MAUMIVU YA MATITI

munguyupo

Member
Sep 4, 2015
22
1
MAUMIVU YA MATITI

Maumivu ya matiti hutokea mara kwa mara kwa wanawake, hasa kwenye matiti yenyewe au karibu na kwapa. Hujulikana kwa kitaalamu kama mastalgia.

Matiti au wengine wakiita maziwa, huweza kuuma yenyewe au kupata maumivu pale unapoyashika. Hali hii huwapa baadhi ya wanawake hofu wakidhani kuwa ni dalili ya saratani au mimba.

Maumivu ya matiti mara nyingi hutokea sehemu za juu za titi, wakati mwingine yakisambaa karibu na kwapa. Maumivu huwa ya kawaida, ingawa wakati mwingine yanaweza kuwa makali kiasi cha kukufanywa ushindwe kufanya shughuli zako.

Maumivu yanaweza kuwa kwenye ziwa moja au maziwa yote yakiambatana na kuvimba, uvimbe au mara chache kidonda. Pia yanaweza kujirudia kila mwezi.

Sababu Za Maumivu ya Matiti

Kuna sababu mbalimbali za maumivu ya matiti zikiwemo;

Vivimbe kwenye matiti (fibrocystic changes).
Matiti yanaweza kuwa na vivimbe visivyo saratani (cysts) ambavyo hujaa maji na kusababisha maumivu ya kujirudia rudia.
Premenstrual syndrome. Hali hii ni ya mabadiliko ya vichochezi vya uzazi ambavyo hujitokeza kabla ya hedhi kuanza. Husababisha matiti kujaa na kuuuma. Mumivu huwa makali zaidi siku 3 – 5 kabla ya hedhi na kupungua baada ya hedhi kuanza.
Maambukizi ya matiti (mastitis)
Usaha kwenyematiti (breast abscess)
Kutanuka kwa mirija ya maziwa (ductal ectasia)
Matumizi ya Dawa kama digitalis, aldactone methyldopa
Kukoma kwa hedhi (menopause)
Saratani ya matiti. Ni aghalabu sana kwa saratani ya matiti kusababisha maumivu ya matiti.

Matibabu

Mara nyingi maumivu ya matiti huisha yenyewe baada ya muda fulani.

Kukusaidia kupunguza maumivu ya matiti:

Vaa sidiria isiyokubana
Punguza unywaji wa chai na kahawa
Tumia vitamini E na mafuta ya primose

Kama unapata maumivu makali sana unaweza ukatumia dawa za maumivu kama paracetamol, NSAIDs.

Vidonge vya majira hutumika kutibu maumivu yanayotokana na mabadiliko ya kihomoni.ingawa si salama Kabisa,

Ukiona Hali hii njoo pata virutubisho vya Tiba mbadala pekee kutoka Nepstar Tanzania Co Ltd, km. Ginsenoside, Lycopene, spirulina, Neplily Sanitary pads. Hakika utakuwa umeamua vyema,, na hutasikia maumivu ya matiti kamwe. 0753606603 Nickson Health Consultant
Nipigie, nitakuhudumia maana wewe ni wa thamani Sana kwangu.
 
Back
Top Bottom