Habari haiendani na kichwa cha habari yenyewe...haielezi hayo mazito yenyeweWakati mauaji ya watu wanane waliochinjwa usiku wa kuamkia juzi mkoani Tanga yakizua maswali lukuki na kuzidisha hofu, imebainika kuwa wauaji waliwachinja wote kuanzia sehemu ya chini ya kisogo.
Watu hao waliuawa kwa kuchinjwa katika kitongoji cha Mabatini, Kata ya Mzimama, Tanga.
Tukio hilo lilifanywa nje ya nyumba ya mwenyekiti wa kitongoji hicho, ikiwa ni mwendelezo wa mauaji ya uchinjaji yaliyoikumba nchi tangu mwanzoni mwa mwezi uliopita.
Mauaji hayo yametokea wakati mkoa wa Tanga ukizidi kukumbwa na matukio yanayohisiwa kuwa ni ya kigaidi tangu polisi kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) walipopambana na watu wasiojulikana kwenye mapango ya Amboni Januari 26 mwaka jana.
Chanzo: Mwananchi
Labda mazito yenyewe ni marehemu, kuchinjwa kuanzia chini ya kisogo.Habari haiendani na kichwa cha habari yenyewe...haielezi hayo mazito yenyewe
Kwangu mimi hayo ni mazito sana, kumchinja mwanadamu mwenzako kama kuku, sasa polisi tunapoomba vibali vya kununua Silaha au kumiliki Silaha mtoe mapema, ona sasa hapo angekuwepo mmoja tu mwenye bastola sasa hivi ingekuwa habari tofauti
Wewe inaonekana uko gerezani hujui kituChina raia hawana silaha na haya hayatokei!
Cha maana ni kupiga marufuku kumiliki silaha..ni Majeshi TU.
Kweli?RPC na RC wa Tanga wafungwe maana wananchi waliripoti na Jamaa wakajitokeza kwenye media na kukanusha akiwemo pia Advero Msemaji wa Jeshi la Polisi aliyesema kuwa nchi iko salama.
Fuatilia utaujua ukweli zaidi, next time wasiropoke tu, na huenda tatizo ni kubwa kuliko tunavyodhaniKweli?
Jamaa umeandika ugoro. Kwani silaha iliyotumika hapo kuwachinja watu ni silaha gani? Na matumizi na upatikanaji wake ukoje?China raia hawana silaha na haya hayatokei!
Cha maana ni kupiga marufuku kumiliki silaha..ni Majeshi TU.