Mawasiliano serikalini!..

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Nilikuwa natafuta nambari ya simu ya kiganjani ya Mhe. .., nikajaribu kwa mahangaiko makuu na kupitia http://www.utumishi.go.tz/index.phpoption=com_docman&task=doc_view&gid=288 nikaweza kupata kitabu cha mawasiliano serikali (attached.)

Lakini kilichoniacha mdomo wazi ni kuwa sijaweza kuipata namba yoyote ya mkononi wala ya moja kwa mojaya ofisini kwa Mhe. na hata kwa wafuasi wake hakuna namba za viganjani. Kadhalika baadhi ya watumishi hawana kabisa namba za simu za ofisi wala mkononi ni majina tu na vyeo vyao vimeorodheshwa. Na cha kusikitisha zaidi, lugha mbili tofauti imetumika ndani ya kitabu hiki jambo ambalo lina kanganya ni kwa Serikali inayohimiza matumizi ya lugha ya Taifa!.

Najiuliza hivi ni kweli ninyi wa Serikalini (UTUMISHI WA UMMA) hawa jamaa ambao wametajwa tu kwa majina na nafasi zao, hawana simu za viganjani au moja kwa moja ofisi kwao????. Je, ipo haja gani kuwa na jina la mtu ambaye simu yake haijaonyeshwa katika kitabu hiki nyeti cha kutusaidia wapigakura kuwasiliana na Serikali yetu???.
 

Attachments

  • KITABU CHA MAWASILIANO SERIKALINI.pdf
    1.4 MB · Views: 2,055
Back
Top Bottom