Mawakili wa Kujitegemea waaswa kutowakamua wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawakili wa Kujitegemea waaswa kutowakamua wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Feb 5, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280

  Mawakili wa Kujitegemea waaswa kutowakamua wananchi

  Imeandikwa na Grace Chilongola, Mwanza; Tarehe: 4th February 2011 @ 23:50

  MAWAKILI wa kujitegemea nchini wameaswa kutotanguliza maslahi binafsi pale wananchi wanapohitaji huduma yao na badala yake wafanye kazi katika viwango vya juu ili utetezi wao uwe na maana katika jamii.

  Wito huo ulitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro katika sherehe za siku ya sheria ambapo alidai mawakili wengi wa kujitegemea wamekuwa wakitanguliza maslahi wakati wanapokuwa na kazi za kuwatetea wananchi.

  Alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia huduma zao na kudai kuwa wamekuwa wakiwatoza fedha nyingi za utetezi na bila ya kuwepo kwa mafanikio katika kesi zao na kuwaacha wakiwa masikini.

  Mkuu huyo wa Mkoa alisema amani na utulivu wa nchi ya Tanzania inachangia utendaji kazi mzuri na ili amani hiyo iweze kuendelea mawakili hao wanatakiwa kufanya kazi zao kwa amani zaidi na kuidumisha amani iliyopo.

  Akizungumzia utoaji wa elimu ya mfumo wa Mahakama, Mkuu wa Mkoa alisema wananchi walio wengi hawajui mfumo wa Mahakama hali inayosababisha kuondoa kesi zao mahakamani na kuzipeleka serikalini.

  Alisema amekuwa akipokea watu wengi ofisini kwake wakilalamikia kutokutendewa haki katika Mahakama ikiwemo kucheleweshwa kwa kesi zao jambo ambalo linahitaji elimu.

  Alisema malalamiko hayo yanatokana na wananchi kutokujua namna Mahakama inavyofanya kazi zake na kudai kuwa elimu zaidi inahitajika ili wananchi wawe na uelewa wa kutosha.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Alisema amekuwa akipokea watu wengi ofisini kwake wakilalamikia kutokutendewa haki katika Mahakama ikiwemo kucheleweshwa kwa kesi zao jambo ambalo linahitaji elimu

  Alisema malalamiko hayo yanatokana na wananchi kutokujua namna Mahakama inavyofanya kazi zake na kudai kuwa elimu zaidi inahitajika ili wananchi wawe na uelewa wa kutosha.
  This is a piece of baloney..............................waelemishweje kuhusu ucheleweshwaji wa kutoa haki?...............................the response is pathetic, to put it mildly...................................
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  HTML:
  MAWAKILI wa kujitegemea nchini wameaswa kutotanguliza maslahi binafsi pale wananchi wanapohitaji huduma yao na badala yake wafanye kazi katika viwango vya juu ili utetezi wao uwe na maana katika jamii. 
   
  Wito huo ulitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro katika sherehe za siku ya sheria ambapo alidai mawakili wengi wa kujitegemea wamekuwa wakitanguliza maslahi wakati wanapokuwa na kazi za kuwatetea wananchi. 
   
  Alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia huduma zao na kudai kuwa wamekuwa wakiwatoza fedha nyingi za utetezi na bila ya kuwepo kwa mafanikio katika kesi zao na kuwaacha wakiwa masikini. 
  Hizi blah blah kamwe hazitupeleki popote................................kinachotakiwa ni sheria za malipo haya yawaje tu.....................Advocates have mouths to feed too.................................
   
 4. P

  Pokola JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  You explained it all, fella. Quite a clumsy rubbish!!
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  quite absurd! Anyone who has the power to make you believe absurdities has the power to make you commit injustices.
   
Loading...