Mawe ya msingi 'vituko'

Mawe ya msingi 'vituko'

MANILABHONA

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2015
Posts
462
Reaction score
351
Hivi karibuni mheshimiwa ametembelea mikoa kadhaa na kuweka mawe ya msingi katika miradi kadhaa. Kilichowashangaza wengi miradi hiyo ilianza mingi wakati wa serikali ya awamu ya tatu, nne na mingine ilishawekewa mawe ya msingi, mfano barabara fulani imeshawekewa jiwe la msingi upande mmoja na Raisi Kikwete, na juzi mheshimiwa ameweka tena jiwe la msingi upande mwingine. Miradi mingine ameweka mawe ya msingi wakati mradi umekaribia kukamilika(sio kuzinduai).Mawe ya msingi huwekwa wakati mradi unaanza kujengwa!!!!! Sasa sielewi kama yeye mwenyewe analijua hili au ni mchezo wa walioko chini yake kumrubuni kuwa kaanzisha miradi mipya? wampake mafuta kwa mgongo wa chupa au hakuna mradi wowote wa kuanzisha katika mikoa hiyo. Wewe walionaje hili?
 
Hilo hata mimi limenishangaza kidogo, mfano jana nilimsikia wakati anaweka jiwe la msingi Tabora, anasema ameona "Quotation" ya bilioni zaidi ya 100 kwenye barabara ya km 58 na kwamba haiwezekani kuwa bei hiyo (japo sijui alitumia vigezo gani kusema hiyo ni bei kubwa), kikawaida kama anaweka jiwe la msingi maana yake mkandarasi ameshapatikana na mkataba umeshasainiwa, kama contract imesainiwa hakuna namna yeyote ya kufanya negotiation kupunguza bei labda quantity zipungue.
 
Back
Top Bottom