VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Huwa natetemeka kila ninapoona kiongozi wa Serikali anaposema au kutenda katika kupambana na Mawakili. Kiongozi wa Serikali hakuwa hapo alipo. Wapo walioanzia kwenye Ubunge wa kawaida na baadaye kuwa Mawaziri na hata zaidi ya hapo. Viongozi hao wametoka mbali. Wana historia zao.
Mawakili wana siri nzito za nchi hii: siri za viongozi na wananchi wa kawaida. Mawakili ndiyo walioshiriki katika kuandaa mikataba safi na tata inayowahusisha viongozi wa sasa wa Serikali. Mikataba ya kiserikali ya kununua, kuuza, kukodisha, kutafuta madini, kuagiza na kadhalika imeandaliwa na Mawakili. Ima sirini au ofisini, Mawakili wametenda na kulinda vingi.
Katika kuzuia kashfa mbalimbali dhidi ya viongozi waandamizi wa kiserikali, Mawakili wameshiriki katika kunyoosha na kupindisha sheria ili mambo yakae sawa. Viongozi wa kiserikali wameuza, wamenunua, wamepanga, wamepangisha, wamekodi na kukodisha, wameagiza na kutoa mali zao binafsi kupitia Mawakili.
Ni kwakuwa tu Mawakili hutunza siri za wateja wao, mambo ndiyo yapo kama yalivyo. Pametulia. Lakini, kuonesha kupambana kwa kutishatisha Mawakili na chama chetu cha Tanganyika Law Society (TLS) ni kuwachokoza Mawakili. Ni sawa na kuanzisha ugomvi wa mawe ukiwa unaishi kwenye nyumba iliyojengwa kwa vioo.
Mawakili wana mambo makubwa kwenye vichwa na mioyo yao. Wameyanyamazia ili Taifa libaki na amani na utulivu wake. Mawakili wasichokozwe. Wakichokozeka, nchi itatikisika. Tuacheni tuchaguane na kuongozana kadiri ya Sheria na Taratibu zetu. Msituingilie. Mawakili ni watu makini, wana uwezo mkubwa wa kupembua na kuamua. Tuachwe tufanye yetu, tuyalinde yenu.
Mwafaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha kumchagua Lissu kuwa Rais wa TLS)