tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,490
Ukilisikiliza kila siku Bunge kutoka upande wa Mawaziri wakijibu maswali na hata Bajeti zao mipango ya wizara zao wanakuwa wanaongelea mikakati,mipango,ahadi kwa asilimia kubwa kuliko utekelezaji wa mambo ambayo yanafanyika au hata kukamilika utekelezaji wake.
Wakati wenzetu majirani wa Africa Mashariki wakieleza utekelezaji wa mipango yao na kuweka mambo hadharani sisi bado tunaongea sana maneno mengi sana na mipango mingi sana lakini kasi ya utekelezaji ni kwa mwendo wa konokono.
Kuna haja hata ku review mikutano ya Bunge kama ina tija hasa Mkutano wa Bajeti kukaa miezi mitatu huko ukisikiliza hotuba za Mawaziri ni muendelezo ule ule tu miaka yote...utekelezaji wa bajeti zilizopita unakuta uko chini ya 50% kiukweli sioni sababu ya kukaa muda wote wa siku 90 huko outcome ya kukaa huko ni chini ya 50%.