Mawaziri Wamshukia Vikali Mbunge aliyesema Nchi inakufa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,773
Filipo Mulugo Mbunge wa Songwe alinukuliwa alisema Nchi inakufa hii wakati akichangia taarifa ya CAG.

Wakijibi hoja Mawaziri wamemshukia Vikali Mbunge Mulugo Kwa Kauli yake hiyo kwamba ni dhihaka Kwa Rais na Nchi kusema Nchi inakufa wakati Kuna maelfu ya miradi yanatekelezwa na Nchi inaaminika kwenye jukwaa la Kimataifa.

Waziri wa Mipango Prof.Kitila na Nape wameoneshwa kutokubaliana na Kauli hiyo
DODOMA: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema, serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) haitetei wezi na ina historia katika kuwachukulia hatua wezi ambao wanabainika hata kama walikuwa ni viongozi wa serikali.

Mkumbo ameyasema hayo leo Novemba 4, 2023 bungeni mjini Dodoma na kudai kuwa hakuna Waziri anayeikataa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

“Kuna hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwemo viongozi waliobainika kwa wizi kufikishwa mahakamani na kufungwa na kuongeza kuwa utekelezaji wa jambo hilo halijaanza leo” amesema na kuongeza

"Tunaposimama kujibu hoja isionekane tunatetea majambazi, serikali ya CCM ilishawahi kuwafunga mawaziri, suala la kuwapeleka mahakamani wezi na majambazi kwa CCM halijaanza leo. Wapo mawaziri na makatibu wakuu walishafikishwa mahakamani, muhimu ni kwamba lazima sheria zifuatwe"amesisitiza.

Aidha, Prof. Mkumbo ameng’aka kuwa wanaodai nchi inakufa itakufaje wakati miradi mikubwa ya maendeleo inaendelea kujengwa.

“Kuna Mbunge anasema eti nchi inakufa, katika political science (Sayansi ya Siasa) ni failed state, unasemaje nchi inakufa wakati inajenga reli yenye urefu wa kilometa 2,600 kutoka Dar es Salaam hadi Karema?

Unasemaje nchi inakufa wakati imetoa Rais wa IPU (Umoja wa Mabunge Duniani)” amesema kwa kuhoji na kuongeza

“Nchi ambayo dunia nzima inaiamini na kukubali Spika wake awe ndio Rais wa IPU unasemaje inakufa?"

My Take
Mulugo msameheni tuu akichangia Kwa jazba.

Pili tunataka hatua za kuwaondoa watu kazini sio kusimamisha Wakurugenzi pekee huku mnawaacha Wakuu wa Idara.
---
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewasha moto bungeni na kudai kuwa hata kama kuna ubadhirifu wa fedha za umma kwa kiwango gani siyo sawa kusema nchi inaenda kufa.

Waziri Nape ameendelea kutoa ufafanuzi na kudai kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anapambana usiku na mchana kuleta maendeleo katika nchi hii kwahivyo kusema ni kumkosea Rais Samia.
 
Filipo Mulugo Mbunge wa Songwe alinukuliwa alisema Nchi inakufa hii wakati akichangia taarifa ya CAG.

Wakijibi hoja Mawaziri wamemshukia Vikali Mbunge Mulugo Kwa Kauli yake hiyo kwamba ni dhihaka Kwa Rais na Nchi kusema Nchi inakufa wakati Kuna maelfu ya miradi yanatekelezwa na Nchi inaaminika kwenye jukwaa la Kimataifa.

Waziri wa Mipango Prof.Kitila na Nape wameoneshwa kutokubaliana na Kauli hiyo.

View: https://www.instagram.com/p/CzOcz8bIPIA/?igshid=aWIwd3FhMTlmejVy

My Take
Mulugo msameheni tuu akichangia Kwa jazba.

Pili tunataka hatua za kuwaondoa watu kazini sio kusimamisha Wakurugenzi pekee huku mnawaacha Wakuu wa Idara.

View: https://www.instagram.com/reel/CzOIdccCuTf/?igshid=MWNlOWMwa3Y5YzE2cQ==

Wabunge wengi kwa kweli walijitahidi lakini hatuna Mawaziri tuna majangili tupu
 
Wapinzani ndani ya CCM ni hatari kuliko wa nje maana hao wanajua wanachohoji kuliko wale wengine wanaoropoka.

Nakumbuka Mpina aliwahi kusema, namnukuu " watendaji wanapuuza maagizo ya Waziri mkuu ", akatakiwa na Spika kuleta ushahidi alipoleta kimya" . Badala ya kumbeza Mulugo aambiwe athibitishe ili tutatue tatizo badala ya kukimbia
 
Filipo Mulugo Mbunge wa Songwe alinukuliwa alisema Nchi inakufa hii wakati akichangia taarifa ya CAG.

Wakijibi hoja Mawaziri wamemshukia Vikali Mbunge Mulugo Kwa Kauli yake hiyo kwamba ni dhihaka Kwa Rais na Nchi kusema Nchi inakufa wakati Kuna maelfu ya miradi yanatekelezwa na Nchi inaaminika kwenye jukwaa la Kimataifa.

Waziri wa Mipango Prof.Kitila na Nape wameoneshwa kutokubaliana na Kauli hiyo.

View: https://www.instagram.com/p/CzOcz8bIPIA/?igshid=aWIwd3FhMTlmejVy

My Take
Mulugo msameheni tuu akichangia Kwa jazba.

Pili tunataka hatua za kuwaondoa watu kazini sio kusimamisha Wakurugenzi pekee huku mnawaacha Wakuu wa Idara.

View: https://www.instagram.com/reel/CzOIdccCuTf/?igshid=MWNlOWMwa3Y5YzE2cQ==

MULUGO kasema kweli, wizi, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, kutokuwajibika, ukivurunda pale wapelekwa kule, kesi TAKUKURU zipo kwenye makaratasi tu....
Ulizeni Kwa watu hao viongozi wanavyojilimbikizia mali, kuanzia mabasi, malori, majumba, viwanja, magari...
Nendeni Dodoma muone walivyojirasimisha maviwanja...
Wanaobanika WANYONGWE tu, hiyo itakomesha huu UDHALIMU..
 
Filipo Mulugo Mbunge wa Songwe alinukuliwa alisema Nchi inakufa hii wakati akichangia taarifa ya CAG.

Wakijibi hoja Mawaziri wamemshukia Vikali Mbunge Mulugo Kwa Kauli yake hiyo kwamba ni dhihaka Kwa Rais na Nchi kusema Nchi inakufa wakati Kuna maelfu ya miradi yanatekelezwa na Nchi inaaminika kwenye jukwaa la Kimataifa.

Waziri wa Mipango Prof.Kitila na Nape wameoneshwa kutokubaliana na Kauli hiyo.

View: https://www.instagram.com/p/CzOcz8bIPIA/?igshid=aWIwd3FhMTlmejVy

My Take
Mulugo msameheni tuu akichangia Kwa jazba.

Pili tunataka hatua za kuwaondoa watu kazini sio kusimamisha Wakurugenzi pekee huku mnawaacha Wakuu wa Idara.

View: https://www.instagram.com/reel/CzOIdccCuTf/?igshid=MWNlOWMwa3Y5YzE2cQ==

Nchi haifi ila ccm ndoitakayokufa
 
Dawa ya Wezi wa fedha za Umma ni hii👇
giphy (2).gif
 
Back
Top Bottom