mnyama yeyote ukimkondisheni anafata. kaka ni kiumbe rahisi kukielekeza.
Mi kanga wangu wrote wanatagia ndani tena wengine sebuleni. Mda wa kutaga kanga ni kati ya SAA 4 mpaka SAA 9 mchana. na kuna mlio ambao Kanga Jogoo anatoa kipindi jike anataga. mda huo mfukuze na ondoa mayai polini baada ya hapo ktk harakati za kutafuta pa kutagia mtengenezee bandani na sehemu yenye uficho. akiingia mfungie pamoja na
jogoo yule anayefatana nae. Daily atataga pale na unaweza kuta wote wanataga hapo. kama walitotolewa na kuku mtumie pia mama yao kuwaweka bandani.
 
Yai la kanga ni shilingi ngapi? Na vp wadau unaweza kufuga kanga na kuku kwenye banda moja? Na soko la kanga likoje? Kanga mkubwa anauzwa shilingi ngapi? Naomba kujuzwa na bei ya mayai ya bata bukini. Natanguliza shukrani
Inategemea na ulipo mi ntajibu swali moja. Ndio unaweza kufuga kanga na kuku pamoja ila kanga jogoo ni wakorofi wanadonoa sana kuku hadi kuvuja damu.
Nyama yake ni tamu. kuna watu wanawaitaji sema hawapatikani. Kanga mmoja namuuza kati ya elfu 15 hadi 20 na niko kijijini.
na hawaitaji chanjo wala madawa. wanataga sana mwezi wa 11 mpaka wa 6. Tatizo lao na wanyama hasa mbwa na pia kama ukiwaruhusu kutembea ni rahisi kugongwa na magari au pikipiki. Kanga ni mtamu.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Ila wanasema ukichinja kanga hakikisha wenzake hawajui kinachoendelea hata manyoya wasiyaone vinginevyo......
 
Back
Top Bottom