Mawazo Mkakati ya Mwalimu Julius K. Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawazo Mkakati ya Mwalimu Julius K. Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chuwaalbert, Jul 7, 2012.

 1. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,054
  Likes Received: 1,440
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana jamvi, nimesoma Hotuba aliyoitoa Mwalimu Nyerere, wakati huo akiwa Rais, kwenye mkesha wa kuamkia 1.1.1970. Nawashirikisha sehemu yeke, maana hotuba yenyewe iko kwenye kijitabu chenye kurasa nyingi.

  Hatuwezi kungoja mpaka watoto wetu wamalize shule ndipo tupate maendeleo ya uchumi na maisha. Ni wajibu wa wale watu wazima wa nchi hii kuanza kazi hii ya maendeleo.

  Elimu ni kitu ambacho sisi wote tunapaswa kuendelea nacho toka siku ya kuzaliwa mpaka siku ya kuiacha dunia. Taifa ambalo watu wake hawajifunzi wala hawaotumii elimu yao, litabaki nyuma kwa kuwa maskini daima. Taifa hilo uhuru wake siku zote utakuwa katika hatari ya kumezwa na mataifa yenye elimu zaidi na nguvu zaidi, na watu wake daima watakuwa katika hatari ya kunyonywa na kukandamizwa na watu wengine.

  Elimu haiishi ukimaliza ulichosoma darasani. Tuna mambo mengi zaidi ya kujifunza juu ya kazi zetu na juu ya mambo ambayo tulipokuwa shule hatukupata nafasi ya kujifunza. Najua kuwa kuna wasomi wenzangu ambao sasa hawasomi kabisa. Nia yao ya kwenda shule ilikuwa kutafuta hati ambayo wangeweza kutumia kama hirizi kupata kazi. Baada ya kuipata hati hiyo kweli iliwapa kazi na sasa imetundikwa ukutani mahali ambapo kila mtu anaweza kuiona. Lakini kusoma sasa hawasomi kabisa. Hili ni kosa kubwa ambalo limetokana na mawazo ya kikoloni.

  Nchi nyingine zinatumia maarifa mapya ya kuzalisha mali na zinajitegemeza kwa faida yao wenyewe. Tusipoazimia kujielimisha tutaachwa nyuma. Uhuru wetu utategemea tu huruma za watu wengine na mataifa mengine, siyo uwezo wetu sisi wenyewe. Na uhuru wa kutegemea watu wengine si uhuru, ni kilemba cha ukoka.


  Source; Elimu haina Mwisho. Risala ya Rais kwa Taifa katika Mkesha wa Mwaka 1970.
   
 2. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  He was a real Great thinker!
   
 3. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huo ndiyo ukweli tunaopaswa kuufahamu zaidi sasa pengine kuliko wakati alipokuwa hai huyo msemaji wa maneno hayo..

  Tungeelewa ukweli huo, tusinge...
  (1) zunguka na bakuli la matonya mikononi mwetu
  (2) Tusingeficha pesa zetu kwa wazungu ili ziwaendeleze zaidi wao kuliko sisi
  (3) Tusingekaribisha wageni kumiliki kila kitu bila hata ya kulipa kodi
  (4) Tusingepuuzia elimu kwa vijana wetu .... ambao sasa hawaajiliwi katika mashirika ya wageni kwa sababu ya kupunguwa ubora unaohitajiwa..
  (5) ...
   
 4. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,054
  Likes Received: 1,440
  Trophy Points: 280
  Nyerere awalimjua MADUI aliyepigana naye, yaani UMASIKINI, UJINGA na MARADHI. JMK HAJUI chanzo cha umasikini wa nchi yake!
   
Loading...