Mawazo yenu tafadhali.

Mawazo yenu tafadhali.

mjanjamjanja

Member
Joined
Feb 11, 2014
Posts
32
Reaction score
2
Wadau kuna swali nataka kuuliza humu jf.Je mtu mwenye ukimwi anaruhusiwa kusafiri nje ya nchi.Nje ya Tz?
Nawasilisha.
 
mh....kaulize embassy ya nchi unayotaka kusafiri kuhusu sheria zao!nadhani inategemea na safari yako ni ya madhumuni gani kama kimasomo,kimatembezi n.k
 
Acha unyanyapaa .kwa hiyo kwa mawazo yako yote wote wanaosafiri nje ya nchi hawana ukimwi..?
 
Wenye ukimwi ni wengi sana na huwezi kuwatambua kwa kuwaangalia kwa macho na wanasafiri kwenda nchi mbali mbali. Kwa jibu sahihi ni kwamba wanasafiri.
 
kwani unataka kwenda wapi na umetoka wapi?
 
Mfano mtu anataka aende china kibiznez au Dubai.Au kwenda nchi za ulaya kwa ajili ya matembez.
 
Wadau kuna swali nataka kuuliza humu jf.Je mtu mwenye ukimwi anaruhusiwa kusafiri nje ya nchi.Nje ya Tz?
Nawasilisha.

Mi nafahamu kimasomo hususan kupitia scholarship kama unao ukimwi au hepatitis au magonjwa mengine waliyoorodhesha nchi husika basi unakosa hiyo fursa
 
Wadau kuna swali nataka kuuliza humu jf.Je mtu mwenye ukimwi anaruhusiwa kusafiri nje ya nchi.Nje ya Tz?
Nawasilisha.

Vua nguo .kakojoe. kaoge uwahi kulala. sheitwaani wewe ulishaenda kuomba viza wakakuomba kadi ya majibu ya vipimo vya umeme ? mwana izaya weye. Kama unao unaweza kabisa kwenda kutibiwa Nje.
 
Unaenda popote na ukimwi wako mkuu kamata frusa nenda zako
 
Nchi pekee ambayo ukienda kimasomo ama kukaa muda mrefu wanakufanyia medical examination na kukupima ukimwi kwa siri ni urusi. Otherwise hapo china wakinga kibao wapo wanaingia na kutoka kama nyuki mzingani
 
mh kwani pekee ndo wenye umeme?
 
Mfano mtu anataka aende china kibiznez au Dubai.Au kwenda nchi za ulaya kwa ajili ya matembez.

Kusafiri kibiashara kwa Dubai hakuna tatizo utapata visit visa na safari itakuwa haina tatizo lakini akitaka visa ya makazi(Residence Visa)haiwezekani maana mwombaji lazima apimwe kwenye hosipitali zao,Kwa Dubai ukiomba kazi /masomo ukakutwa una Ukimwi au Hepatitis B utajikuta upo ndani ya Emirates Airline tayari kwa safari ya kupelekwa ulipotoka na ukikutwa na Tb watakupa matibabu ukipona watakupa visa.Kuna rafiki yangu alipata kazi Dubai na mshahara ulukuwa $7000 kila kitu kilikuwa safi lakini kwenye vipimo alikutwa na HEPATITIS B ndio ukawa mwisho wa safari...lakini kusafiri kibiashara haina tatizo.
 
mkuu usiniambie kuwa toka uanze kuumwa hujawahi kusafiri!?
 
Ukiendanao ukumbuke kwenda nazana kwani ugundulika unao hutapa akamuulize waziri wakazi navijana wazamani juzi walimuzushia anao nabaada yahapo ikaripotiwa kua alisafiri nje ya nchi
 
Back
Top Bottom