Mauaji ya wanawake Mto wa Mbu Kama kawa

Mauaji ya wanawake Mto wa Mbu Kama kawa

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Wimbi la wanawake kuendelea kuuawa katika Mji wa Mto wa Mbu wilaya ya Monduli Mkoani hapa ,limeendelea kushika kasi kufuatia Mwanamke mwingine kuuawa na kunyofolewa viungo vya mwili.

Mwanamke Anastazia Paulo (62), akikutwa ameuawa katika nyumba aliyokuwa anaishi huku mwili wake ukiwa umenyofolewa macho ,sehemu za utupu na kuvunjwa mguu wake wa kushoto.

Tukio hilo la kumi kuuawa kwa wanawake huyo ndani ya miaka mitatu katika mazingira ya kutatanisha, yanayohusishwa na imani za kishirikina, ulevi, wivu wa mapenzi na ukatili wa kijinsia jambo ambalo limeibua hofu kwa wanawake wa mji huo ambao wamelazimika kujifungua ndani inapofika majira ya saa 12 jioni na kuamka SAA Mbili asubuhi.

Akizungumzia kuuawa kwa Anastaazia ,mtoto wa marehemu ,Hadija Gidion alisema kuwa mama yake aliacha kuonekana na kutopatikana kupitia Simu yake tangu April 14 mwaka huu na kugundulika akiwa amefariki dunia nyumbani kwake baada ya siku tano.

Hadija ambaye anaishi eneo la Losirwa kati akiwa na ndugu zake wengine aliamua kwenda nyumbani kwa marehemu mama yake eneo la Nyasi kwa lengo la kujua nini kimemsibu.

Anasema Mara baada ya kufika nyumbani kwa marehemu walikuta mlango haujafungwa na kitasa na alipousukuma na kuingia ndani alikunana na mkono wa mama yake mlangoni na alipoangalia ndani zaidi aliona mwili wa marehemu ukiwa umeharibika vibaya.

"Niliuona mwili wa marehemu mama yangu ukiwa umetobolewa na kutolewa macho,pia kizazi hakipo na tumbo lake lilikuwa limevimba na kuwa gumu sana " Alisema

Alisema alitoa taarifa polisi ambao walifika eneo la tukio wakiwa wameambatana na daktari ambaye aliufanyia uchunguzi mwili huo na kubaini kuwa alikuwa amekufa na kifo chake kimetokana na majeraha.

Baadhi ya majirani wa nyumba aliyokuwa akiishi Anastazia eneo la Nyasi walisema juzi baada ya kutomuona walitilia shaka na kuamua kuvunja mlango uliokuwa umefungwa.

“Mlango ulipovunjwa mwili wake ulikutwa tayari umeanza kuharibika na tulitoa taarifa polisi, wakafika na kuanza uchunguzi wao.”

Anastazia ambaye alikuwa akiishi peke yake ameacha watoto wanane na mwili wake ulizikwa nyumbani kwake baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Jonathan Shana alisema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha kifo hicho na tiyari watu saba wanashikiliwa kwa mahojiano

Baadhi ya matukio ya mauaji yaliyowahi kutokea nipamoja na tukio la marehemu Ester Fisso (26) alibakwa kisha kuuawa kikatili.

Mbali na Ester wwngine waliuawa na kutambuliwa ni Ruth Elias, Vick Kivuyo, Elizaberth Hango, Shikweshi Boaz, Mwapwani Mawezi

IMG_20190511_134743.jpeg
IMG_20190511_134908.jpeg
 
Wamasai na ushirikina wapi na wapi mi najuaga hawa jamaa wako busy na ng'ombe tu hata mambo ya dini sijui makanisa hawajui
 
Kuanzia SIRO mpaka OCD wapo tu ofisini. Wapo tu wanangoja Rais awafundishe la kufanya .
 
naona huko imani imepungua,inabidi tumtume kakobe au Gwajima wapeleka imani ya upendo huko
 
Back
Top Bottom