Mauzauza yanayowatatiza wanawake….!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
couple-talking-pf2.jpg

Hivi ni kwa nini wanaume wazuri na wenye muafaka kwa maisha ya ndoa hujitokeza kwa wingi kwa nia ya dhati ya kutaka kuoa baada ya kuwa mwanamke keshapata mwenza, lakini wakati alipokuwa singo akiwinda walikuwa wala hawaonekani na hata wakionekana wanakuwa wasumbufu na wenye tabia za sitaki nataka…….?
 
Haya wanaume na wanawake mtiririke hapa ili kujua sababu hasa ni nini.....
 
mimi nadhani sababu kubwa ni kwamba,
  • waoaji daima hutaka mwanamke aliye tulia(hata kama wao hawajatulia) na asilimia kubwa ya wanawake hutulia baada ya kuolewa. huku waoaji wakiwa hawajui chanzo cha utulivu huo. Lakini hapo kabla wanawake huwa hawajiamini na hujihususha na wanaume mbalimbali.
  • Pia wakati huu mwanamke hunawili zaidi sababu ya .... na daima anapendeza maana huacha kuvaa ovyo kama mke wa mtu
  • Kisaikologia, mwanamke aliyeolewa hupunguza dharau dhidi ya wanaume. tofauti na hapo awali alikuwa akidhani kila mwanaume anaye msemesha anaelekea kumtongoza na mara moja kuanza kumjibu kidharau kama hamtaki. lakini sasa hofu hiyo humwisha kabisa na kuwa huru kwa kila mwanaume na kumueshimu. Hapo ndipo kila mwanaume huvutiwa nae kwa minajili ya kumuoa na si kudate tu.
  • Akiolewa hupunguza ama kuacha kabisa maisha yasiyo na tija kimaendeleo, kama kulewa, kwenda klabu, kula magengeni, kuji-over decorate, na kupoteza muda kwenye vijiwe vya udaku. chunguza sana utagundua wengi wa wanaoendeleza tabia hizi huwa wanaachika au ndoa zao zina matatizo.
Ngoja na wengine waseme....
 
Hii shughuli. Wenye hoja za maana tiririkeni mtusaidie na siye "Mbumbumbu mzungu wa reli"

Bazazi!
 
Yaaaaaaaani! Umejuajeeeeeeee? Tatizo ndo lile lile la kutaka KUBANANA HAPO HAPO.

Yaani kuna tabia flani siielewagi kabisaaaa! Unakuta kuna mdada famaous kama Wema Sepetunga, afu kuna a nobody kama Daimondo. Huyu Daimondo akimtokea demu wanamtoa race kali. Ila dem mwenzao ambae wanamkubali akijitoa ufahamu na kutoka nae! Baaaaaaaaass! Automatically inakuwa kama kapanda chati!!!! Kila demu wale wale waliomtosa wanaanza kumtaka kwa udi na uvumba!!!!

Yaani inakuwa kama unataka tiketi ya kujimuvuzisha na mademu bomba basi utafute mmoja ambae wao wanampitisha then unakuwa umetoka!!!!!

Ngoja nikimbia maana Manoah kaniweka WANTED humu JF
 
Mwanamke anapopata mchumba kwa maana yoyote ile

1. Hujiheshimu na kuheshimu - wanaume wengi hupenda sana heshima wakiamini kuwa huo ndio msingi wa ndoa

2. Huwa mpole, mtulivu na mnyenyekevu - Hutoa mwanya kwa waowaji kuamini katika kudumu naye katika ndoa

3. Huwa na malengo kwa maana ya nini afanye kwa nafasi gani, wapi na kwanini afanye - huonekana kuhodhi hoja ya mke mwema (ambayo ndiyo hoja inayowindwa na wanaume kwa nguvu zote)
4. Uwezo wake kutathimini mambo kwa maana ya madhara anakuwa sensitive na makini sana - hujiepusha na suala la kuonekana mapepe mda wote hutaka kuonekana ni bora na makini

5. Mavazi yake huwa ya staha, nadhifu - hili huongeza mvuto kwa watafutaji wakiamini kwamba hiyo ni mojawapo ya matendo ya mke mwema

Kwa wanawake waliowengi, kabla ya kufunga uchumba na mwanaume yeyote huwa wanakosa hofu ya atanionaje kama nitafanya hivi au nitatoka hivi ambayo huipata mara baada ya kupata mchumba, wanakuwa na uhuru mpana kabla ya uchumba na mambo mengi ambayo kwa bahati mbaya wanaume hupata hofu na kuchukulia uhuru huo wa mwanamke kwa mtazamo hasi, matokeo yake hawamtokei kwa kudhani hanasifa za mkemwema ambao sio mtazamo sahihi lakini ndio ukweli wenyewe.
 
mimi nadhani sababu kubwa ni kwamba,
  • waoaji daima hutaka mwanamke aliye tulia(hata kama wao hawajatulia) na asilimia kubwa ya wanawake hutulia baada ya kuolewa. huku waoaji wakiwa hawajui chanzo cha utulivu huo. Lakini hapo kabla wanawake huwa hawajiamini na hujihususha na wanaume mbalimbali.
  • Pia wakati huu mwanamke hunawili zaidi sababu ya .... na daima anapendeza maana huacha kuvaa ovyo kama mke wa mtu
  • Kisaikologia, mwanamke aliyeolewa hupunguza dharau dhidi ya wanaume. tofauti na hapo awali alikuwa akidhani kila mwanaume anaye msemesha anaelekea kumtongoza na mara moja kuanza kumjibu kidharau kama hamtaki. lakini sasa hofu hiyo humwisha kabisa na kuwa huru kwa kila mwanaume na kumueshimu. Hapo ndipo kila mwanaume huvutiwa nae kwa minajili ya kumuoa na si kudate tu.
  • Akiolewa hupunguza ama kuacha kabisa maisha yasiyo na tija kimaendeleo, kama kulewa, kwenda klabu, kula magengeni, kuji-over decorate, na kupoteza muda kwenye vijiwe vya udaku. chunguza sana utagundua wengi wa wanaoendeleza tabia hizi huwa wanaachika au ndoa zao zina matatizo.
Ngoja na wengine waseme....
nakubaliana nawe ila wako wadada single na wametulia wanatabia njema ila hao wanaume waoaji wala hawahangaik nao!
 
Yaaaaaaaani! Umejuajeeeeeeee? Tatizo ndo lile lile la kutaka KUBANANA HAPO HAPO.

Yaani kuna tabia flani siielewagi kabisaaaa! Unakuta kuna mdada famaous kama Wema Sepetunga, afu kuna a nobody kama Daimondo. Huyu Daimondo akimtokea demu wanamtoa race kali. Ila dem mwenzao ambae wanamkubali akijitoa ufahamu na kutoka nae! Baaaaaaaaass! Automatically inakuwa kama kapanda chati!!!! Kila demu wale wale waliomtosa wanaanza kumtaka kwa udi na uvumba!!!!

Yaani inakuwa kama unataka tiketi ya kujimuvuzisha na mademu bomba basi utafute mmoja ambae wao wanampitisha then unakuwa umetoka!!!!!

Ngoja nikimbia maana Manoah kaniweka WANTED humu JF
Wewe kweli unazifahamu tabia zenu. Ulichokisema hapo ndicho ninachokishuhudia miongoni mwa jamii mbalimbali.
 
Sababu kubwa ni kutokuwa na uvumilivu kwa sababu kila jambo na wakati wake.Watu wengi wakati wa Mungu unapofika ndio utakuta wamefanya makosa.
 
Umesahau hulka ?
Watu hawana originality kwa mambo mengi hata kwenye mahusiano.
Mwanamke akishapata mwanaume, ndipo wanaume wengine hufunguka macho na
kumuona "anafaa"!
Usishangae kuona kasi ya kufuatilia wake za watu inaongezeka.
 
Ni nature ya maisha.
Si wanawake tu wapo wanaume wakishaoa ndio akina dada wanajitokeza.
Siku zote unapopata mafanikio ndio upinzani wa lile ulilofanikiwa linapojitokeza ili kupima uzito wa msimamo wako.
In short,,SHIDA INAPOISHA NDIPO MSAADA HUJITOKEZA.
Ndivyo maisha yalivyo
 
nakubaliana nawe ila wako wadada single na wametulia wanatabia njema ila hao wanaume waoaji wala hawahangaik nao!

Mimi pia nakubaliana na wewe, ukichunguza kwa kina hao watakuwa wanakumbwa na moja wapo ya yafuatayo au yote:
  • Inawezekana wanaelimu kubwa sana kuliko ile ya wanaume wowote anaopata kukutana nao katika pitapita zake, wanaume walio wengi hawataki mwanamke aliyemzidi kielimu
  • Ama atakuwa na kipato kikubwa/ tajiri sana kuliko wanaume waoaji wanaomzunguka. Mwanaume kawaida huogopa kasha ya kuambiwa kaolewa na si kaoa. hii ni kwa sababu wanawake wengi waliotangulia wakaolewa huko wakiwa na mali kuliko mwanaume waliishia kumtumikisha na kumdharau mume wake.
  • Inawezekana inasababishwa na tabia mbaya za wazazi wake au ndugu zake wa karibu. hilo pia wanaume wanaangalia kabla ya kuoa. mfano kama dume alitaka kuoa demu filani ilikhali hajui kuwa ni mtoto wa mama fulani ambaye ni jamvi la kufikia wageni hapo mtaani, akijua tu uoaji unaahirishwa
  • Pia inawezekana binti huyo kwa muda fulani alikuwa hataki kuolewa na akawa anakataa mahusiano na wanaume. kila aliyejaribu kumwendea alimtoa balu bila sababu ya msingi huku akisahau kuwa waoaji wa lika lake wanaisha. baada ya muda wanaume wote waoaji wanaacha kumfuata maana huwa wanaambiana kuwa hapaingiliki. Wanaume wanaofuata humkataa sababu ya umri wake.
  • Au pia inawezekana mwadada huyo hapati muda wa kijichanganya kijamii. hivyo haonekani kwa wanaume, au akionekana pia hatoi mwanya na mazingira ya kupendwa(kutongozwa). mfano yeye ni mwajiriwa, akiwa kazini ni busy na kazi tangu ameingia hadi anatoka, baada ya hapo ni kwenye gari mpaka nyumbani. akienda kanisani/msikitini huenda kwa gari kwa kuchelewa na hutoka kabla ya muda. hakuna kwenda sokoni, au matembezi yoyote yale. akija kustuka umri umeenda na hakuna muoaji wa lika lake tena
  • Wengine hawataki kuolewa wao wenyewe, kwa sababu zao binafsi.
 
Kuna wanawake wamekaa kama vile hawaingiliki kimapenzi kabisaaa. ila pale inapojulikana amechumbiwa hapo ndipo wanaume wanapata kujiamini kwamba kumbe anaingilika tu. kwani J kaweza mimi nisiweze?
 
hii hata mie siielewagi mweh!

Ingawa kwa upande mwengine wanaume wanapenda wanawake walioolewa kwa maana hawana gharama na hawasumbui, mizinga ya hapa na pale hakuna....

Wakati wanawake wanapenda wanaume waliooa maana wanajua kutunza na hawakubani
 
Kuna wanawake wamekaa kama vile hawaingiliki kimapenzi kabisaaa. ila pale inapojulikana amechumbiwa hapo ndipo wanaume wanapata kujiamini kwamba kumbe anaingilika tu. kwani J kaweza mimi nisiweze?

sory,wewe
ni,mwanasaikolojia?
 
Back
Top Bottom