Maumivu kifuani na tumboni wakati wa Kula Chakula

Mjasiriamali M

Senior Member
Jan 15, 2013
142
71
Habari za Jion, jamani tangu juzi nimejigundua nna pata maumivu kuanzia usawa wa kifuani(chembe) mpaka tumboni, yaani nikila chakula nakifeel kinavyopita mpaka kinafika mwisho, mwanzoni nilihisi nakula bila kutafuna vizuri na kumeza na maji lakini bado leo ni siku ya 3 naendelea kupata maumivu haya, nimekunywa maziwa na kula matango lakini sijapata relief kivile, nawasilisha huku naimani naweza pewa ushauri mzuri.

cc: MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Pole sana ushauri mzuri tutakao kupa kwanza ungelienda Hospitali kumuona Daktari ndio ungelifanya

jambo la maana sana kuliko kuleta hapa mkuu.@
Mjasiriamali M huenda isijekuwa ni dalili ya vidondavya

tumbo (Ulser) hivyo vinakuanza?


Dalili za vidonda vya tumbo

Vidonda vya tumbo huambatana na maumivu ya kuchoma, kuwaka katika sehemu ya juu ya tumbo. Kwa kuwa aina mbili zote za vidonda vya tumbo hutofautiana, ni vizuri zaidi kuelezea kila kimoja.

(a) Vidonda vya tumboni

Maumivu ya vidonda vya tumboni mara nyingi hukaa katikati, takribani kati ya nusu ya chini na kwenye kitovu na mara nyingi kula huifanya kuwa mbaya zaidi. Tofauti na maumivu ya vidonda vya utumbo, maumivu ya vidonda vya tumbo mara nyingi hayaishi mara moja pindi yanapoanza.

(b) Vidonda katika utumbo

Maumivu ya vidonda vya katika utumbo pia hukaa pale pale (kama katika vidonda vya tumboni). Tofauti na vidonda vya tumboni, katika vidonda vya utumbo mara nyingi kula husaidia kupunguza maumivu.

Tofauti nyingine ni kuwa, wakati katika vidonda vya tumboni maumivu huongezeka haraka baada ya kula chakula, katika vidonda vya utumbo inaweza kuchukua saa mbili au tatu. Tabia nyingine ya vidonda vya utumbo ni kupotea kwa majuma au hata miezi bila sababu ya wazi.

Mtu anaweza kulalamika kuwa anapata maumivu baada ya chakula. Hii ni kutokana na msisimko wa mnyunyizo wa asidi ambao hububujika kwenye kidonda. Katika vidonda vya duodeni, huchukua takribani saa mbili hadi tatu ili asidi ifike sehemu ya kidonda.

Utambuzi wa vidonda vya tumbo

Utambuzi wa kubainisha vidonda vya tumbo hujumuisha X-Ray. Upimaji wa tumbo na vilivyomo ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana kama 'endoskopy' au 'biopsy', ambayo huyakinisha hali halisi.



peptic-ulcer.jpg


USHAURI WANGU


Nenda Hospitali kisha uje hapa utupe feedback Pendelea pia kunywa maji ya Uvuguvugu kabla

ya kula chakula na unapo amka asubuhi kunywa hayo maji japo glasi 3 kabla kupiga mswaki

kisha kaa saa 1 bila ya kula kitu baada ya saa 1 kupita waweza kula. Na mchana kunywa tena

glasi 2 kabla ya kula chakula kisha ukae kama saa 1 ipite ndio waweza kula chakula n ausiku

kunywa tena glasi 1 kisha kaa saa 1 ipite waweza kula chakula cha usiku. Na wakati wa kwenda kulala

usiku kunywa glasi moja maji ya uvuguvugu kisha lala fanya hivyo kila siku.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom