Mawazo muda wote, nisaidieni pliz!

Mfarisayomtata

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
474
188
Jamani mi nlifiwa na girlfriend wangu mwaka jana mwezi wa 10 kwa ugonjwa wa moyo. Tangu amefariki sijisikii hata kuingia kwenye uhusiano tena manake naona kama namsaliti vle. Naombeni msaada nifanyeje ndugu zangu?
 
Pole sana! Tumia muda mwingi kujiweka busy na kazi,kuspend time na marafiki,usipende kukaa peke yako,epuka kufanya mambo uliyokua unafanya ukiwa na yeye..kadri siku zinavyokwenda utasahau..
 
Nashukuru sana kwa ushauri cartura. Ila mbaya zaidi hata kaburi lake sijaliona maana mimi nlikuwa huku masomoni na bado sijarudi Tanzania tangu muda huo. Huwa naumia sana kwa kweli.
 
Nimejitahidi kusali sana, kufanya mazozi ila wapi! Ila nashukuru sana kwa ushauri wako purple.
 
Nashukuru sana kwa ushauri cartura. Ila mbaya zaidi hata kaburi lake sijaliona maana mimi nlikuwa huku masomoni na bado sijarudi Tanzania tangu muda huo. Huwa naumia sana kwa kweli.

pole sana mkuu... jambo la kutia moyo ni kwamba sooner or latter everything will be over and you will be able to start a fresh page and enjoy your life once again...
 
unahitaji muda walau mwaka , mahusiano yapo . muenzi mwenzako nawe jipe muda wa maamuz
 
Jipe Muda , Huku ukimwomba Mungu Ukiingia haraka kwenye mahusiano mengine ni Rahisi sana kuumia na kushindwa kuendelea kwa sababu ya kulinganishaMuda wa kutosha kukufanya usahau ndio tiba
 
Ndugu, maisha ndivyo yalivyo, be strong...maisha lazima yaendelee mbele kufiwa na wapenDwa wetu inatokea katika maisha ya kila siku, najua ni ngumu sana,na naweza nikajaribu kuimagn wakati mgumu ulionao kipindi hiki, ILA USIRUHUSU UDHAIFU NA HUZUNI IKABADILI NA KUPOTEZA MWELEKEO WA MAISHA YAKO. ITS HARD BUT KUBALI KUWA MUNGU AMEMWITA NA UJIPANGE UPYA MAISHA YAKO BILA YEYE MAANA NI HAKIKA HAYUPO. POLE SANA.
 
pole sana kaka, ni mambo yanayowakuta wengi,na kwa hakika ni unforgettable memories... nilipokuwa o-level kulikuwa na dada aliyefiwa na BF wake kwa ajali.... she was unhappy kwa karibu miaka 5, na siku zote alikuwa alikia na kuvaa nguo nyeusi.... but baadae aliweza kumov on na ameolewa sasa... mungu atakutendea sawa nae!!
jaribu kutokuwa peke yako, spend time na marafiki...nenda kwenye michezo, na kama huchezi anza!! jichanganye na watu na tumia muda mwingi kutokuwa peke yako.... jipe muda pia usiingie kwenye mahusiano sasa!! hakika utapona na utarudi kama mwanzo....
lakini kubwa zaidi mwombe sana mola wako.... naamini hilo limetokea kwa sababu, naamini yeye anao mpango nawe... sali sana na mwambie mungu akuchagulie mchumba.. Pole sana!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom