Maxcom Africa iangaliwe kwa jicho la karibu

kijembeee

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
409
Reaction score
105
Nitoe rai kwa waziri na wizara husika, tume ya ushindani na kwa raisi kuangalia kwa ukaribu jambo hili.

Nimefanya uchunguzi mdogo nimegundua madudu haya, uchunguzi wa kina utagundua mengi zaidi, hivyo vyombo husika vifanye majukumu yake ipasavyo

USHAURI: KAMPUNI YA MAXCOM ICHUNGUZWE KATIKA HAYA MACHACHE, NA MENGI ZAIDI YATAGUNGULIKA KWENYE HII KAMPUNI YA KITAPELI

Usalama wa servers na taarifa za wateja na usalama wa taifa

Usalama wa server zao unatia mashaka, natumai uchunguzi ukifanyika hili litabainika, labda wawe wamefanya mabadiliko baada ya kusoma makala hii.

Ukizingatia kua mfumo wao unaunganishwa na mitandao ya serikali kama TRA, ni vyema kujiridhisha na usalama wa server zao, ili kuhakikisha hali ya usalama.

Pia kwakua ni kampuni inayokua na ipo kwenye sekta nyeti sana, ni vyema iwe lazima wapate kibali cha ISO , ili kuhakikisha hawafanyi biashara zao kienyeji enjeji.

Ni vyema kujua Kuna cyber attacks, na shambulio kwa kampuni hii ni kwamba mwendokasi haitafanya kazi,matrafki nao siku hio wataweka pesa mfukoni etc, na kadri siku zinavyokwenda na wanavyohonga kupata tenda, itafika wakati wamepata tenda kwenye sekta nyeti zaidi na cyber attack itakua na madhara makubwa sana.

Mfumo wa biashara kwa mikoani umeambatana na utapeli

Kampuni hii inafanya kazi Tanzania nzima, na pia ina wasambazaji wa bidhaa mikoa yote, kwa miaka mingi tatizo ni kwa baadhi ya mikoa mingi kampuni haina ofisi, na biashara zinafanyikia barabarani hivyo kusababisha watu wengi kutapeliwa fedha na watu wanaojifanya kua ni maajenti wa maxcom, na pia wateja waliotoa pesa taslimu hawapewi risiti, hivyo kukosa kielelezo kama kweli walitoa pesa
.Ni jukumu la kampuni kulinda wateja wake na kuhakikisha kua ina ofisi isiyohamishika, ili kulinda maslahi ya mteja.

Matangazo ya uongo kwa bidhaa ambazo hazipo kwenye mashine.

Tume ya ushindani na serikali kwa ujumla imekalia kimya swala la wateja wa bidhaa kutoka maxcom kulaghaiwa mchana kweupe. Kampuni hii kwa miaka mingi kupitia matangazo yake imedai kutoa huduma nyingi, ambazo nyingine ni mapambo tu, hazipo kwenye mashine, na timu ya mauzo imedanganya wateja kuhusu uwepo wa bidhaa hizo kwenye mashine ilihali bidhaa hizo hazipo, au zipo kwa kiwango kidogo tofauti na ilivoelezwa kwa tangazo. Mfano wa bidhaa hizo ni huduma za tigo pesa, airtel money ambazo kiuhalisia hazipo, mambo ya pensheni na huduma za hospitali zote zimewekwa kama mapambo kuvutia wateja. Wanaponunua ndio wanagundua wametapeliwa.
Hii si haki kwa mteja. Inabidi walipe faini kwa kudanganya uma.

Tume ya ushindani kumlinda mteja juu ya bidhaa ambayo mara nyingi mtandao upo chini

POS za maxmalipo zinakumbwa na tatizo ambalo ni la muda mrefu, na limekua sugu la mtandao kua chini, hivyo mteja alienunua bidhaa hio kwa sababu ya kuzungusha pesa yake anapokumbwa na tatizo la mtandao siku nzima kisa hio siku kuna mawingu, au mtandao umekorofisha siku nzima sio haki, na uonevu kwa mteja na kampuni inatakiwa imlipe mteja kwa biashara aliopoteza kwa siku hio.

Kuvunja mkataba na mteja kuhusu umbali wa msambazaji mmoja na mwingine.

Mkataba kati ya mteja wa mashine na kampuni ni kwamba, kampuni haitamuuzia mtu mwingine mashine wa eneo jirani na biashara ya mteja wa kwanza ili kulinda maslahi ya mteja huyo(kumlinda na ushindani).kampuni haijatekeleza sharti hili la mkataba, na imekua ikiuza mashine bila kuzingatia hili, hivyo kuwafanya wateja wa mashine hizo walizonunua awali wakijua kua katika maeneo husika watakua ndio watoa huduma pekee, kupatwa na hali ya simanzi na kuhisi kutapeliwa.

Kufukuza wafanyakazi bila kufata taratibu

Wafanyakazi wa kampuni hii hawajaandikishwa kwenye vyama vya wafanyakazi, na hivyo kuna uonevu mkubwa kwa wafanyakazi, na uchunguzi ukifanyika utabaini ubabe na kufukuzwa kazi kwa wafanyakazi wengi pasipo kufata taratibu za wafanyazi (Tanzania Labor Laws)
 
Mtoa mada maelezo yako mengi uko sahihi.

Nadhani Maxcom wangerekebisha haya mambo kwa haraka bila ubahili na unyonyaji kwa wafanyakazi wake ingekuwa poa.

Maxcom ni kampuni ya mtanzania mwenzetu ndg Juma. Ikiwa tunachochea watanzania wafungue viwanda basi anahitaji support kubwa toka Costech,TCRa na wadau wengine wa serikali.

Tatizo la network kuwa down Tanzania naona ni janga la taifa ukienda TRA mifumo yao ya TANCis na mengineyo mengi inakuwa down kila kukicha,
Ukienda mabank crdb, nmb, Western union platforms kwa bongo kila kukicha tupo down.
Imefika wakati hata trafiki anakumbia mfumo upo down.

Tunahitaji ku import na experts wa mifumo, Fedha zitutoke za maana tujenge network servers za ukweli.

Afrika ya kusini huwezi hata siku mojaa ukasikia hakuna network bank au popote hata Reservation systema za hotel tuu hapa bongo zinasumbua.

Ukitaka kujua bado tunajikongoja angalia website tu za mashirika ya serikali na binafsi uone zilivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la nchi hii tupo reactive, hatupo proactive. This is a ticking bomb lakini hatufanyi chochote hadi disaster itokee ndio tunaanza kutafta wa kumlaumu.
Nadhani approach nzuri ingekua hii ya kuonyana b4 disasters happen
Kweli kabisa.
 
Ndio ubepari huo.

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
 
Wameanza ondolewa mdogo mdogo
Trafic washawatoa tayari
Dawasco pia
 
Una maelezo marefu na Mazuri, ila Nnadhan Hii research yako haina mizania. Mimi ni Mdau wa ICt na nimekua naifuatilia vyema Kampuni hii.

UZi wako unatakiwa uuboreshe.

1. Je Umejiridhishaje kwamba servers sio salama?

2. Je umewahi kukutana na wadau kujua haya?

Sisi tuliopitia Ujasiriamali Tunasema Hizi ni propaganda za maji taka.

Watanzania Tunatakiwa kubadilika, tuenzi vitu vya nyumbani, tunapitwa na majirani zetu kwa kuwa na wivu. Ungekua na maana kama ungetuandikia barua ulizoandikia serikali au kampuni hii kuwataka waboreshe utendaji wao.

Tubadilike

Nitoe rai kwa waziri na wizara husika, tume ya ushindani na kwa raisi kuangalia kwa ukaribu jambo hili.

Nimefanya uchunguzi mdogo nimegundua madudu haya, uchunguzi wa kina utagundua mengi zaidi, hivyo vyombo husika vifanye majukumu yake ipasavyo

USHAURI: KAMPUNI YA MAXCOM ICHUNGUZWE KATIKA HAYA MACHACHE, NA MENGI ZAIDI YATAGUNGULIKA KWENYE HII KAMPUNI YA KITAPELI

Usalama wa servers na taarifa za wateja na usalama wa taifa

Usalama wa server zao unatia mashaka, natumai uchunguzi ukifanyika hili litabainika, labda wawe wamefanya mabadiliko baada ya kusoma makala hii.

Ukizingatia kua mfumo wao unaunganishwa na mitandao ya serikali kama TRA, ni vyema kujiridhisha na usalama wa server zao, ili kuhakikisha hali ya usalama.

Pia kwakua ni kampuni inayokua na ipo kwenye sekta nyeti sana, ni vyema iwe lazima wapate kibali cha ISO , ili kuhakikisha hawafanyi biashara zao kienyeji enjeji.

Ni vyema kujua Kuna cyber attacks, na shambulio kwa kampuni hii ni kwamba mwendokasi haitafanya kazi,matrafki nao siku hio wataweka pesa mfukoni etc, na kadri siku zinavyokwenda na wanavyohonga kupata tenda, itafika wakati wamepata tenda kwenye sekta nyeti zaidi na cyber attack itakua na madhara makubwa sana.

Mfumo wa biashara kwa mikoani umeambatana na utapeli

Kampuni hii inafanya kazi Tanzania nzima, na pia ina wasambazaji wa bidhaa mikoa yote, kwa miaka mingi tatizo ni kwa baadhi ya mikoa mingi kampuni haina ofisi, na biashara zinafanyikia barabarani hivyo kusababisha watu wengi kutapeliwa fedha na watu wanaojifanya kua ni maajenti wa maxcom, na pia wateja waliotoa pesa taslimu hawapewi risiti, hivyo kukosa kielelezo kama kweli walitoa pesa
.Ni jukumu la kampuni kulinda wateja wake na kuhakikisha kua ina ofisi isiyohamishika, ili kulinda maslahi ya mteja.

Matangazo ya uongo kwa bidhaa ambazo hazipo kwenye mashine.

Tume ya ushindani na serikali kwa ujumla imekalia kimya swala la wateja wa bidhaa kutoka maxcom kulaghaiwa mchana kweupe. Kampuni hii kwa miaka mingi kupitia matangazo yake imedai kutoa huduma nyingi, ambazo nyingine ni mapambo tu, hazipo kwenye mashine, na timu ya mauzo imedanganya wateja kuhusu uwepo wa bidhaa hizo kwenye mashine ilihali bidhaa hizo hazipo, au zipo kwa kiwango kidogo tofauti na ilivoelezwa kwa tangazo. Mfano wa bidhaa hizo ni huduma za tigo pesa, airtel money ambazo kiuhalisia hazipo, mambo ya pensheni na huduma za hospitali zote zimewekwa kama mapambo kuvutia wateja. Wanaponunua ndio wanagundua wametapeliwa.
Hii si haki kwa mteja. Inabidi walipe faini kwa kudanganya uma.

Tume ya ushindani kumlinda mteja juu ya bidhaa ambayo mara nyingi mtandao upo chini

POS za maxmalipo zinakumbwa na tatizo ambalo ni la muda mrefu, na limekua sugu la mtandao kua chini, hivyo mteja alienunua bidhaa hio kwa sababu ya kuzungusha pesa yake anapokumbwa na tatizo la mtandao siku nzima kisa hio siku kuna mawingu, au mtandao umekorofisha siku nzima sio haki, na uonevu kwa mteja na kampuni inatakiwa imlipe mteja kwa biashara aliopoteza kwa siku hio.

Kuvunja mkataba na mteja kuhusu umbali wa msambazaji mmoja na mwingine.

Mkataba kati ya mteja wa mashine na kampuni ni kwamba, kampuni haitamuuzia mtu mwingine mashine wa eneo jirani na biashara ya mteja wa kwanza ili kulinda maslahi ya mteja huyo(kumlinda na ushindani).kampuni haijatekeleza sharti hili la mkataba, na imekua ikiuza mashine bila kuzingatia hili, hivyo kuwafanya wateja wa mashine hizo walizonunua awali wakijua kua katika maeneo husika watakua ndio watoa huduma pekee, kupatwa na hali ya simanzi na kuhisi kutapeliwa.

Kufukuza wafanyakazi bila kufata taratibu

Wafanyakazi wa kampuni hii hawajaandikishwa kwenye vyama vya wafanyakazi, na hivyo kuna uonevu mkubwa kwa wafanyakazi, na uchunguzi ukifanyika utabaini ubabe na kufukuzwa kazi kwa wafanyakazi wengi pasipo kufata taratibu za wafanyazi (Tanzania Labor Laws)
 
wadau nimesoma mjadala na kuelewa....nadhani ni vyema tukajadili mchango wa technoloji kwa nchi yetu hasa hasa kwa kampuni zetu za wazawa ndani vinginevyo tutaishia kulalamika kwa kuendekeza makampuni ya nje yanayokuja hapa kuchuma na kuondoka....mwishoe tunaishia kwenye yale yale ya makinikia....TUJIKITE KWENYE HOJA ZA MSINGI BADALA YA KUENDELEZA PROPAGANDA AMBAZO KIUKWELI KAMA TAIFA HAZITUSAIDII....TUJENGE NCHI JMN HII NCHI NI YA KWETU WOTE.....LETENI HOJA NA SIO VIOJA
 
Awamu ya Tano tayari imeanza kumvunjia Mikataba Maxcom katika baadhi ya Idara za Serikali!
 
maxcom wakala wake akikosea wakati wa kujaza flot kwenye mashine yake hela ikaenda kwa wakala mwingine hela hairudi na wanakauli mbaya kuliko kawaida, mashine ikiibiwa mwizi akaenda kutoa hela yako hawana msaada kwa hilo, wao wakijisikia kuongeza huduma wanaongeza tu hamshirikishwi wala hujui utapewa sh. ngapi kwa ujumla hawajali chochote
 
na mashine mkiomba wanaweza toa hata mtaa mzima ukishindwa biashara ukarudisha mashine hawapokei labda upate wewe mteja umuuzie kwa hasara wana lugha mbaya hatari kila mtu pale ni kambale
 
Hivi ukiweka hela kwenye account ya mtu mwingine hata kwenye M-PESA wanarudishaga?
 
na mashine mkiomba wanaweza toa hata mtaa mzima ukishindwa biashara ukarudisha mashine hawapokei labda upate wewe mteja umuuzie kwa hasara wana lugha mbaya hatari kila mtu pale ni kambale
wewe kwasababu n cute umeanza kufananisha wenzako na kambale daaah....Kwel cute shy una kauli mbaya ana wewe
 
Awamu ya Tano tayari imeanza kumvunjia Mikataba Maxcom katika baadhi ya Idara za Serikali!

Usiigombanishe Awamu ya Tano na wafanyabiashara.

Mh. Rais hajaja kukandamiza wananchi wala wawekezaji,Serikali ya Awamu hii sio kama unavyowaza.

Umeanzisha thread iliyojaa upinzani kibiashara. @Jamiiforum Inatakiwa kukuchunguza usije ukawa umetumwa

/
 
Back
Top Bottom