'Mawaziri Waonesha Ushabiki'

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Wazri Nape Nnauye akiwa amevalia jezi ya Mbeya City alipokuwa mgeni rasmi wa pambano baina ya Mbeya city na Coastal Union

nape na jezi ya RB battery.jpg


download (1).jpg

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia) akimkabidhi Baiskeli 120 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 22, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu kwa ajili ya kuwakabidhi makatibu wa matawi wa CCM Jimbo la Misungwi ili ziweze kutumika kwa ajili ya shughuli za chama jimboni humo. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi ya Wilaya ya Chama hicho, mjini Misungwi.
 
Mashabiki na viongozi wa Coastal Union wameonekana kutofurahishwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye kutinga jezi ya Mbeya City.
Nape alivaa jezi hiyo wikiendi wakati Mbeya City ‘ilipoitumbua’ Coastal Union kwa mabao 4-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Mashabiki hao walionekana wakipinga kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandaoni wakiamini haikuwa sawa.
Lakini pia walikuwa wakilalamika kuhusiana na suala hilo, wakidai kwamba wanataka kumuona pia akiwa amevaa jezi ya Coastal Union.
Hata hivyo, baadhi hasa mitandaoni nao wamekuwa wakipinga na kuamini hakuna jipya katika hilo na Nape anaweza kuvaa jezi yoyote anayotaka.
 
Back
Top Bottom