Hii nchi tukisema haina utawala bora ni sahihi kabisa. Mwekezaji kutoka Uturuki anapewa kuwekeza katika njia ya maji ya mto Mbezi ni kitu cha ajabu kabisa. Pale ni mkondo wa mto Mbezi na ule mto unahamahama pale sehemu ndio maana paliachwa palivyokuwa bila kuendeleza chochote.
Siku za karibuni Manispaa ya Kinondoni ilifika kuvunja eneo wanalojenga kwa sababu hawakutoa kibali cha ujenzi. Wakavunja tu matofali yaliyokuwa yanaongeza kina cha mtaro wa barabara ya Mwai Kibaki wakaondoka. Baadae mwekezaji akachangamka na sasa nasikia panafunguliwa tena na waziri sijui wa wizara ipi.
Hivi kweli wasomi wote wa nchi hii wamesoma au hawakusoma? Wataalamu wa mazingira wasingeruhusu mahali hapa kujengwa, serikali ya mtaa na kata wako wapi?
Hii ni yale yale ya mama Lwakatare kwenda kujenga kwenye lango la mto Ndumbwi unapoingia baharini kisa ni ile naye aseme anaishi beach! Viongozi wote wa nchi kuanzia rais wanajua hili lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa zaidi ya kusema kesi iko mahakamani; na huko mahakamani sijui kuna wafanyakazi wa aina gani kwani sijasikia hukumu yoyote juu ya hili.
Wa kulaumiwa zaidi niviongozi wa serikali ya Mtaa na Kata kwa kushindwa kusimamia maeneo yao vilivyo kwa kufuata sheria zilizopo! Huku wakitegemea kuchguliwa tena mwaka huu kuongoza mtaa. Aibu!
Hii ya ufunguzi nimeisikia kwenye redio na mimi mwenyewe napita pale darajani kila siku!