Mawaziri wa serikali ya Magufuli kuchunguzwa

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, atatumia muda mrefu kutangaza baraza lake la mawaziri endapo atashinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ili kujiridhisha kwamba watakaopita kwenye chujio ni wale wasio na kashfa, Raia Mwema, limeambiwa.

Taarifa hizi mpya zimekuja katika wakati ambapo tayari ametangaza kuunda jopo la wataalamu wazalendo wa masuala mbalimbali watakaomsaidia kufanya uchambuzi wa masuala muhimu anayoweza kuyatatua haraka mara atakapoanza urais. Vyanzo vya gazeti hili vilivyo karibu na Magufuli vimeeleza kwamba mgombea huyo anataka kutumia staili iliyotumiwa na Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, ambaye ametangaza baraza lake la mawaziri takribani miezi sita baada ya kushinda uchaguzi.

“Magufuli ameamua kwamba atachagua mawaziri ambao wataendana na kasi yake, wasio na kashfa na ambao wataweza kumudu changamoto za utawala wake. Ndiyo maana itabidi ajiridhishe kwa mengi. “Kama ikibidi, kuna uwezekano wa watu wanaotakiwa kupewa uwaziri kuchunguzwa kwanza na vyombo vya usalama kuhusu historia zao za huko nyuma na sasa. Wanahusiana na nani? Ni wasafi? Hawataichafua serikali yake? Yote hayo yatasababisha wapekuliwe kwenye maisha yao,” kilisema chanzo hicho ambacho ni sehemu ya timu ya kampeni ya CCM. Mjumbe huyo ambaye ni miongoni mwa wale wanaozunguka naye kwenye mikoa mbalimbali, alisema Magufuli amedhamiria kuunda serikali ambayo wananchi watakuwa na imani nayo kuanzia siku yake ya kwanza madarakani.

Katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania zinazoendelea hivi sasa, Magufuli amekuwa akisema kwamba anachukia rushwa na kwamba amedhamiria kuunda Mahakama Maalumu itakayokuwa ikishughulika na rushwa kubwa ambayo amekuwa akiita “Mahakama ya Majizi”. Raia Mwema ambalo ndilo pekee lililoweza kumhoji Magufuli tangu alipojitosa kwenye kinyang’anyiro hicho, linafahamu kwamba mgombea huyo tayari amejiwekea utaratibu wa kampeni ambao unamuepusha kukutana na watu ambao wana historia zenye utata. Gazeti hili linafahamu kuwa Magufuli, ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, hakutani na watu asiowafahamu au wenye kashfa za kifisadi kabla au baada ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea hapa nchini.

Mawaziri hao wapya watakaoteuliwa endapo Magufuli atashinda katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, watatakiwa kutekeleza mapendekezo mbalimbali ya kitaalamu ambayo jopo hilo la Magufuli litakuwa limeyafanyia uchambuzi.

Jopo hilo na hadidu zake za rejea ilizopewa lilitangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam. Makamba alizitaja hadidu hizo kumi za rejea kwa jopo hilo kuwa ni “Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo serikali itabana matumizi, ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari, ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa; “Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo serikali itaongeza mapato mara moja bila hatua za kibajeti kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa. Kuchunguza na kupendekeza maboresho makubwa katika mfumo wa utendaji na utumishi na ufanisi katika Serikali; “Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi zote, wakulima, wafugaji na wavuvi iwapo unaweza kurekebishwa bila kuathiri bajeti ya serikali inayotekelezwa sasa,” alisema Makamba.

Katika maeneo hayo ya awali, Magufuli inaonekana anataka kuongeza mapato ya serikali ili iweze kutoa huduma zaidi kwa wananchi na pia kupunguza matumizi ya serikali yasiyo ya lazima ili kutunisha mfuko wa serikali.

Masuala mengine ambayo jopo hilo la wataalamu litayaangalia kwa kina ni; “Kupitia sheria zote za nchi na kuorodhesha sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo ameyaahidi kwa Watanzania; “Kupitia na kuorodhesha masuala yote na kero zote zinazosubiri maamuzi ya Serikali ili atoe uamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa.

“Kupendekeza miundo na idadi ya Wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu na watendaji wengine wakuu atakaowateua mara baada ya kuapishwa. “Kupendekeza njia za haraka za kumaliza kero za watumishi wa umma, hasa walimu, askari, madaktari na wauguzi, ili aanze nao kazi wakiwa na ari na morali ya kusukuma mabadiliko ya kweli. “Kutengeneza rasimu ya mpango-kazi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi alizozitoa kwenye kampeni, hasa upatikanaji wa ajira kwa haraka na umeme wa uhakika. “Kupendekeza muundo wa kitaasisi na utaratibu muafaka wa kutekeleza ahadi ya kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa nchini,” alisema Makamba.

Kwa kutazama hadidu hizo za rejea kwa jopo alilounda Magufuli, inaonekana kuwa mgombea huyo wa CCM ana lengo la kupunguza ukubwa wa baraza lake la mawaziri kama anavyoahidi katika wakati huu wa kampeni. Hadidu hizo za rejea kwa jopo zinaonyesha kuwa Magufuli pia anataka kuwa na suluhisho la kudumu la matatizo ya ajira nchini pamoja na suala la matatizo ya umeme yanayogubika taifa hivi sasa. Katika historia ya siasa za Tanzania, Magufuli atakuwa mgombea wa kwanza wa nafasi ya urais ambaye ataingia madarakani wakati tayari akiwa na picha ya nini anatakiwa kufanya kuibadilisha nchi kwa mujibu wa maelekezo ya wataalamu wa ndani.

Baadhi ya wasomi kama Profesa Issa Shivji wamekuwa wakilaumu kwamba baadhi ya mipango ya kuikwamua Tanzania kutoka ilipo imekuwa haifanikiwi kwa sababu imekuwa ikiandaliwa na wataalamu kutoka nje ya nchi ambao hawajui maslahi ya taifa letu wala mazingira yake.

Kwa hisani ya RaiaMwema.
 
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage katika Hotuba zake aliwahi kusema kuwa Vyama vinatakiwa kutoa Mgombea ambaye anakidhi Matarajio ya Wananchi wote na Siyo matarajio ya wewe mpiga kura.

Mwl. Nyerere alisema, '' Mgombea mtakae mteua lazima tumtetee, Lakini inatakiwa ukiulizwa swali, huyu atatusaidia kupiga rushwa vita?, jibu litoke ndani ya roho yako. Hapana hapa tu (mdomoni). Kwamba NDIYO, anaweza''.

Mwl. Nyerere akaendelea kusema, '' sasa watu wanazungumza dini, udini bila haya bila aibu , wanajitapa kwa udini. Tunataka mtuchagulie mgombea ambae atatusaidia kuondoa mawazo haya ya kipumbavu katika nchi yetu. Na ukiulizwa na wananchi Watanzania kwa dhati, mnadhani mgombea huyu analiona hilo kwa uchungu kabisa kama mnavyoliona nyinyi? Useme NDIYO. Uweze kujibu kwa dhati kabisa kwamba ndiyo''.
 
Agenda ya mwaka huu ni kuondoa umaskini, mgombea anayeonyesha kuuchukia umaskini kwa vitendo ni Lowassa pekee. Tumechoka kuona wanawake wetu wanateseka wakati wa kujifungua, tumechoka barabara za vumbi dawa ni Lowassa tu
 
Umasikini utauondoa kwa naneno?

Lowassa anachukia umasikini wake na siyo umasikini wa Watanzania wengine.

Kama kweli angekuwa anachukia umasikini wa wananchi tungeona hata ishara katika jimbo alilokuwa Mbunge kwa zaidi ya miaka 30.

Sensa ya watu na makazi 2012 imeonyesha Monduli ni moja ya jimbo lenye wananchi masikini sana wa elimu na kipato ukilinganisha na sehemu zingine nchini.

Charity begins at home!

Ajenda kuu ya uchaguzi huu ni rushwa na ufisadi katika msingi wa mabadiliko ya kweli.
 
umeona eeee!!!! singidadodoma, Tatizo watanzania wengi ni wavivu hututaki kufanya kazi ila tunataka maendeleo,Maendeleo gani yatakuja bila kufanya kazi?Maendeleo ya kweli yataletwa na watanzania kwa kufanya kazi kwa bidii!!! na si maneno tuuu halafu umekaa kijiweni!!
 
Si ungechangia tu vizuri jamani sasa Singida na Dodoma wavivu imetoka wapi mbona wengi wanakimbilia kuoa Singida white na Dodoma brown kama ni wavivu si ingekuwa tabu, Yaani nyie mnataka wahaya tu
 
Watanzania tusikubali kuimbishwa wimbo ambao hatujui mtunzi wake alikuwa na masilahi gani na huo wimbo,Utamsikia kijana anaimbishwa "Lowasa na yeye anaitikia Mabadiliko"wewe unayajua mabadiliko anayo yasema Lowasa!!!?
 
Serikali ya magufuli itakuwa ni kazi tu mtu,,,magufuli rais bora ambaye hata sahaurika
 
Agenda ya mwaka huu ni kuondoa umaskini, mgombea anayeonyesha kuuchukia umaskini kwa vitendo ni Lowassa pekee. Tumechoka kuona wanawake wetu wanateseka wakati wa kujifungua, tumechoka barabara za vumbi dawa ni Lowassa tu

Hapo umedanganyika sana, Fisadi na nwizi wanazidisha umasikini, Lowassa sio msafi hata siku moja.

Chadema wameingiza Gari bovu kwenye mashindano ya Grand Pri
 
Hii ni shidaaa. Kwa hiyo anagombea urais wakati hajui ni nini cha kufanya?

Halafu hao mawaziri si watatokana na wabunge wa CCM? Kama ni hivyo wakati wa kura za maoni wagombea wote wa CCM walitoa rushwa kwa njia moja au nyingine. Wengine kwanza ni wapiga debe wakubwa walihojiwa na TAKUKURU. Sasa hao mawaziri wasafi watatoka wapi?

Magufuli mwenyewe kama waziri, wizara yake ya Ujenzi imeripotia na CAG kufanya malipo yenye utata. Hii ina maana alishindwa kusimamia vizuri hiyo wizara. Sasa haweza vipi kusimamia nchi yote?
 
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, atatumia muda mrefu kutangaza baraza lake la mawaziri endapo atashinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ili kujiridhisha kwamba watakaopita kwenye chujio ni wale wasio na kashfa, Raia Mwema, limeambiwa.

Taarifa hizi mpya zimekuja katika wakati ambapo tayari ametangaza kuunda jopo la wataalamu wazalendo wa masuala mbalimbali watakaomsaidia kufanya uchambuzi wa masuala muhimu anayoweza kuyatatua haraka mara atakapoanza urais. Vyanzo vya gazeti hili vilivyo karibu na Magufuli vimeeleza kwamba mgombea huyo anataka kutumia staili iliyotumiwa na Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, ambaye ametangaza baraza lake la mawaziri takribani miezi sita baada ya kushinda uchaguzi.

“Magufuli ameamua kwamba atachagua mawaziri ambao wataendana na kasi yake, wasio na kashfa na ambao wataweza kumudu changamoto za utawala wake. Ndiyo maana itabidi ajiridhishe kwa mengi. “Kama ikibidi, kuna uwezekano wa watu wanaotakiwa kupewa uwaziri kuchunguzwa kwanza na vyombo vya usalama kuhusu historia zao za huko nyuma na sasa. Wanahusiana na nani? Ni wasafi? Hawataichafua serikali yake? Yote hayo yatasababisha wapekuliwe kwenye maisha yao,” kilisema chanzo hicho ambacho ni sehemu ya timu ya kampeni ya CCM. Mjumbe huyo ambaye ni miongoni mwa wale wanaozunguka naye kwenye mikoa mbalimbali, alisema Magufuli amedhamiria kuunda serikali ambayo wananchi watakuwa na imani nayo kuanzia siku yake ya kwanza madarakani.

Katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania zinazoendelea hivi sasa, Magufuli amekuwa akisema kwamba anachukia rushwa na kwamba amedhamiria kuunda Mahakama Maalumu itakayokuwa ikishughulika na rushwa kubwa ambayo amekuwa akiita “Mahakama ya Majizi”. Raia Mwema ambalo ndilo pekee lililoweza kumhoji Magufuli tangu alipojitosa kwenye kinyang’anyiro hicho, linafahamu kwamba mgombea huyo tayari amejiwekea utaratibu wa kampeni ambao unamuepusha kukutana na watu ambao wana historia zenye utata. Gazeti hili linafahamu kuwa Magufuli, ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, hakutani na watu asiowafahamu au wenye kashfa za kifisadi kabla au baada ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea hapa nchini.

Mawaziri hao wapya watakaoteuliwa endapo Magufuli atashinda katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, watatakiwa kutekeleza mapendekezo mbalimbali ya kitaalamu ambayo jopo hilo la Magufuli litakuwa limeyafanyia uchambuzi.

Jopo hilo na hadidu zake za rejea ilizopewa lilitangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam. Makamba alizitaja hadidu hizo kumi za rejea kwa jopo hilo kuwa ni “Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo serikali itabana matumizi, ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari, ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa; “Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo serikali itaongeza mapato mara moja bila hatua za kibajeti kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa. Kuchunguza na kupendekeza maboresho makubwa katika mfumo wa utendaji na utumishi na ufanisi katika Serikali; “Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi zote, wakulima, wafugaji na wavuvi iwapo unaweza kurekebishwa bila kuathiri bajeti ya serikali inayotekelezwa sasa,” alisema Makamba.

Katika maeneo hayo ya awali, Magufuli inaonekana anataka kuongeza mapato ya serikali ili iweze kutoa huduma zaidi kwa wananchi na pia kupunguza matumizi ya serikali yasiyo ya lazima ili kutunisha mfuko wa serikali.

Masuala mengine ambayo jopo hilo la wataalamu litayaangalia kwa kina ni; “Kupitia sheria zote za nchi na kuorodhesha sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo ameyaahidi kwa Watanzania; “Kupitia na kuorodhesha masuala yote na kero zote zinazosubiri maamuzi ya Serikali ili atoe uamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa.

“Kupendekeza miundo na idadi ya Wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu na watendaji wengine wakuu atakaowateua mara baada ya kuapishwa. “Kupendekeza njia za haraka za kumaliza kero za watumishi wa umma, hasa walimu, askari, madaktari na wauguzi, ili aanze nao kazi wakiwa na ari na morali ya kusukuma mabadiliko ya kweli. “Kutengeneza rasimu ya mpango-kazi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi alizozitoa kwenye kampeni, hasa upatikanaji wa ajira kwa haraka na umeme wa uhakika. “Kupendekeza muundo wa kitaasisi na utaratibu muafaka wa kutekeleza ahadi ya kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa nchini,” alisema Makamba.

Kwa kutazama hadidu hizo za rejea kwa jopo alilounda Magufuli, inaonekana kuwa mgombea huyo wa CCM ana lengo la kupunguza ukubwa wa baraza lake la mawaziri kama anavyoahidi katika wakati huu wa kampeni. Hadidu hizo za rejea kwa jopo zinaonyesha kuwa Magufuli pia anataka kuwa na suluhisho la kudumu la matatizo ya ajira nchini pamoja na suala la matatizo ya umeme yanayogubika taifa hivi sasa. Katika historia ya siasa za Tanzania, Magufuli atakuwa mgombea wa kwanza wa nafasi ya urais ambaye ataingia madarakani wakati tayari akiwa na picha ya nini anatakiwa kufanya kuibadilisha nchi kwa mujibu wa maelekezo ya wataalamu wa ndani.

Baadhi ya wasomi kama Profesa Issa Shivji wamekuwa wakilaumu kwamba baadhi ya mipango ya kuikwamua Tanzania kutoka ilipo imekuwa haifanikiwi kwa sababu imekuwa ikiandaliwa na wataalamu kutoka nje ya nchi ambao hawajui maslahi ya taifa letu wala mazingira yake.

Kwa hisani ya RaiaMwema.[/QUO

Who told him that he will win this upcoming election?

He will never be a president of this country bacause the fate is not with him, trust me!!

So he and his companions should better stop being paranoid!!
 
Watanzania tusikubali kuimbishwa wimbo ambao hatujui mtunzi wake alikuwa na masilahi gani na huo wimbo,Utamsikia kijana anaimbishwa "Lowasa na yeye anaitikia Mabadiliko"wewe unayajua mabadiliko anayo yasema Lowasa!!!?
Lowassa anasema atapambana na umasikini lakini hataki kufahamu kama moja ya kikwazo cha kupambana na umasikini ni rushwa na ufisadi.

Huwezi kumsikia akitamka neno ufisadi kwa sababu itakuwa ni kama kujipiga risasi mwenyewe.

Kampeni za Lowassa na genge lake zimejaa usanii wa kiwango cha juu.
 
Hapo umedanganyika sana, Fisadi na nwizi wanazidisha umasikini, Lowassa sio msafi hata siku moja.

Chadema wameingiza Gari bovu kwenye mashindano ya Grand Pri

Je,ni kwa nini Serikali ya CCM imeshindwa kumchukulia hatua stahiki huyo mnayemwita mwizi na fisadi!?
Kasha nyingi za ufisadi mkubwa,wahusika wakubwa si ndio viongozi wakubwa wa ccm na serikali!?Je,wamewekwa kando na kuchukuliwa hatua au ndio hao hao wanaonadiwa majukwaani na kuitwa majembe na matingatinga?
Hakika wewe na wenzako ni wanufaika na wafaidikaji wakubwa wa elimu duni ya kumdumaza mtanzania kiakili ya ccm.
 
juzi wakati amekuja mkoa wa Mara eneo la sirari lowasa amepanda jukwani kuomba kura kwa wananchi za urais kaomba vizuri tu kasheshe alipokuja udiwani na ubunge eti mnichagulie na madiwani na wabunge wa CCM...hivi huwa anafanya makusudi au? sasa huyu ndio wa kumpa urais kweli au tunacheza kamali
 
Back
Top Bottom