fimboyaasali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 8,606
- 8,270
Wanandoa nyie ni mawakala wa Mungu,zaeni watoto,muwalee vizuri ili nao waje kuzaa na kuanzisha familia zao.Iki mtimize wajibu huo,acheni migogoro midogo midogo mara,mje kafanya hivi,mara mume kafanya vile,hiyo ni akili ndogo.Maisha yenu ni yenu nyie 2 tu,hakuna haja ya kushirikisha wengine.Pangeni kwa pamoja maisha yenu,mkubaliane kwenye kila kipengele cha maisha,kazi,biashara,nyumba,unyumba,watoto,chakula,matibabu,misaada kwa familia,usulihishi wa migogoro,misaada kwa ndugu,sala kwa kutegemea dini zenu,ngono na starehe