Maumivu ya mgongo, kiuno, kichwa na shingo

Mr Leo

JF-Expert Member
May 1, 2021
604
1,262
Amani iwe kwenu ndugu wanajamvi!

Namshukuru mwenyezi mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuiona tena siku nyingine miongoni mwa masiku yake tukiwa ni wazima wa afya na wale wa matatizo mbalimbali awafanyie wepesi mwingi wa huruma.

Ndugu wanajamvi nimekuja hapa kwenu kupata msaada kwa kijana ambae ni wakaribu sana kwangu mwenye shida ya mgongo na kiuno ila hasa hasa maumivu kiuno hususani akikaa yaani low back pain

Sababu anayodai yeye ni kuwa kuna siku ambayo ni wiki mbili zilizopita alibeba furushi kubwa sana la kokoto kama umabali wa mita 300 kwenda kutoa gari iliyokuwa imekwama kwenye tope

Anadai ndio kwa Mara ya kwanza kubeba mzigo mzito kama ule na pindi alipo uweka mwilini aliskia kabisa umemzidi uwezo ila akajikaza kwa kuhisi labda tu yeye anajizembesha ila akijitahidi ataweza

Baada ya kumshinda sana akawa anauamisha kwenye bega ili baadae began lile baadae kichwani ila alishindwa hata kuufikisha eneo husika

Kuanzia siku iliyofuata alianza kuhisi maumivu hayo ya mgongo, shingo na kiuno kwa sana na kichwa kwa maumivu ya kubeba kitu kizito

Alijaribu kutumia dawa za maumivu na kuchuwa kwa takribani wiki mbili ila ikawa inaachia siku mbili au moja baadae inaamka tena

Tumemshauri aende hospital kufanya x ray na akutane na wajuvi zaidi mambo hayo ila anaogopa cost za hayo mambo maana hana kitu alipo

Binafsi nikaona katika hatua za kumsaidia ngoja nifikishe kisa chake katika jukwaa hili wajuvi wanaweza msaidia muda huo anajipanga atapata vipi pesa ya kwenda huko lugalo basi Wenda kuna dawa flani au kadhaa wa kadhaa akikifanya au akitumia wanaweza pata afadhali au kupona kabisa

Naombeni mchango wenu kwa hilo pia naomba kuwasilisha
 
Pole kwake,

Dawa ya maumivu ni muhimu kwake, lakini muhimu zaidi ni kupata vipimo. Hasa kwa suala lake anaweza kuhitaji vipimo zaidi ya Xray kulingana na dalili mbalimbali atakazopata mhudumu wa afya.
 
Back
Top Bottom