Mauaji ya watu 3 Ilala - Dar

fimbombaya

Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
47
Reaction score
12
Nimepita hapa maeneo ya ilala karibu na club ya wazee, kuna mauaji yametokea kwa watu wawili kupigwa risasi na muuaji nae kajiua,pia wawil wamejeruhiwa. Taarifa zaid ntawajuza.


Kwa mujibu wa shuhuda wa Clouds FM.

Mauaji hayo yamefanyika maeneo ya Ilala, kataja maeneo kwa jina lake maarufu (bahati mbaya sikudaka vizuri). Inadaiwa kuna gari ilikua inatoka ndani ya geti kutoka ikiwa na dereva mwanaume, abiria mwanamke mbele, na abiria wengine wawili wakiwa seat ya nyuma.

Pembeni hapo kulikua na jamaa kasimama. Inadaiwa alishushwa hapo dakika chache toka katika tax, walipotokeza abiria hao kupitia gari yao alitoa silaha yake na kupiga risasi gari akilenga zaidi abiria wa mbele pande zote kisha na nyuma. Baada ya kumaliza hapo muuaji huyo naye alijipiga risasi na kufariki hapo hapo.

Dereva na abiria wake wa mbele wamefariki dunia, huku abiria wa nyuma mmoja mama mtu mzima kajeruhiwa na risasi mgongoni na dada mwingine kujeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni.

--------------------------------
Ni maeneo ya Club ya wazee!! ilala Amana. kuna jamaa kapiga watu wawili risasi kwenye gari na kuwauwa hapo hapo na kujeruhi wengine wawili na kisha kujimaliza yeye mwenyewe. hii habari ni kwa mujibu wa breaking news ya mawingu FM.


 
Ndo nasikiliza clouds wameiongelea hiyo kwakweli ni jambo ambayo limesikitisha sana
 
Mimi nimepita hapo muda si mrefu risasi zilipolia watu walifikiri ni majambazi na walijaribu kufuatilia ili kuwadhibiti, watu walikuwa wengi sana kila upande kuzunguka eneo la tukio. Hapakuwa na askari polisi na hata wale wa usalama barabarani wanaokuwa pale Bungoni hawakuonekana.
 
Mbona habari zinadai kwamba mtu kamuua dada yake na shemeji yake...daaaah hii dunia bhana ni noma ..RIP waliokufa.
 
Hivi hizi silaha watu wanaazimana au zinatolewa kwa kufuata taratibu?
Wapumzike kwa amani marehemu na hao majeruhi wapate nafuu ya haraka
 
Nimepita, ngoja nikapate updates za Kapuya.
 
Mfanyabiashara wa magari wa mwanza amemuua dada wa mchumba wake na yeye kujimaliza,kisa wivu wa mapenzi na kumjeruhi mchumbake,na mtu mwingine,. Source radio wapo na Masau bwire.
 
Watu wengine hamnazo unajiua kisa mapenzi!
 
NI MAUAJI YA KUTISHA SANA YALITOKEA ILALA,NJE YA "M"HOTEL,JAMAA ALIKUJA SOFTLY HUKU AKINYWA SUPU KAMA HAKUNA ANALOTAKA KUFANYA! KWELI KILLER HAS NO CLEAR FACE,R I P alls
 
Watu wengine hamnazo unajiua kisa mapenzi!

Ni maeneo ya Club ya wazee!! ilala Amana. kuna jamaa kapiga watu wawili risasi kwenye gari na kuwauwa hapo hapo na kujeruhi wengine wawili na kisha kujimaliza yeye mwenyewe. hii habari ni kwa mujibu wa breaking news ya mawingu FM.
 
itv wametangaza pia.
turudi kwenye issue ya kapuya ndio habari ya mujini kwa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…