Mavunde awashushia rungu wafanyabiashara ya madini

Robot la Matope

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
7,052
13,705
Kahama: Serikali imesimamisha leseni zote nchi nzima za Kampuni ya Nadoyoo Mineral Trading kufuatia kukamatwa kwa mmoja wa wahusika wa kampuni hiyo akituhumiwa kutorosha dhahabu zaidi ya kilo 4.3 zenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 562.3.

Dhahabu hizo zimekamatwa katika operesheni ya kushtukiza iliyofanywa usiku na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde.

Akizungumza mara baada ya dhahabu hiyo kukamatwa, Mavunde amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, haitakubali kuona watu wachache wanajihusisha na vitendo hivyo viovu vya kutorosha madini.

"Nataka niwaambie, tutachukua hatua kali dhidi ya yeyote tutakayemkamata akijihusisha na utoroshaji wa madini, "amesema Mavunde na kuongeza:

"Nilipoingia Wizara ya Madini mwezi mmoja uliopita nilisema, ukitaka kufahamu sura yangu nyingine basi jaribu kutorosha madini.;.... Sasa basi, kuanzia leo mtu yeyote atayekamatwa kwa kosa la kutorosha madini, tutakwenda kusimamisha leseni zake zote nchi nzima wakati tukisubiri hukumu ya vyombo vya sheria," amesema.

Amesema, iwapo mahakama itabaini mhusika ana hatia, atachukuliwa hatua kali ikiwem

Mavunde ametoa wito kwa wafanyabiashara wa madini kuwa wazalendo kwa kufuata taratibu zilizopo na kulipa tozo, ada na kodi mbalimbali ili kuiwezesha serikali kupata mapato na kuendelea kuimarisha huduma kwa wananchi ikiwemo ujenzi wa barabara, umeme, afya na elimu.

Amesema, yupo tayari kukaa na wafanyabiashara wa madini ili kwa pamoja wamweleze hasa ni nini wanadhani inaweza kuwa ni changamoto kubwa inayopelekea baadhi yao kufikia hatua ya kujihusisha na vitendo vya utoroshaji madini, hatua ambayo anaamini itasaidia Serikali kuchukua njia sahihi kushughulikia suala hilo.

Vilevile, ameweka bayana kuwa pamoja na hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi ya watoroshaji wa madini, pia madini yote yatakayokamatwa yatahifadhiwa na serikali na kupelekwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kusubiri hatma ya Mahakama.

FB_IMG_1697097539629.jpg

My Take

Mwambieni Mavunde akaangalie movie ya SISU!
 
Kazi nzuri Sana,

Ila mwambieni Jiji la Dodoma kwa sasa

1. Lina shida ya Maji ya kufa mtu.
2. Kuna migogoro ya Ardhi isiyopimika.

Aje ashughulikie na haya kama Mbunge wa DODOMA MJINI.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom