Mawaziri wawili wapewa kibali cha kusafiri na Rais Magufuli

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Tangu Novemba 5 wakati Dk John Magufuli alipoapishwa, ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustine Mahiga pekee waliotoka nje ya nchi, lakini jana Rais aliwaruhusu mawaziri wengine wawili kusafiri nje.

Rais Magufuli alizuia safari za nje siku chache baada ya kuapishwa akisema watumishi wa umma watakaokuwa wakitaka kwenda nje watalazimika kuomba kibali kutoka Ikulu, ikiwa ni mkakati wake wa kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali.

Tangu wakati huo, safari za nje kwa watumishi wa umma zimekuwa za nadra na mawaziri wamekuwa wakifanya ziara za kwenda mikoani kufuatilia utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Jana, Rais Magufuli aliwaruhusu mawaziri wawili kwenda Vietnam kujifunza mbinu za kuinua kilimo na kujenga viwanda ili kuwaondoa Watanzania kwenye lindi la umaskini.

Mawaziri wawili waliopata kibali hicho ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba.
Rais Magufuli alitoa uamuzi huo jana baada ya kufanya mazungumzo na Rais Truong Tang Sang wa Vietnam juzi na kukubaliana kuweka sawa mazingira ya biashara na uwekezaji baina ya nchi zao.

Akizungumza jana baada ya kumtembeza Rais huyo kwenye Eneo Maalumu la Uwekezaji la Benjamini Mkapa (EPZ) lililopo Ubungo jijini hapa, Waziri Mwijage alisema Dk Magufuli ametoa kibali hicho baada ya kuridhishwa na mabadiliko ya muda mfupi ya Vietnam.

“Kutokana na hatua waliyopiga, Rais ameniruhusu mimi na Waziri wa Kilimo, Mwigulu Nchemba kwenda nchini humo muda mfupi baada ya Rais Truong kuondoka.

"Nitakwenda kujifunza mbinu zao ili sekta ya viwanda iajiri zaidi ya asilimia 46 ya vijana wa Kitanzania,”
alisema Mwijage.

Baada ya kuondolewa vikwazo na Marekani, Vietnam ilichagua kuendeleza maeneo maalumu ya biashara na kufanikiwa kujijenga kiuchumi na kufikia uchumi wa kati katika kipindi cha miaka 23.

Rais Truong alieleza kuwa waliwekeza Sh10 bilioni katika miradi na asilimia 80 ya fedha hizo ilielekezwa katika mauzo ya nje.

“EPZ zina mchango mkubwa kwenye uchumi wetu. Ninaamini, Tanzania inaweza kupata zaidi ya Dola 20 bilioni kwa mwaka itazipata kutoka katika maeneo haya.

"Hata sisi wakati tunaanza tulikuwa na EPZ chache lakini sasa tunazo nyingi na zinatuingizia dola 20 bilioni (za Marekani) kwa mwaka,”
alisema.

Pamoja na eneo hilo, Mwijage alisema Serikali ina mpango wa kuijenga Bagamoyo na kuifanya kuwa mji wa uwekezaji.

“Taratibu za kuwalipa wananchi ili kupisha eneo la kilomita 100 za mraba zimekamilika na ndani ya mwaka huu mchakato huo utahitimishwa kabla wawekezaji hawajaanza kukaribishwa,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa EPZ, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia alisema Serikali imeuagiza kila mkoa kutenga eneo la uwekezaji ili kuongeza idadi ya viwanda vilivyopo nchini.

“Kwa sasa EPZ zinaingiza kiasi cha dola bilioni moja za Marekani (zaidi ya Sh2 trilioni) kwa mwaka.Serikali kwa kushirikiana na Singapore imetenga dola 10 bilioni (zaidi ya Sh20 trilioni) ambazo zitatumika kujenga mji wa Bagamoyo,” alisema Kanali Simbakalia.

Mikoa mingine iliyotengwa kwa ajili ya kujenga EPZ ni Kigoma, Morogoro na Mtwara.
 
hivi wanaotakiwa kujifunza ni wanasiasa au wataalamu ni aibu kwa waziri kusema anakwenda kujifunza ndio maana tunaona maneno mengi kuliko vitendo.Kama wanataka kujifunza wangesoma azimio la arusha na kulielewa kwani hivyo viwanda wanavyozungumzia tulianza kuwa navyo kabla ya vietnam watafute sababu kwanini viwanda vyetu vilizorota na vietnam imepata mafanikio , data zote wanaweza kuzipata BOT badala ya kupoteza kodi za wananchi
 
Kilimo hatuna haja ya kujifunza nje.wataalamu wamejaa tele hatujaamua tu kuinua kilimo.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Safari moja huanzisha ingine....1)Majaliwa na Mahiga..2)Mwijage na Mwingulu...3) tusubiri watakuja
 
hivi wanaotakiwa kujifunza ni wanasiasa au wataalamu ni aibu kwa waziri kusema anakwenda kujifunza ndio maana tunaona maneno mengi kuliko vitendo.Kama wanataka kujifunza wangesoma azimio la arusha na kulielewa kwani hivyo viwanda wanavyozungumzia tulianza kuwa navyo kabla ya vietnam watafute sababu kwanini viwanda vyetu vilizorota na vietnam imepata mafanikio , data zote wanaweza kuzipata BOT badala ya kupoteza kodi za wananchi
Nafikiri tungemwomba Rais wa Vietnam atuletee exparts na consultants waje watushauri tufanye nini ili tupige hatua kama wao, kwenda huko sidhani kama kuna tija, kwanza jiografia ya vietnam na tabia za watu wao ni tofauti na za kwetu, pili huwezi enda wiki moja au mbili vietnam ukaja na weledi labda tupeleke maprofesa wa SUA.

Mkapa alipotaka kuanzisha mradi wa mabasi ya mwendo kasi alimleta mtaalamu mshauri prof mmoja kutoka Brazil laiti tungefuata ushauri wa Mkapa sasa hivi usafiri dar usingekuwa tatizo. Tuwale wa Vietnam watufundishie hapahapa.
 
hivi wanaotakiwa kujifunza ni wanasiasa au wataalamu ni aibu kwa waziri kusema anakwenda kujifunza ndio maana tunaona maneno mengi kuliko vitendo.Kama wanataka kujifunza wangesoma azimio la arusha na kulielewa kwani hivyo viwanda wanavyozungumzia tulianza kuwa navyo kabla ya vietnam watafute sababu kwanini viwanda vyetu vilizorota na vietnam imepata mafanikio , data zote wanaweza kuzipata BOT badala ya kupoteza kodi za wananchi

Mawaziri huwa wanasafiri na washauri na watalaamu wa sekta husika. Siyo lazima watajwe wote.
 
Mwanasiasa akienda kujifunza anapata experience ya kudanganya zaidi
Badala ya kupeleka mabwana shamba tunapeleka mawaziri ambao kwanza wako busy pili Uwaziri sio nafasi ya kudumu......lakini vyovyote iwavyo bwana shamba hiyo ndio fani yake na atazeeka nayo na tayari ana ujuzi kwenye hilo hivyo anaenda tu kukazia maarifa
 
Na wakirudi waje na ripoti ya walichojifunza ili ku justify safari yao...mboni tutanyooka....
Safari ziwe na malengo...
Safi sana JP<
 
Nchi hii bana.badala waende wataalam wa kilimo wanapeleka watu tofauti kabisa.labda hawa mawaziri wataambatana na maafisa kilimo.
 
Badala ya kupeleka mabwana shamba tunapeleka mawaziri ambao kwanza wako busy pili Uwaziri sio nafasi ya kudumu......lakini vyovyote iwavyo bwana shamba hiyo ndio fani yake na atazeeka nayo na tayari ana ujuzi kwenye hilo hivyo anaenda tu kukazia maarifa

Nadhani ni utashi wa kisiasa tu. Magufuri Haitaji kujifunza kitu hukoVEVE. Viatel (Hallotel) walivunja mkataba so Magu akataka kuitimua Jamaa ndio amekuja kupooza soo.
 
Back
Top Bottom