Mawaziri wa JK wagongana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri wa JK wagongana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by graceirene, Sep 13, 2011.

 1. g

  graceirene Member

  #1
  Sep 13, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  • Mawaziri wa JK wagongana
  • Kushtakiwa mahakama ya kimataifa

  na Mwandishi wetu

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]MAWAZIRI wawili wa serikali ya Rais Kikwete wametoa kauli za kupingana kuhusiana na sakata la sheria mpya ya wanyamapori ambayo ilipingwa vikali na wabunge wa kambi ya upinzani bungeni na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii nchini.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ndiye aliyetoa kauli inayopingana na ile ya Waziri wa Mali asili na Utalii, Ezekiel Maige, ambaye wakati akiwasilisha hotuba yake katika kikao cha Bunge la Bajeti mwaka huu, alisema sheria ya uwindani haikuwa na matatizo, lakini majuzi Waziri Membe amesema ina matatizo na lazima ifanyiwe marekebisho.
  Waziri Membe amekiri kuwa sheria hiyo ni ya kibaguzi kwa kuwa inawabagua Watanzania walionunua hisa kuanzia asilimia 25 kwenye makampuni ya kigeni.

  Akiongea na waandishi wa habari katika hoteli ya kitalii ya Mount Meru jiji hapa kuhusu msimamo wa serikali juu ya athari zinazoweza kusababishwa na sheria hiyo kimataifa, Membe alisema kuwa wamekubaliana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, kuwa sheria hiyo ijadiliwe kwenye baraza la mawaziri kabla ya kurudishwa bungeni kwa ajili ya kurekebishwa.
  "Lazima sheria iseme endapo mtu wa nje anaendesha kampuni yake kwa ubia na Mtanzania, kampuni hiyo itapewa fursa sawa na makampuni mengine ya wazalendo," alisema Membe.

  Hata hivyo, wakati Membe akisema hayo, sheria hiyo imeshaanza kutumika na ugawaji wa vitalu vya utalii ulishafanyika ambapo kwa mujibu wa tangazo la wizara makampuni 51 yanayoendeshwa kwa ubia kati ya Watanzania na wageni yakinyimwa vitalu.
  Waziri Membe alionekana kushangaa alipoambiwa juu ya habari ya kugawiwa kwa vitalu kwa mujibu wa sheria hiyo na kuidhinishwa na waziri mwenzake na kuomba apewe muda kulifuatilia zaidi suala hilo.

  Katika ugawaji huo wa vitalu uliotangazwa katikati ya wiki, makampuni ya Kitanzania 51 yaligawiwa vitalu kati ya makampuni 60 yaliyoomba ikiwa ni asilimia 85 ya makampuni yote ya uwindaji hapa nchini ambapo makampuni tisa tu yanayoendeshwa kwa ubia kati ya Watanzania na wageni ndiyo yaliyogawiwa vitalu.
  Mapungufu ya sheria hiyo ya mwaka 2009 yamepigiwa kelele na wadau wa sheria hapa nchini na Watanzania waliowekeza kwenye makampuni ya kigeni na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Hata hivyo tayari makampuni yanayoendeshwa kwa ubia kati ya Watanzania na wageni yalishaeleza wazi kuwa endapo sheria hiyo haitarekebishwa wako tayari kufunga shughuli zao hapa nchini sanjari na kuishtaki serikali kwenye mahakama ya usuluishi ya kimataifa nchini Ufaransa.
  Kuondoka kwa makampuni hayo 18 kutaisababishia serikali kukosa mapato yasiyopungua dola milioni 70 kutokana na kodi huku Watanzania zaidi 5,000 wakiachwa bila ajira.
  "Sisi tumetumia mamilioni ya fedha kuwekeza kwenye vitalu hivyo; tumejenga miundo mbinu ikiwemo viwanja vya ndege , barabara na kutunza wanyama kwa ajili ya kuwinda leo wanatuambia makampuni yanayopewa vitalu ni tisa tu bila kuangalia kiasi cha fedha tulichowekeza kwenye maeneo hayo kwa kweli tunaangalia namna ya kwenda kuishtaki serikali ya Tanzania kwenye mahakama ya usuluishi ya kimataifa nchini Ufaransa kudai fidia," walisema baadhi ya wawekezaji wazawa ambao hawakuwa tayari majina yao kuandikwa magazetini.

  "Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye amepewa madaraka ya kuandaa kanuni na sheria anaweza kuondoa mgongano huo wa kisheria kwa kuweka mgawo wa umiliki kuwa asilimia 50 kwa wageni na wazawa badala ya sasa kutaka kampuni zingine zinazomilikiwa na wageni na wazawa kuondoka nchini," walishauri wawekezaji hao.
  Hivi karibuni akiwasilisha hotuba ya kambi ya rasmi ya upinzani bungeni, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, aliishauri serikali kuifanyia marekebisho sheria hiyo kabla haijaanza kutumika huku akimtaka waziri kuivunja kamati ya kumshauri juu ya ugawaji vitalu vya uwindaji aliyoiteua kwa kile alichosema kuwa hakuzingatia matakwa ya sheria katika uteuzi huo.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Serikali ikiwa na msimamo mmoja haiwezi kuyumbishwa Lakini kama kila Waziri ana mtazamo wake watayumbishwa sana.
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  waendelee KUGONGANA
   
 4. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  vita vya panzi furaha kwa kunguru!
   
 5. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni vijikosa vidogo tu katika utendaji na vinarekebishika
   
 6. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sasa CHADEMA si ndiyo panzi wenyewe. Mbona mfano hauendani kabisa.
   
 7. S

  Simcaesor Senior Member

  #7
  Sep 13, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni haibu sana, sijui tuziweke wapi sura zetu na hawa mawaziri ambao wanashindwa kujua mambo sahihi na yapi siyo sahihi... lakini hii ni kwasababu hakuna mawasiliano kati ya wizara moja na nyingine, pia hakuna ushirikiano zaidi mawaziri hawajui wanachokifanya wanapelekwa tu na watendaji matokeo yake wajui mambo kwa kina wanafahamu juujuu tu....
   
 8. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  napita tuu
   
 9. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mawaziri wote wa serikali ya Kikwete wanafuata nyayo za mkubwa wao kwa kushindana kujilimbikizia mali ; kila mmoja anatafuta nafasi katika wizara yake au nyingine yeyote ili apate upenyo wa kupewa rushwa. Huyu Membe anataka kulifanya zoezi la kugawa vitalu ni la kimataifa simply because wawindaji na wamiliki wengi ni wakutoka nchi za nje, hivyo nae anataka sauti yake isiskike katika maamuzi na ndio iwe chambo cha kuvuta mkwanja kumsaidia kupata Urais 2015!!. Ugawaji vitalu ni kazi ya wizara ya Maliasili na Utalii yeye inamhusu nini? wageni wakija kwetu ni lazima wafuate sheria zetu kama hawawezi warudi kwao!!
   
 10. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Vipi mbona hujibu meseji zangu?
   
 11. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  si ameshagundua we ni mpuuzi.................huh
   
 12. W

  Wan chai Member

  #12
  Sep 13, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ajibu nini?? hakuna hoja ya kujibu hapo.
   
 13. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  magamba yakiwa kazini lazima yagongane tu
   
Loading...