Maulid Said Mtulia umepotoka!

Ubavu

JF-Expert Member
Jun 19, 2012
2,791
3,236
Nikiwa kama kijana niliyekulia Mwananyamala na kuishi wilaya ya Kinondoni, nimesikitishwa sana na kitendo cha kujiuzuru ndugu Maulid Said Mtulia kuwa Mbunge pamoja nafasi zake zote ndani ya chama cha CUF.
Sijashangaa kutokana na kitendo hicho hasa ukizingatia kwa jinsi upepo wa kisiasa unavyo vuma, kilichonipata naweza kukielezea kama kukata tamaa (disappointment) na kijana mwenzangu.

Wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, nakumbuka jinsi Mtulia alipopata shida kuyafikia masikio ya wanakinondoni kupitisha azma yake ya kuwawakilisha Bungeni, hasa ukizingatia kuwa alikuwa ni mpya kwenye macho ya wengi. Kwa juhudi kubwa tawi la KUNDUS Mwananyamala pamoja na Ofisi ya CUF wilaya zilisababisha kijana huyu kupata kutambulika na mwisho kuibuka kidedea!

Ni kweli usiopingika kuwa juhudi binafsi za bwana Mtulia zilisaidia yeye kupata ridhaa ya wananchi, lakini kwa asilimia kubwa (zaidi ya sabini) zilitokana na juhudi za wananchi hasa wakereketwa wa CUF na CHADEMA waliohamasisha watu wengi kujitokeza kupiga kura na mwisho walikesha usiku kucha kuzilinda kura zile ili zisiibiwe na CCM.

Chakushangaza baada ya kazi kubwa iliyozaa mafanikio makubwa ya Vijana wa UKAWA kuisambaratisha ngome ya CCM KINONDONI na kumuibua Mtulia kidiedea miaka miwili pekee imetosha kumsahaulisha bwana huyu NGUVU YA UMMA iliyomuweka pale alipo.

Sijui kama amenunuliwa au ni kwa mapenzi yake toka moyoni, ila ninachosema mimi ni kuwa MTULIA UMEPOTEA! Mtulia wewe uliyefungua kesi mahakamani ili kuzuia serikali ya rais Magufuli isivunje nyumba za watu masikini zilizopo maeneo ya Kinondoni Mkwajuni, leo hii unaungana na serikali ileile iliyosababisha majonzi na simanzi kwa wananchi hawa! SIJUI UTAWAANGALIA VIPI WANANCHI HAWA!

Ninachoweza kukwambia ndugu yangu Mtulia ni kuwa waliokuweka hapo ulipo ndio watakao kushusha. Mark my words Mr. Mtulia, mwaka 2020 usitegemee kurudi na kuwa mbunge wa Kinondoni kwani WANANCHI HATUTASAHAU!
Kama umeahidiwa kuwa utapatiwa jimbo la Kinondoni jua fika kuwa UMEONGOPEWA!

NGUVU ILIYOTUMIKA KUKUWEKA HAPO ULIPO NDIO NGUVU HIYOHIYO ITAKAYOTUMIKA KUKUTOA HAPO ULIPO!

Na Zuberi Mohamed Ubavu
 
Hivi atathubutu kurudi jukwaani kuomba kuchaguliwa tena? Sidhani. Huyu kapotezwa mazima kwenye siasa za bongo labda ateuliwe viti maalumu akapige vigelgele kule! Katia aibu mno! Kwanini hakuita mkutano wa wanakino awaambie nia yake?
 
Ndio wabunge wenu wa darasa la saba/form four failure, uwezo mdogo wa kufikiri, ukimpa pipi wa kwako.
 
Nimeishia kucheka tu nikifikilia jinsi tulivyoanza kumtoa diwani wa CCM kata ya Makumbusho Mr Mtayoba kumuweka Harub tulivyofanikiwa kuchukua udiwani tukaanza mikakati ya kuchukua Jimbo kutoka Kwa Iddi Azzan tukafanikiwa nakumbuka tulikesha Mimi nikiwa mmoja wao ambaye tulitumia mpaka pesa zetu za mfukoni ilimradi CCM tuifute Kinondoni.

Bodaboda na gari zote tulizo tumia Kwa kukodi na kuanzima zilikunywa mafuta mpaka zikatapika tulijitajidi kutumia pesa zaidi ili watu wetu wasije wakashawishika Kwa pesa nikafikiria muda na pesa niliyotumia naishia kucheka tu
 
Yaani uamuzi aliochukuwa huyu maulid,ni kwamba kawafanya wale wote waliomchagua na kumpa ubunge ni wapumbavu;na kwamba yeye ndio mwenye akili,kitu ambacho ni kibaya sana.

Haya masikitiko na huzuni uliotuachia hapa kinondoni kwa usaliti wako ni zaidi ya msiba.

Machozi ya hawa wapiga kura wako yanatosha kukulaani kwa level hata ya kugongwa au kupata ajali ya gari; au ukajikuta umejiua mwenyewe."Yuda iskarioti alimsaliti yesu. Alipewa vipande 30 vya fedha. Matokeo yake, hata hiyo fedha hakuifaidi. Baadaye alijiua mwenyewe kwa kujinyonga.

Ndo ujue ubaya wa usaliti. Kama 2015 ulijua ccm wanakupenda kweli, kwanini hukugombea huo ubunge kupitia ccm? Sisi tungeweka mgombea wetu mwingine wa upinzani kuliko ulivyotusaliti.

Hukututendea haki.
 
Na Ukawa yanatapatapa!

Maji kupoa na kurejea kwenye Ubaridi sio Breaking news Tena !
 
mkwawa complex,

Mkuu yaani mie hata nisikie wema mia mbili wamehama kwenda CCM wala nisingeumia..!

Mtulia watu waliwekeza mpaka utu wao bila ya malipo ili jamaa ashinde..! Watu walikuwa wanahamasisha mpaka CCM wakereketwa wampigie kura yeye..!

Leo hii wote amewasaliti!
Nadhani kwake alidhani ni siasa tu wakati wananchi kwao ndio maisha yao kabisa..!
 
Mkuu Ubavu mimi nilisoma hiyo shule jirani hapo miaka ya 80, kila nipitapo hapo tawi la Kundus lazima nawakuta wanachama wakiendelea na harakati.

Mimi ni CCM lakini nafahamu namna wanacuf wa Mwananyamala walivyompigania Maulidi ilibakia kidogo jamaa apokee 300m kutoka kwa Idd lakini wanangangari walisimama kidete!!
 
Ila Nyalandu yupo sahihi...
Yaani mkuu.! Hata leo zitto akisema anahamia CCM mie sitaumia..! Issue ya Mtulia watu wali-sacrifice mambo mengi sana ili jamaa ashinde..! Hawezi akatoka kirahisi rahisi tu..! Angewaita wananchi wa kinondoni akawaambia mwenyewe na atoe sababu za msingi kwelikweli..!
 
Back
Top Bottom