Maumivu ndani ya tundu ya haja ndogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maumivu ndani ya tundu ya haja ndogo

Discussion in 'JF Doctor' started by Amosam, Jun 22, 2009.

 1. Amosam

  Amosam Senior Member

  #1
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna jamaa yangu anaomba msaada wa ushauri kimatibabu kwani anasumbuliwa na maumivu katika eneo la shingo ya uume wake.Tatizo hilo amekuwa nalo kwa zaidi ya miaka saba sasa kwani ameshakwenda katika hospitali nyingi kupata matibabu lakini bado hajapona.Baadhi ya madakitari walipompima walimwambia ana mchubuko ndani ya urethra na wakampatia dawa za antibiotic lakini pamoja na matibabu hayo bado hakupata nafuu.Akaenda kwa madakitari wengine wakamwambia ana tatizo la ugonjwa wa zinaa hali iliyomfanya achanganyikiwe kwani kwa tabia yake na ya mkewe hakutarajia kitu kama hicho kutokea(hawa jamaa ni walokole wa hali ya juu).Yeye pamoja na mkewe wakapatiwa matibabu(sindano za penadol)-ziliwatesa sana kwa uchungu,pamoja na tiba hizo bado jamaa anaendele kusumbuliwa na tatizo hilo. Akaenda hospitali nyingine akaambiwa ni mchubuko tuu unaomsumbua kwani wakapimwa yeye na mkewe magonjwa yote ya zinaa hawakukutwa nayo,akapatiwa tiba ya antibiotic tena lakini bado jamaa anasumbuliwa.Kuna wakati anaweza akawa fiti karibu wiki nzima lakini baadae hali hiyo hujirudia.
  Wana JF wenzangu wenye utaalamu wa magonjwa na matibabu naomba msaada wenu wa ushauri ili huyu jamaa yangu aweze kutibiwa na kupata nafuu.Nawakilisaha.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hayo maantibiotics yatamuua....amtafute urologist haraka....atakuwa na stricture huko kny njia ya mkojo....tiba yake ni operation ndogo inaitwa DVU! Lakini kabla ya kufanyiwa hii kitu, kunavipimo anatakiwa akavifanye.....! Pale tumaini, Aghakhan, Muhimbili, Regency...wanafanya hii kitu!

  Tatizo la hii DVU kama hata zingatia mazoezi fulani ...hali hii huwa inajirudia....na solution yake huwa ni hiyo kitu tu!

  Can PM nikupe contact za baadhi ya urologists ninaowafahamu!
   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
 4. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pole sana kwa matatizo yaliyomsibu huyo ndugu yako. Ushauri aliokupa Next level ni mzuri na muhimu. Direct Vision Urethroscopy (DVU) ni aina ya kipimo ambacho humsaidia urologist kuitazama urethra kwa macho yake mwenyewe (direct) pia kama kuna stricture au aina yoyote ya kidonda ni rahisi kuiona na kuitibu hapohapo kwahiyo naona ni muhimu kuifanya DVU kwa urologist kwanye hospitali ulizo tajiwa.
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Amtafute urologist, pia angalie vyakula anavyokula na kiwango cha maji anachokunya
  asichoke wakati mwingine inachukua muda mrefu sana kungudua chanzo na tatizo la ugonjwa husika ,pia ningemshauri kwenda kwenye hospitali za rufaa za serikali hata kama kuna foleni sana na tabu sana kuwaona wataalamu lakini vipimo vya maabara mara nyingi huwa vya uhakika
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  pole sana mkuu!
  wataalamu waliotangulia wameshauri vizuri tu.napenda kukusisitizia tu wakamwone mtaalam 'urologist' ili akushauri kitaalamu zaidi.

  POLE SANA!
   
 7. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu ushauri wako umezingatia uwezo wa mgonjwa? Unamshauri mwenzio kutofanya operation yoyote bongo, mbona husemi akafanye wapi....china,au kenya or India? Na kama uwezo wakwenda huko kwingine hana...afanyeje?

  Ingekuwa bora zaidi useme operation za bongo zina matatizo gani pia ile wote tujifunze hapa!
   
 8. Amosam

  Amosam Senior Member

  #8
  Jun 24, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nashukuru wote mliochangia na ushauri wenu utazingatiwa,ahsanteni sana.
   
Loading...