Huwezi kumzuia mtu mzima kufanya kitu, but at least unaweza wewe ukajiweka on the safe side, ukamuacha yeye aendelee na upuuzi wake
Naheshimu maamuzi yako lakini, coz sijui ilikuwaje ukawa hivyo. If you don't mind na kama upo free, unaweza ukanipa tu hiyo story my dear. Kikawaida kutakuwa na kitu cha kujifunza/ kukumbushana kwenye hiyo story
Hahahahhahahahah acha nicheke kwanza
Ni hivi niliolewa 2010 na mwanaume niliyempenda kwa moyo wote.
Ndoa ikawa tamuuuuu sanaaa tamu kweli (nilikuwa nawaambia rafiki zangu mume wangu hata aje mwanamke ameumbwa vipi hajavaa nguo hata moja hatamtamani, nilimuamini sana na before marriage tulishakaa kama miaka mitano hivi so nilijiaminisha).
Basi bwana mambo yakabadilika weeee hadi ikafika muda mume nyumbani harudi hata wiki ila kazini yupo muda wote. Iliendelea hivyo hadi tukatengana (nakata story)
Basi baadae tukasuluhishwa pale tukarudiana (simu pia ilichangia hadi tukatengana), basi maisha yakaendelea ila ule upendo ukawa umepungua kwa upande wangu, mume akajitahidi sana kunirudisha kawaida akawa mtulivu kweli kweli taratibu (na wanawake tulivyo) nikajikuta narudisha upendo vile vile japo kuna muda nakuwa na wasi wasi.
(Tuokoe muda), kuna siku nikawa naumwa nimelala nimeshindwa hata kupika nikampigia simu kumwambia, akarudi kama saa 3 usiku kakuta nimelala, tumesalimiana kaniuliza unaendeleaje na vitu kama hivyo, baadae pale kitandani akakaa ila hatazamani na mimi akawa busy na simu hadi saa tano (me nilipitiwa na kausingizi ka homa) nashtuka nakuta mtu yupo busy bado, akaniomba maji ya kuoga ki ukweli sikuwa naweza hivyo nikamuomba ajiandalie alichukia kwa sababu nilimzoesha ni lazima ni muandalie maji na lazima tuoge wote hata kama nimeshaoga ila akaanda akaenda kuoga.
Mimi nikawa naitamani sana ile simu, nikaishika yeye yupo bafuni, yaani kufungua tu kwenye sms nakutana na chatting moja mataa (baby, honey swty darling majina yote yale mazuri mazuri unayoyajua) ila kubwa zaidi ni sms za pitia ofisini nikuone mwanaume ndo anamtumia mwanamke nimekumiss nahitaji kufanya mapenzi na ww, your so sweet na vitu kama hivyo mwisho kabisa wakamalizana na hii, "kesho saa tisa basi tukutane kule kule wewe tangulia ukifika niambie" (nilivyofika hapa nilipona nikawa mzima kabisaa).
Basi mume katoka kuoga nikamuuliza, jibu lake sasa hahahahahahahah "alikwambia ushike simu yangu nani umeyataka" (nililia sana zaidi ya sana haielezeki kumbuka me nilikuwa naumwa nipo kitandani yeye ndo anafanya hayo). Niliumia sana.
Nikajitahidi nijidai mkali nikaishia kupewa maneno ya kuumiza zaidi.
Kweli Mungu yupo. Nilijikuta nawaza niamke nisali tu, basi hivyo hivyo huku nalia nikaingia kuoga nikapata udhu vizuri nikaswali (me ni muslim), niliswali huku machozi yanatoka, niliamua kumlilia Mungu nilitumia muda mrefu sana hadi pale moyo wangu ulivyopoa.
Nilivyoridhika nikapanda kitandani yeye alivyoona ninaswali akalala, basi nikajiandaa kulala ila kabla nikamuamsha nikamshika mkono nikamwambia "nisamehe mume wangu", akaniuliza kwanini nikamjibu "kwa sababu nimeshika simu yako nisingeshika haya yote yasingetokea, nisamehe sana, nakupenda mume wangu".
Mh machozi yakamtoka akaniambia nisamehe pia mke wangu, nikamjibu nimekusamehe na moyo wangu mweupe, sina kinyongo na wewe, akaniambia nakupenda mke wangu hawa nawapotezea muda tu ndio maana nimekuoa wewe, nikamjibu najua mume wangu na nakuahidi sitashika simu yako tena. Baada ya HAPO SIKUSHIKA SIMU YAKE TENA NA SITASHIKA SIMU YA MWANAUME TENA
Ila baadae tuliachana. So kushika simu ya mtu ni kujitafutia matatizo, mwanaume ukigundua hajatulia unaamua tu au kumvumilia (ndo ile kwa shida na raha) au kuachana nae ila kushika simu unajiumiza na ukimuuliza anaweza kukujibu ukahisi dunia nzima inakuona unavyojibiwa