MAWAKALA WA MABUS MSAMVU TERMINAL NI KERO

Katali

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
859
694
Mnamo tarehe 02/03/2017 nilifika stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani maalufu kama Msamvu terminal Morogoro nikasoma tangazo Abood bus service kutoka Dar-Tunduma nikalipia tiketi kwaajili ya tarehe 04.03.2017 nilipotoka nje ya ofisi za abood nikaambiwa na baadhi ya mawakala kwamba abood haifanyi safari za tunduma nikarudi tena ofisini lkn wakanisisitizia kwamba safari ipo na niwabuuze wapiga debe maana kunaushindani wa kibiashara siku ya safari ilipofika nikawahi standi lakini nilipofika nikaambiwa abood itaishia mbeya mjini hivyo wakanitafutia bus la saibaba kwamba ndilo linalokwenda Tunduma mpaka Sumbawanga!lakini chaajabu tulipofika mbeya mjini nao wakadai hawaendelei na safari!!lakini mbaya zaidi kulikuwa na abiria zaidi ya kumi ambao nao walikatiwa tiketi za tunduma na sumbawanga na tukatelekezwa mbeya mjini bila kurudishiwa ongezeko la nauli kwani mawakala walitoa tiketi zenye kiwango husika lkn kondakta akazichukua na kuandika tiketi mpya kwa kiwango cha chini tulipohoji kuhusu chenji walikuwa makaidi.Ninachotaka kueleza hapa kwamba mamlaka husika pamoja na umma uelewe kwamba hawa wapigadebe/mawakala ni janga kubwa maana nimeshuhudi akina mama na watoto wakiachwa standi hawajui la kufanya usiku ule huku wakizongwa na wapiga debe wa bajaji,taxi na maguest najua mchezo huu upo kwa siku nyingi lakini kunakilasababu ya kuchukua hatua pia vyombo vya dola viwepo maeneo ya standi ilikupokea kero za namna hii lakini pia tujulishane sisi abiria kujua mchezo huu mchafu na kuepukana na makampuni yanayolea matapeli kwani hili siyo jambo dogo nimeshuhudia usumbufu huu na nilazima tupaze sauti ili kukomesha tabia hii mbovu.
 
Back
Top Bottom