Mawakili 24 wameungana kumtetea Mbunge wa Kyadondo, Bobi Wine Mahakamani Agosti 23

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mawakili 24 wameungana kumtetea Mbunge wa Kyadondo, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, huku wakimtaka Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu nchini humo, Med Kaggwa kutumia vyema haki ya kikatiba ili kuhakikisha haki inatendeka

Mbunge huyo anatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Kijeshi Agosti 23, ambapo hadi sasa anashikiliwa kwenye gereza la Kijeshi la Makindye akidaiwa hawezi kuongea wala kutembea

Hata hivyo madai hayo kuwa hali Bobi Wine ni mbaya yalikanushwa na Rais Yoweri Museveni akisema habari hizo ni uongo na kuongeza "Mjukuu wangu Bobi Wine yupo salama na hali yake ni njema."

Aidha, Mwanasheria wa mbunge huyo, Male Mabirizi amefungua kesi Mahakama Kuu kutaka kuachiwa kwa mbunge huyo na wenzake wakiwamo wanaharakati mbalimbali waliokamatwa wakati wa kampeni za ubunge wa Arua
 
Back
Top Bottom