Maxence Melo: Neno la shukrani kwa wote

Heshima kwenu wakuu!

Shukrani:

Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kuiona siku ya leo nami kuwa nanyi siku hii ninapoandika waraka huu mfupi ukilenga zaidi kutoa shukrani. Shukrani hizi nilitamani nimtumie mmoja mmoja lakini nimeshindwa kwani ni wengi wanaostahili kushukuriwa.

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kupaza sauti zao (kwa njia yoyote ile) ili aidha nifikishwe mahakamani au niachiwe bila masharti yoyote (nilipokuwa Kituo cha Kati) na baadae kuendelea kupaza sauti kutaka mahakama initendee haki niwe huru baada ya kupelekwa gerezani Keko.

Nawashukuru mawakili wangu na wengine walioamua kujitolea kuingia katika utetezi wangu hata bila kuombwa. Kipekee, namshukuru na kumpa pole sana Ndg. Albert Msando ambaye tayari alishaonesha nia ya kuwa mtetezi wangu lakini yakamkuta yaliyomkuta, tumwombee kwa Mwenyezi Mungu apate uponyaji wa haraka.

Nipende kuwashukuru wana JamiiForums wote kwa mijadala iliyoendelea wakati wote ambao sikuwepo; vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi vilivyoshiriki katika hatua hii ya awali (kazi ndio imeanza); watumiaji wa mtandao wa Twitter(bila kutaja mmoja mmoja) kwa jitihada zao ambazo zimenishangaza kuhakikisha hashtag ya [HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG] ina-trend na kuwa tayari kwao kutoa maoni yao kwa vyombo vya habari pale walipohitajika kufanya hivyo; nawashukuru Wahisani mbalimbali na wadau wa maendeleo ambao walituma wawakilishi wao Central na Gerezani kufuatilia napitia maisha gani na hata kuwasiliana na mamlaka zinazohusika kutaka nitendewe haki.

Aidha, nawashukuru sana wafanyakazi wa Jamii Media ambao naelewa kwa kiwango gani kilichotokea kilivyowaathiri kisaikolojia na hata kiutendaji. Nawashukuru Asasi za Kiraia zikiongozwa na THRDC, LHRC, Sikika, C-Sema, TMF n.k kwa kuwa mstari wa mbele kufuatilia na kuelewa kinachoendelea na hata kujitoa kwa ajili ya udhamini wangu pale walipoombwa na wengine hata bila kuombwa. Jukwaa la Wahariri(TEF) – Asanteni sana!

Nichukue fursa hii kuwashukuru pia watanzania katika makundi mbalimbali ya WhatsApp, Facebook na Telegram kwa ushirikiano waliouonesha. Watumiaji wa Instagram(nashindwa kutaja mmoja mmoja), nawashukuruni sana kwani nimeona posts nyingi toka kwa watu hata ambao hawanifahamu lakini walioelewa ninachosimamia wakitoa support kubwa sana.

Ndugu, marafiki na majirani zangu – asanteni sana kwani mlikuwa nasi bega kwa bega wakati wote. Watanzania na wote ambao si watanzania mliojitahidi kufika Central na Gerezani kunijulia hali – Asanteni sana na Mungu awabariki sana!

Kuna wale ambao hata hawajaelewa kesi inahusu nini hasa na wameanza kuwashambulia waliokuwa wakinitetea, nao nawashukuru kwani naamini ni kwakuwa hawajajua nini kimo kwenye kesi. Ila niwahakikishie kuwa si rahisi kutetea mhaini, unapoona mtu anaamua kufanya hivi ni vyema kutafakari.

Askari wa Kituo cha Kati(Central) na wale wa Gereza la Keko – asanteni sana. Naelewa ni vigumu umma wa watanzania kuelewa namaanisha nini lakini ninyi kwa andishi hili mnaelewa vema ninachomaanisha. Wengi mliifanya kazi yenu kwa weledi mkubwa.

Viongozi wa kidini(wachungaji, ma-sheikh, maaskofu n.k) na wanasiasa wote(toka vyama vya upinzani na chama tawala) mlioshiriki katika hili – Asanteni sana. Hamkuingiza itikadi za kisiasa wala misimamo ya kidini bali mlitaka haki kutendeka. Nawashukuru!

Kuhusu kesi:

Ndugu zangu, ndio kwanza kesi inaanza kuunguruma tarehe 29 Disemba 2016. Si rahisi mimi kuongelea nini kilichomo kwenye kesi lakini naamini vyombo vingine vya habari kwakuwa tunayo sheria ya Haki ya Kupata Taarifa vinajua namna ya kuhakikisha vinaueleza umma nini kilichomo ndani yake (Mahakama Kuu na Mahakama ya Kisutu) ili watanzania waweze kuelewa mbivu na mbichi. Kuna ambao watajikuta kuwa walikuwa ndio walengwa hata hawakuguswa na kukamatwa kwangu, hapo ndipo watajua tunapigania nini.

Nipende kuwaomba tuendelee kuwa pamoja katika safari hii tunayoianza. Mimi ni sampuli tu, nasimama kwa ajili ya wale ambao naamini wana haki ya kutoa maoni na kufichua maovu (ili mradi hawajavunja sheria) na ninaamini wengi tunataka haki hii isipotee na iendelee kulindwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri wa Muungano.

Sina mengi kwa leo zaidi ya shukrani.

Wenu,

Maxence M. Melo

Huo ndiyo utu kutoa shukrani. safi na pole ya huko gerezani Keko. Tupo pamoja.
 
Ndugu zangu, ndio kwanza kesi inaanza kuunguruma tarehe 29 Disemba 2016. Si rahisi mimi kuongelea nini kilichomo kwenye kesi lakini naamini vyombo vingine vya habari kwakuwa tunayo sheria ya Haki ya Kupata Taarifa vinajua namna ya kuhakikisha vinaueleza umma nini kilichomo ndani yake (Mahakama Kuu na Mahakama ya Kisutu) ili watanzania waweze kuelewa mbivu na mbichi. Kuna ambao watajikuta kuwa walikuwa ndio walengwa hata hawakuguswa na kukamatwa kwangu, hapo ndipo watajua tunapigania nini.
Mkuu, tarehe hii ni kama mwendelezo wa 'ukomoaji', hapa wanajua itakuwia vigumu kusafiri wakati huu wa sikukuu!
 
Across the bridge, there is no sorrow,
Across the bridge, there is no pain,
([HASHTAG]#JimReeves[/HASHTAG])
.........
Keep well & keep living maestro Max!
 
Nitakuweka kwenye maombi yangu kwa Mungu, huko ndo naamini kweli na haki ipo, huko ndo Mungu alijidhihirisha dhidi ya jeshi la Farao.
 
Pole sana kaka. Kama yalivyopita hayo na nyuma nina imani na yajayo yatapita pia. M'mungu azidi kukutangulia kwa kila jambo.
 
Nipende kuwaomba tuendelee kuwa pamoja katika safari hii tunayoianza. Mimi ni sampuli tu, nasimama kwa ajili ya wale ambao naamini wana haki ya kutoa maoni na kufichua maovu (ili mradi hawajavunja sheria) na ninaamini wengi tunataka haki hii isipotee na iendelee kulindwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri wa Muungano.

Sina mengi kwa leo zaidi ya shukrani.

Wenu,

Maxence M. Melo

Pole sana Bro.Max. Ni wachache wanaoweza kusimama imara hata pale maumivu wanayapowaguza mpaka kwenye mifupa ya miili yao. Ni wape Pole kubwa Familia yako iliyopata wakati mgumu kipindi uko ndani kwa masilahi mapana ya Watanzania. Mambo haya yanagharama zake. Mfano mzuri wa Mandela -mpka mwisho wa siku Familia yake iliparaganyika kwa kuwatetea Waafrika weusi wa Afrika Kusini toka mikono ya Ubaguzi.

Malipo ya hapa Duniani ni magumu muda mwingine,lakini Muumba wa Bingu na Nchi anajua njia sahihi ya kutuongoza.

Pole sana na endelea kuwa na imani hiyo kwa faida ya Vizazi vya leo na Kesho.
Nikisoma hoja ya MMM kuhusu kinachotafutwa kweli inaumza na ni vigumu kauamini kama kweli kuwekwa kwako ndani kunauhusiana na watoa taarifa za kifisadi?.

Kama hili linaharufu ya ukweli basi walaaniwe Tanzania ya Viwanda na Maendeleo Kedekede ni ndoto ya mchana.
 
Tupo Pamoja Mkuu, Mungu na Azidi kuwa nawe nyakat zote! Ili nguvu nyepesi ya adui ikapate kushindwa, kwa Jina la Yesu
 
Back
Top Bottom