Maumivu: Niliyemfumania na mpenzi wangu kanipiga

Mapenzi bhana! Hata uyasomee kwa kiwango cha uprofesa uwezi kuwa mtaalamu nayo.
 
hapana mkuu , ila hapo kwenye kichapo,,,,,,,,,,,,,,,

sijui kwakweli , ila kudhalilishwa namna hiyo siyo vizuri.
 
Muda mwingi nilikua nikipita na kuchangia mada hapa MMU. Lakini sikuwahi kupost chochote.
Hili la leo limeniuma sanaa.!

Nina mpenzi wangu ambaye yuko chuo fulani hapa Dar lakini kutokana na maamuzi yetu tuliamua aishi mtaani badala ya Hostel. Huyu msichana nilianza nae mahusiano kwa kipindi kirefu sana na hata tumefikia kuvalishana pete na nyumbani kwao nafahamika pia.

Kutokana na shughuli zangu nyingi kua mikoani hua tunakutana kwa baadhi ya wikiendi tu ninapokuja hapa Dar.

Basi Ijumaa hii nikaona sio vibaya kum-surprise my wife to be. Nikatoka zangu mkoani na shauku ya kujiandaa kwenda kwa P-square na mamaa.

Nilipofika pale Geto kwake hali sikuielewa. Nikaona sio mbaya kubisha hodi. Niligonga kidogo tu sauti yenye hasira na mikwaruzo ikatoka ndani. "Wewe Nani"???

Nikajibu kwa kujiamini nikijua wako discussion na wenzake.. "Mimi ni Edwin"

Ndani nikasikia kama wanabishana kidogo.

Ghafla jamaa akafungua mlango na kuniuliza huku amekasirika wewe nani? Nikajibu kwa kujiamini. "Kama Grace yupo ndani muulize Edwin ni nani?"

Basi Grace alipoulizwa akakana kunifahamu. Hapo jamaa akaanza kunishushia kipigo. Kutokana na mwili mdogo nilionao jamaa alinipga kwa kweli huku akitishia kunipigia kelele za mwizi.

Basi baada ya pale nikaenda hospital kupata matibabu. Nikaamua kumtaarifu mama yake Grace. Mama Grace alishangaa sana na kudai mbona Grace alimtaarifu tumeachana kwa Mwezi sasa?

Nikachanganyikiwa zaidi. Nilipopeleleza zaidi kwa rafiki yake mmoja, nikagundua jamaa ndio anamgharamia Grace kila kitu na kias nilichotoa kwa Grace ilikua hela ya chumvi tu..

Hapa nilipo nina maplasta usoni na sehemu nyingine.

Nisaidieni nichukue hatua Gani kisheria juu ya huyu jamaa? Je akisema nilitaka kuiba nitajitetea vipi? Ushauri wenu ni muhimu sana

Note
Nimetumia majina ya kweli ili kama Grace yupo humu ndani ujumbe umfikie na ajue ameniumiza sana moyoni kwa usaliti aliouonyesha mchana kweupe.

Asanteni

Nakushauri utumie njia wanazotumia vijana wa kisasa wa Kichaga
 
Pole sana ndugu yangu ,achana na huyo Grace kwani siku moja hatakumbuka yote aliyofanya kwako .Lazima arudi kwa machozi mengi sana na kuomba msamaha sana lakini wewe achana nae kabisa kabisa sasa fanya yako pia tafuta wako huyo sio wako tena.But" what's goes around comes around" hatajuta sana huyo Grace mwenye tamaa ya fisi.
 
Ahahahah..dah japo nipo kitandani naumwa hii thread imenichekesha sana.Pole mkuu msahau uyo msaliti tofauti na hapo unaweza jikuta unaua yeye na baunsa wake hakuna. mnyonge duniani ni maamuzi na timing tu.Mungu akupe uvumilivu
 
inauma sana, hakuna kitu kibaya kama kudhalauiliwa kiasi, jamani wezangu niwaulize je kama kijana angekuwa anayo kiunoni si majanga???? Si kwamba anaua kwa ajiri ya mwanamke, bali ni kwa ile hali ya dharau, kibaya zaidi unapigwa mbele yake, na huna la kufanya.. wadogo zangu dada zangu ni nani kawaloga? Mbona hamtosheki? Pole sana mtoa mada hayajanikuta lakini imeniuma saana sana!.
 
kweli inaonyesha silaha zikiwa nje nje mauaji yatakuwa mengi sana.

Unafikiri kaka Edwin angekuwa na bastola tungekuwa na stori gan kwenye magazeti ya Jana na leo?
 
Du!Nimesoma hii habari mwili wote umenisisimka,pole sana ila mwanaume haiwezekani umvishe mwanamke pete halafu akukane na kichapo ukipate,lazima ufanye namna ya kupoza machungu la sivyo hutoweza kumudu maisha ya kimapenzi maana tukio hilo litakuandama maisha yako yote na hutofurahia kuwa na mwanamke na ukamuamini.
 
mtafute kibonde mwenzako ili usishushe adhi yako mimi sistahili kuwa mpenzi wako."kimbia bro maisha yako yote usije kumuamini mwanamke % zote,pole
 
Tafuta bastola mkuu.... hata hivyo pole kwa kichapo! hiyo ndio taswira katika taifa
 
mtafute kibonde mwenzako ili usishushe adhi yako mimi sistahili kuwa mpenzi wako."kimbia bro maisha yako yote usije kumuamini mwanamke % zote,pole

Kweli kabisaa. Kwa sasa mwanamke pekee ninayemuamini ni mama mzazi tu.
 
kweli inaonyesha silaha zikiwa nje nje mauaji yatakuwa mengi sana.

Unafikiri kaka Edwin angekuwa na bastola tungekuwa na stori gan kwenye magazeti ya Jana na leo?

Hata hivyo nitaitafuta mkuu. Roho iliniuma sana siku ile.
 
..ulipokosea we ni hapa "Nikajibu kwa kujiamini. "Kama Grace yupo ndani muulize Edwin ni nani?" hata ningekuwa mie nakuuliza we nani hujibu vizuri ningetoka na kukudunda ka alivyofanya jamaa..lakini pole sana mkuu, ndo maana mie nkaamua kuendelea kutengeneza PESA hawa viumbe wallet yako ikiwa haina mtuno mbona utasasidiwa tu..ha haha haha haha hahaha jamani sijui umepasuka na mdomo manake hadi plasta ujue kipigo kilikuwa HEAVY..imebaki story kitaa jamaa kamegewa demu wake na kipigo juu...
 
mabinti kama hawa huishia kuliwa tu hawawezi kuolewa
hata huyo anaegharamia atamwacha soon ameshajua ni kicheche.
ndugu achana nae Mungu ameshakuonyesa hakufai
kama keshawaambia wazazi mmeachana wakati sio kweli huyu hafai kua mke
wanawake wako chungu nzima tena wazuri zaidi yake usinganganie kisichonganganika.
 
Grace nitamsahau tu.. Ila kurudisha mashambulizi kwa jamaa ni risk nyingine hiyo.

Ila ni risk ambayo kiume ni lazima kuibeba, si vyema ku acknowledge defeat kirahisi namna hiyo. Kamwe siwez kumuacha mtu wa aina hii. Umle baby wangu na kichapo unipe!!!!! Tutachoma nyumba aisee ni bora nife kwa kuitwa mwizi lkn kabla sijafa............
 
ndo maana sipendi wanaume wasiofanya mazoezi na wenye umbo dogo.
Pole sana
 
Back
Top Bottom