Mawaziri wa chama kimoja,serikali moja wanapopinga hadharani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri wa chama kimoja,serikali moja wanapopinga hadharani!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KakaKiiza, Jan 9, 2011.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Nijambo linaloshangaza kuona mawaziri wa serikali moja,chama kimoja wakianikana hadharani!
  Kitendo cha Mh Samwel Sitta kumpinga Waziri Ngereja kinaonyesha Ujasiri wa Sitta aliokuwanao katika medani ya siasa Nakinaonyesha Dowans si kampuni halali hivyo haikupaswa kulipwa!Na inaonyesha mwanasheria wa serikali ni mla rushwa kwakushindwa kusimamia ofisi yake!!
   
 2. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,522
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Ni haki yao lakini
   
 3. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Hapo mweye haki ni mmoja mchukia ufisadi!!
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndio Demokrasia iliyojengwa na JMK.

  Ungekuwa ni mfatiliaji wa habari, duniani, wengi tu huwa wa chama kimoja lakini wakatofautiana mawazo, hata wakati wa chama kimoja hapa Tanzania, na udikteta wote wa Nyerere lakini wapo waliompinga, wengine aliwaficha, wengine wakakimbia nchi, wengine wapo mpaka leo, hohehahe.
   
 5. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Uturuki zinapigwa katikati ya bunge!
   
 6. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Unajua Mzee Sita anaelewa vizuri sana issue ya DOWANS hivyo si rahisi kumdanganya kama Ngereja anavyojaribu kutudanganya Watanzania. Kumbuka Dr. Mwakyembe alisema mambo mengine wameyaacha kwa usalama wa nchi lakini Sitta kama Speaker anayafahamu. Anasema anachokifahamu!!!

  Binafsi naona Sitta yuko kwenye nafasi nzuri sana ya kutetea hoja zake kuliko AG Werema na Ngereja. Werema yeye alipitia hukumu tu na kutoa maoni yake bila kufuatilia historia ya tatizo lenyewe. AG yuko sahihi kwa mtazamo wa haraka jinsi hukumu ilivyo lakini ameshindwa kupata ukweli sahihi na kutoa maamuzi yenye maslahi kwa Watanzania kwa kukosa kufuatilia majadilano ya Bunge na taarifa za kamati ya Bunge. Hapo ndo alipopotoka ndugu Werema.
  Ngereja anaangaishwa na ujana wa kutetea maslahi ya Wazee. Ameangukia pua na hana utetezi.
   
 7. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Keep close tracking before 2015! ...then youll see JK surprise!
   
 8. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  May Be if not Du
   
 9. m

  mzambia JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Sijui nini kinaendelea!!!!!
   
 10. m

  mpingomkavu Member

  #10
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kupingana kwa hoja kwa maslahi ya taifa ndiyo demokrasia siyo eti usubiri mpaka vikao vya cha ili iwe siri hapo kuna kuwa hakuna kuwatendea wananchi haki waache wananchi wajue nini serikali yao inakifanya
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hii imetulia tehe tehe tehe! Maana ujinga umezidi sana serikalini na unasababishwa na wajinga wachache!
   
 12. Gottee

  Gottee Senior Member

  #12
  Jan 9, 2011
  Joined: Sep 7, 2008
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Labda kama mnakuwa wepesi wa kusahau. Huyu Ngeleja kabla hajaingia medani ya siasa alikuwa ni mwanasheria wa Vodacom Tanzania. Kampuni hii RA ana shea kubwa tu. Ngeleja kuwekwa pale sio jambo la kubahatisha. RA ni mtu ambaye amemchomeka pale kwa maslahi yake binafsi. Kama mnakumbuka hata Lau Masha aliamua kumsafisha Bashe kwamba ni raia halali wa Tanzania wakati Mwenyekiti wake wa CCM ambaye ndiye Rais wa serikali yake alishatamka Bashe si raia wa TZ. Kitendo alichikifanya Masha kilikuwa kinamdhalilisha Rais, lakini Rais alielewa Masha alifanya vile kwa maelekezo ya RA ambaye kimsingi naye ni bosi wake. Ukianza kuwaangalia hawa Mawaziri wetu na hasa lile Baraza la kwanza la JK utaona wengi walichomekwa na RA. Watu kama akina Zakia Meghji, Zakia ilimgharimu hata maisha yake ya kisiasa kwa kudanganya umma. Akina Nchimbi, Karamagi na wengine. Jamani siku moja moja tuwe tunakumbuka maneno ya Mwalimu hata kama yeye tumeshamsahau. Mwalimu alisema Ikulu ni mahali patakatifu na sio pango la wafanyabiashara. Na aliendelea kusisitiza ukiona mtu anataka kuingia Ikulu kwa 'Mbinde na fedha' huyo ni wakuogopwa kama ukoma. Hivi mkichukulia zile kashfa za EPA, Kagoda, Meremeta nk hizi si ndio zilimuingiza Muungwana Ikulu. Amini usiamini maisha yote ya Muungwana pale Ikulu yamekuwa na yatakuwa ni ya kulipa fadhila. Hivi kwa nini muungwana hatumwogopi kama UKOMA? Au kwa kuwa ile sura INALIPA? Acheni bana!
   
 13. V

  Vipaji Senior Member

  #13
  Jan 9, 2011
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TATIZO SI KUTOFAUTIANA TU BALI NI KUNYIMANA MGAWO WA FEDHA ZINAZOPATIKANA KUTOKANA NA UFISADI; MFANO FEDHA ZILIZOPATIKANA KATIKA MIRADI YAO KAMA ALIVYOTOA RIPORT ROSTAM AZIZI KUWA KWA MIEZI MINNE TU WANAWEZA KUKUSANYA BILION 185 Tsh. ndiyo maan a wanatofautia. lakini kutofautiana kwao ndiyo mwanzo wa mafanikia kwa wapigania haki ya watanzania.
   
 14. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  JK avunje tu baraza la mawaziri, kwani halina umoja.. Kila mtu anafanya anachojua yeye, ukiangalia kauli ya Sita Vs Ngeleja, Waziri mkuu Vs Werema na Celina Kombani, kazi iliyofanywa na Nahodha na Mwema kule Arusha Vs Masikitiko ya JK kuhusu tukio hilo
   
 15. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikikutana na michango yako ya Bwana Zomba humu ndani kila wakati lakini wakati mwingine najiuliza hivi kama kila mtu angepima tija ya maneno na michango yake humu sijui kama ni kweli Bwana ZOMBA angepoteza muda wake kuchangia mambo ki-rahisi kama anavyofanya kwasasa na kwa maneno mepesi kiasi hicho? Ebu angalia moja ya mchango wake juu HOJA iliyoruswa kwa kichwa cha habari " Mawaziri wa chama kimoja,serikali moja wanapopinga hadharani - JUU ya swala la Dowans!"

  Napata tabu sana kujibu moja kwa moja kama ZOMBA anatumiwa kupotosha Jamii au la!, labda yeye mwenyewe ajaribu kutoa jibu; maana mimi simuelewi, kama ni uwezo mdogo au anatumika, ila kama jibu ni kuwa anatumika basi mimi ndio nakosea samahani sana, tija hapo ipo na inapimwa na aliyemtuma kulingana na vigezo vya mambo anayomtuma kufanya humu JF, lakini kama jibu ni uwezo mdogo; mimi namshauri ajaribu kupanua uwezo wake na fikra zake shule zipo, taarifa zipo na vitabu vipo, hii itamsaidia sana.

  Ebu tazama hii hoja yake hapo juu
  Hili swala la dowans si la kutofautiana mawazo Ndg. Zomba, swala la Dowans si hoja ya Siasa wala Itikadi ya Ki-siasa ili watu watofautiane mawazo na mtizamo! hili ni suala la ki-ushahidi, uelewa juu ya ukweli halisi, mathalani, kama Bwana XYZ ana-jinsia ya kiume lakini anavaa sketi, maumbile yako na mambo yako yote ni ya kiume, Doctor wake anajua yeye ni mwanaume kasoro mavazi! wazazi wake pia wajua ni mwanaume kasoro mavazi; watu wakibishana juu ya jinsia ya XYZ ubishi huo ni wakitaalam unahitaji ushahidi tu! wa Doctor wake na wazazi wake XYZ kwisha, hamna nafasi ya kujadili kwa hoja ya kutofautiana mawazo hapo, (kama Zomba anavyotaka tuamini) hapo hoja ni ushahidi thabiti wa kuonyesha kuwa XYZ ni mwanaume, hakuna mtazamo hata kidogo ni ukweli na utaalam; hivyo ndivyo ilivyo suala la DOWANS watu wenye ushahidi wanapoongea hilo suala na kupinga sio tofauti ya mtazamo wa kisiasa ni tofauti ya ushahidi, utaalam na uelewa juu ya jambo hilo la Dowans na Sheria ya Ushahidi, Sitta ana-ushahidi mwingine mzuri ndio maana anapinga sio Itikadi ya kisiasa na labda ana-ushahidi thabiti zaidi sio mtazomo kama Zomba anavyopotosha kuwa ni tofauti wa mtazamo wa Ki-siasa.

  Najua ZOMBA anaweza kuuliza mbona serikali imeshindwa kesi; ndio imeshindwa kupereka wataaam wazuri na ushahidi mzuri juu ya kesi hiyo, sasa hapo ndipo mtu anayepima tija ya maneno yake angelijiuliza hivi kwa nini serikali haikupereka ushahidi imara? ni suala la kujiuliza sana mimi Binafsi bado nina jiuliza maswali mengi sana nikipata majibu nitarusha hapa JF, kwa mfano Dr. Mwakyembe ni Mwanasheria wa kiwango cha Falsafa za sheria, na Pili alishiriki kufanya uchunguzi wa awali wa tuhuma hiyo, hivi serikali ilimtumia katika ushahidi wa ICC? mimi sijui! maswali ni mengi ila tumia sana akili yako Bwana ZOMBA Mungu amekupa bure husije-ukaonekana unatumika kupotosha kumbe la!
   
 16. L

  LAT JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Mkuu... hili ni genge la Malaria Sugu aka MS wametumwa na RA ..... usiumize kichwa.......
   
 17. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hivi hamjui hili? Kuna watu wamo humu jamvini kwa niaba ya mafisadi na wapinga ukombozi wa Watanzania wanyonge. Ndio hao hoja yoyote itayozungumzwa inayoelekea ukombozi, wao wanadakia na kuchafua. Kuna ambao wana ujuzi wa kuandika vizuri, na wengine hawajui hata kupanga hoja (nadhani mnawajua). Pamoja na juhudi zao hizo, kamwe hawataweza kuzima joto la mapinduzi ambalo limeshaanza sasa. Wanatupumbaza kwa kudai kuwa mbona fulani alishindwa mwaka fulani etc. Wajue kwamba siku hazigandi, na mabadiliko katika jamii huathiri vile vile matokeo ya harakati katika jamii hizo. Miaka ya 19kweusi sio sawa na sasa ambapo wananchi wameamka kisiasa na habari na ufahamu wa dunia upo karibu zaidi kwa kila binadamu.
   
 18. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #18
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Asante kwa taarifa, sikua najua
   
 19. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Ngeleja anajua siri yote na amekula kitu kidogo
   
Loading...