Mauzauza ndani ya msitu wa Shengena uliopo Wilayani Same

Tayari ishanikuta hiyo... Nimeenda sehemu kwa kutumia dakika kama 30 lakini wakati wa kurudi kwa kutafuta shortcut nilijikuta natumia zaidi ya masaa mawili kufikia nyumbani. Huyo mdudu yupo maeneo ya Mbezi kwa Yusuph mitaa ya ndani ndani huko
 
Stor zingn zilitengenezwa nawazee ili kujenga woga wakutoharibu misitu.
Ni kweli mkuu, nakumbuka kijijini kwetu wakati tukiwa watoto tuliambiwa ukikojoa kwenye maji (mifereji inayotiririsha maji) mama yako atakatika titi. Hii stori iliwatia adabu wale watoto watukutu wenye tabia zisizofaa.


JESUS IS SAVIOR
 
Ni kweli mkuu, nakumbuka kijijini kwetu wakati tukiwa watoto tuliambiwa ukikojoa kwenye maji (mifereji inayotiririsha maji) mama yako atakatika titi. Hii stori iliwatia adabu wale watoto watukutu wenye tabia zisizofaa.


JESUS IS SAVIOR
Yeeah, vitisho vile vimesaidia san baadhi ya maeneo kuwa salama Hadi miaka hii
 
Salam kwenu nyote...

Shengena ni msitu mkubwa unaopatikana milima ya Pare katika wilaya ya Same.

Msitu huu una miti mingi mirefu na mimenene, mito mikubwa ya maji Safi, ndege pamoja na wanyama mbalimbali. Maji yatokanayo na msitu huu ni msaada mkubwa kwa kilimo Cha umwagiliaji katika maeneo ambamo mito hiyo hutiririsha maji yake. Pia inasemekana ndani ya msitu huu Kuna madini mengi ikiwemo dhahabu.

Nikiachana na uzuri wa msitu huu niende Kwenye mauzauza yake; Ndani ya msitu huu Kuna njia za miguu ambazo hupitisha watu kutoka maeneo ya Chome, Vudee, Mbaga na Gonja.

Inasemekana Kuna mdudu fulani ukimkanyaga ndani ya msitu huu utatembea mchana na usiku bila kufika unapokwenda, kwa kifupi ni kwamba unapotea.

Siku moja nikiwa narafiki zangu wa5, tulikuwa tunatoka kwenye sherehe flani huko Gonja. Tukaamua kupita ndani ya msitu huo ili tufike nyumbani Chome. Ikumbukwe kuwa ipo njia ya magari lakini ni mpaka upitie Same ambapo ni njia ndefu kwelikweli.

Wakati tupo katikati ya msitu mwenzetu aliyekuwa ametangulia akaanza kutupoteza huko msituni. Anadai njia zimekuwa nyingi zinamchanganya. Kwakuwa wote tulikuwa tunafahamu njia akatangulia mwingine mbele, hizi njia ni nyembamba hivyo mkiwa wengi mnatembea kwa mstari. Mambo yakawa yale Yale, mnapita njia hii mkifika mbele njia inapotea inabidi mrudi Tena mlipoanzia.

Ilitakiwa tuumalize msitu huo sa6 mchana Ila hadi saa10 jioni tulikuwa tunahangaika kutafuta njia.

Baadae nikaona nitangulie mbele, kutembea hatua chache mbele nashangaa nagongwa nakitu usoni. Sasa kwa kuwa kuna miti mingi ikabidi ninyanyue macho juu nione nini kimenigonga...asee, kumbe ni miguu ya mtu aliyejinyonga Kama sio kunyongwa. Nikawaambia jamaa zangu mnaona hii kitu?

Jamaa wanasema kitu gani, nikawapeleka pale alipo yule mtu. Wajamaa wanadai hawaoni kitu zaidi ya kamba za miti zilizoning'inia. Nikasema hii balaa Sasa kwani wakati huo Mimi nilikua naona mwili wa mtu tena mwanaume.

Nikawaambia siwezi Tena kutangulia aje mwingine awe mbele yetu. Jamaa mmoja akapita kwa hasira akiona tunamfanyia mchezo njiani...hapo kila mmoja ananjaa kwani tuliondoka Gonja saa3 natulikunywa tu chai na maandazi. Jamaa kaongoza njia kufika mbele anasimama ghafla...anadai Kuna shimo kubwa kwa mbele hivyo hyo sio njia turudi.

Tulipoenda kuangalia Ile sehemu hakukuwa na shimo lolote. Sisi tukapita vizuri, shida ikawa kwa jamaa. Anadai hawezi kuvuka hilo shimo kwani linatisha Sana. Sasa tufanyeje na giza lishaanza kuingia,...tukamwambia jamaa tukubebe basi uvuke, anasema haiwezekani hapo hamnivushi Kama vipi nyie nendeni tu mniache. Tatizo ndani ya msitu huu hakuna maawasiliano ya mtandao wowote wa simu ili pengine tuombe msaada kutoka nje yamsitu.

Wakati tunashauriana balaa jingine likajitokeza...mvua. Ilikuwa mvua kubwa na radi ambazo hazikuanza kwa kuonyesha dalili yoyte. Baada yakunyeshewa vyakutosha likatokea kundi la Ng'ombe wengi ambalo lilipita bila shida kwenye Ile sehemu jamaa alosema kuna shimo.

Nyuma yakundi lile la Ng'ombe alikuwepo mzee mmoja ambaye ilibidi tumwelezee kilichotukuta na akashangaa tulivyomwambia Kuna mvua imetunyeshea. Kumbe Ile mvua ilikua inatunyeshea sisi tu nawala pale msituni hakukuwa na mvua. Mzee akacheka Kisha akatusihi tumfate.

Nifupishe tu kwa kusema tulifika nyumban kesho yake baada ya kusaidiwa nayule mzee mchungi wa Ng'ombe.

Miaka mingi imepita ilaSitaisahau Shengena.

Wasalaam!
Na hao wanao chunga mifugo ndani ya hifadhi ya msitu wa Asili wa Chome ndio wanatafutwaga na watu wa Mali asili, ...siunaona wale wachimba madini walivyo haribu ule mto Sasemi ?

Pale wanapaita UNDP, ktk ule msitu wapare wanakata sana miti kwa ajili ya Mbao wana haaribu sana ule msitu mzuri.mnoo ........ Mie nilizunguka hio msitu 5 weeks sikuwah kukutgana na hayo mauza uza, kumne napaswa nimshukuru Allah eh 😀😀 kweli chief ule msitu ni mzuri sanaa asikwambie mtu mie nimefika mpaka kwenye peak ya Shengena,
 
Na hao wanao chunga mifugo ndani ya hifadhi ya msitu wa Asili wa Chome ndio wanatafutwaga na watu wa Mali asili, ...siunaona wale wachimba madini walivyo haribu ule mto Sasemi ?

Pale wanapaita UNDP, ktk ule msitu wapare wanakata sana miti kwa ajili ya Mbao wana haaribu sana ule msitu mzuri.mnoo ........ Mie nilizunguka hio msitu 5 weeks sikuwah kukutgana na hayo mauza uza, kumne napaswa nimshukuru Allah eh kweli chief ule msitu ni mzuri sanaa asikwambie mtu mie nimefika mpaka kwenye peak ya Shengena,
Saivi uharibifu sio mkubwa Sana mkuu.Serikali iko makini
 
Binafsi nimesoma same secondary pale...kwa miaka 6...wakaz wa pale mbongo zao ni tatizo sana...yaan ilibaki kidogo tuu kabila lile wotee waingie kwenye uzuzu...yaan hata nilio soma nao ambao ni wenyej wa pale darasani 😂😂😂 ila bora same sogea kidogo uwende Mwanga...kwa mlio ishi mtwara au lindi mtanielewa namaanisha nini..:😂😂 hizi iman ni rahis sana kuaminika.NB watani zangu nawapenda sana..:AVae
 
Miaka ya 90 au 2000 iliwahi kuanguka shengena ikaua watu wote. Ajali ilihusishwa naushirikina watuwakaacha kupanda hayo magari mmliki akaiingia ubia nakampuni nyingine ya mabasi yakabadilishwa jina narangi yakawa yanitwa tashrif
Wamaanisha Air Shengena "No Challenge"
 
Ndo huo msitu hukohuko upareni, kuna bwawa ndaniyake kunasamaki..
kunamda huruhusiwi kuvua samaki
Sasa kuna watu wakaenda kuvua na ndoano ile kushusha ndoano,

Wakavua ugali nasamaki waliopikwa fresh kabisa kwenye kibakuli...sjui nikweli anaye jua anielekeze
 
Ndo huo msitu hukohuko upareni, kuna bwawa ndaniyake kunasamaki..
kunamda huruhusiwi kuvua samaki
Sasa kuna watu wakaenda kuvua na ndoano ile kushusha ndoano,

Wakavua ugali nasamaki waliopikwa fresh kabisa kwenye kibakuli...sjui nikweli anaye jua anielekeze
 
Daaaaaah!sipendi kukuelezea zaidi kuhus hayo mauzauza Ila nimependa tu ulivyotaja chome,chago,mmeni.
Mmoja Kati ya jamaa tuliyekuwa nae kwao ni mmeni na mwingine pale chago karibu na soko.
Mimi sio mpare lakini maeneo hayo nayajua kinoma, Ngujini, Mhero, Kilindini, Mmeni, Ngw'anga, na Marieni bila kusahau Ukweni kwangu Mtwana..
 
Back
Top Bottom