MAUWASA yatumia Tsh bilioni 29 miradi ya maji Maswa

MAUWASA yatumia Tsh bilioni 29 miradi ya maji Maswa

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Maswa (MAUWASA) imetumia zaidi ya Shilingi bilioni 29 kukamilisha jumla ya miradi 18 ya maji safi na salama katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu.

, Mkurugenzi wa MAUWASA, Mhandisi Nandi Mathias, amesema kiasi hicho cha fedha kimetolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa maeneo yanayohudumiwa na mamlaka hiyo.

Katika kijiji cha Buyubi, Kata ya Mwamashimba, Mhandisi Nandi alisema mradi mmoja kati ya hiyo 18 tayari umekamilika kwa gharama ya Sh bilioni 1.3 na unatarajiwa kunufaisha wakazi zaidi ya 16,000 katika vijiji vitatu vya Buyubi, Likungulyasubi na Dodoma.

Aliongeza kuwa mbali na miradi ya ndani ya wilaya, mamlaka hiyo pia inasimamia utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria, unaoanzia Malampaka wilayani humo Maswa hadi Malya wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa Mhandisi Nandi, lengo kuu la miradi hiyo ni kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji salama kwa wananchi, hususan katika vijiji ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa vikitegemea maji kutoka vyanzo visivyo salama kama mito na mabwawa ya asili.

Miradi hii ni sehemu ya juhudi za serikali ya awamu ya sita kuhakikisha huduma za msingi zinawafikia wananchi vijijini, hasa maeneo yaliyokuwa yakikumbwa na changamoto ya maji kwa muda mrefu
 

Attachments

  • IMG_1970.JPG
    IMG_1970.JPG
    1.2 MB · Views: 26
  • IMG_1889.JPG
    IMG_1889.JPG
    569.6 KB · Views: 23
  • IMG_2006.JPG
    IMG_2006.JPG
    1.3 MB · Views: 21
  • IMG_2021.JPG
    IMG_2021.JPG
    1.1 MB · Views: 27
  • IMG_2032.JPG
    IMG_2032.JPG
    1.1 MB · Views: 27
Miradi ya kimkakati na kipindi cha kutakatisha pesa
 
Back
Top Bottom