Mawkili wanapojichukulia sheri mikononi

Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,705
1,288
Mwanasheria TAKUKURU amjeruhi shahidi



na Jumbe Ismailly, Iramba




SHAHIDI katika kesi ya kuomba na kupokea rushwa ya sh 600,000 inayomkabili Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mbelekese, wilayani Iramba, Singida, Iddi Mughenyi, juzi alipata kipigo kutoka kwa mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Iramba, kwa madai kuwa alimgeuka katika ushahidi alioutoa mahakamani hapo.

Mtuhumiwa alipata kipigo kutoka kwa mwanasheria huyo aliyetambulika kwa jina moja la Mchumi, kwa madai kwamba alimgeuka katika ushahidi aliuotoa mahakamani hapo.

Tukio hilo la aina yake limedaiwa kutokea muda mfupi baada ya Mughenyi kutoa ushahidi katika kesi namba 14/2009 inayomkabili ofisa mtendaji huyo.

Akizungumza kwa njia za simu kutoka Iramba, mmoja wa watumishi wa mahakama hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema kuwa kuna kila dalili kuwa ushahidi uliotolewa na shahidi huyo haukumridhisha mwanasheria Mchumi, kwa madai kwamba ulikuwa kinyume cha walivyokubaliana.

“Idd Mughenyi ni shahidi wa upande wa TAKUKURU kwenye kesi hiyo ambayo Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mbelekese anatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa, lakini juzi aliposimama kizimbani aliikana taasisi hiyo, kitendo ambacho kinawezekana kilimuudhi mwanasheria huyo ambaye ndiye alikuwa mwendesha mashtaka katika kesi hiyo,” alifafanua mtumishi huyo wa mahakama.

Aidha, mtumishi huyo alisema baada ya kesi hiyo kuahirishwa na kutoka nje ya mahakama, ndipo Mchumi alipomweka chini ya ulinzi shahidi huyo na kumtaka apande kwenye gari ili waende ofisi za TAKUKURU Wilaya ya Iramba.

Alisema kutokana na shahidi huyo kugoma kupanda gari kwa madai ya kutofahamu kosa, ndipo mwanasheria huyo alipoanza kumpiga makofi hadi kumuumiza kwenye jicho la upande wa kushoto na kumchania shati.

Alibainisha tukio hilo lilishuhudiwa na baadhi ya mahakimu, na kuongeza kuwa waliwaamru askari kwenda kuamua ugomvi huo, kisha kuwapeleka kituo cha polisi.
 
Pengine shahidi alichukuwa chochote kwa mshitakiwa akaamuwa kuwatosa TAKUKURU. Bongo hii hata mkulima anahitaji posho na itakapotoka ndiko atakapoegemea.
 
Bila shaka hilo ndilo lililotokea Bongo hii manufaa mbele.
 
Hii ndio inaonesha jinsi maadili yalivyoshuka kwa jamii. Yani kila mtu katika eneo lake anashindwa kutumia busara na sheria bali nguvu. Sasa huyu
Wakili naye anatakiwa ashitakiwe.
 
Hii ndio inaonesha jinsi maadili yalivyoshuka kwa jamii. Yani kila mtu katika eneo lake anashindwa kutumia busara na sheria bali nguvu. Sasa huyu
Wakili naye anatakiwa ashitakiwe.


Bado TAKUKURU atapeta kwa hali yetu ilivyo.
 
Hii ndio inaonesha jinsi maadili yalivyoshuka kwa jamii. Yani kila mtu katika eneo lake anashindwa kutumia busara na sheria bali nguvu. Sasa huyu
Wakili naye anatakiwa ashitakiwe.


Maadili na njaa ndugu yangu hayapo kuanzia mkulima hadi Wabunge.
 
Back
Top Bottom