Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,741
Aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Majambazi Mkoa wa Morogoro, Marehemu, ASP Elibariki Israel Palangyo.
HALI ni tete! Matukio ya mauaji ya askari polisi sasa ni tishio. Hilo limebainika kufuatia Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Majambazi Mkoa wa Morogoro, ASP Elibariki Israel Palangyo (53) kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wenye harufu ya ugaidi, Uwazi limechimba.
Tukio hilo la lililoacha maswali mazito kwa majirani, lilijiri Agosti 4, mwaka huu nyumbani kwake, Yombo ya Kilakala wilayani Temeke jijini Dar ambapo ni siku chache tu baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni magadii kuvamia Kutuo cha Polisi Stakishari, Dar na kuua watu saba, wakiwemo polisi wanne.
ALIVYOUAWA
Simulizi za kidaktari zinasema kuwa, watu hao walimvamia marehemu chumbani kwake, wakampiga risasi nne sehemu ya moyo, wakamkatakata mapanga na kumtoboa macho.
Hayo yalifanyika huku binti yake aitwaye Neema Elibariki ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Kibasila, Dar akishuhudia.Akisimulia mkasa mzima tangu kuvamiwa mpaka kuuawa kwa baba yake na yeye kupewa msukosuko, Neema alisema:
"Kwanza sikutegemea kuwa leo hii ningemkosa baba kutokana na mauaji ya kikatili, kidhalimu na kinyama. Hii ni hatari sana kwa usalama wetu sisi wananchi na polisi kwa ujumla. Kama imetokea hali ya magaidi kupenya na kujiimarisha na kuanza mauaji kwa kasi namna hii, usalama unatoweka."
AANZA NA SIKU YA TUKIO"Nakumbuka siku hiyo (Agosti 4) saa tisa usiku, uvamizi ulitokea. Mji wetu uligubikwa na milio ya risasi. Nilishindwa kupata jibu kwa haraka ni kitu gani kilichotokea, tulikaa kimya.
"Kabla ya milio ya risasi tulisikia watu wakiongea kwa sauti ya chini huku geti kuu alionekana mtu akifungua. Ndipo wakaingia watu zaidi ya kumi wakiwa wamejifunika vitambaa vyekundu usoni.
"Baadhi ya watu hao walikuwa na bunduki, wengine mapanga. Walikuja moja kwa moja hadi mlangoni, wakavunja geti na mlango kisha wakafanikiwa kuingia sebuleni. Hawakujua pa kwenda. Baadaye waliingia chumba cha dada ambaye alikuwa amelala na mfanyakazi wa ndani. Waliamshwa wakanyang'anywa simu.
Askari, ameuawa.
"Walipotoka huko, walihamia chumbani kwangu. Mimi nilikuwa nimelala na mdogo wangu. Ana umri wa miaka mitano. Wakatutoa sebuleni, wakamtishia mdogo wangu awaoneshe chumba cha baba.
Mdogo wangu alifanya hivyo. Wakajaribu kubomoa mlango ikashindikana. Mmoja alitoka nje na kuchukuwa tofali, wakaupiga mlango ili ufunguke ikashindikana, wakapiga risasi komeo ikafunguka.
Wakati huo walikuwa wametushikilia."Baba naye kumbe alishaamka. Alijua kuna uvamizi kutokana na ile milio ya risasi. Nilimsikia akipiga simu mahali kuomba msaada mara kwa mara lakini hadi anakufa hakuna aliyeweza kufika. Pengine waliogopa risasi.
Wale watu wakati wanaingia chumbani kwake, baba alikuwa ameshika panga, akamkata mkono yule wa kwanza kuingia.
"Walimpiga baba risasi za kifuani upande wa kushoto kwa chini, akakimbilia chooni kujificha kwa kujifungia lakini hakuweza, walimuwahi kwa kumpiga tena risasi huku wakimwambia kuwa walichohitaji kutoka kwake ni uhai wake tu. Nilimwona baba akiishiwa nguvu na kudondoka chini."
AJARIBU KUITA WATU KWA FILIMBI
"Kuona vile, nilipata ujasiri, nilichukua filimbi ya kazini kwa baba, nikapuliza kwa lengo la kuita watu waje kumuokoa baba, lakini walinipiga kofi na kunitishia kuniua."Niliamua kuingia uvunguni mwa kitanda kujificha, mdogo wangu alichanganyikiwa, alikaa kimya maana hata yeye alikuwa chumbani kwa baba. Walianza kuangalia vitabu, wakaangalia kitabu cha mama na kukuta bahasha yenye shilingi laki tano na elfu arobaini, wakachukua.
"MKE WA MAREHEMU ALIKUWA WAPI?"
Mama yangu mzazi yeye ni muuguzi. Kwa hiyo wakati baba anauawa yeye alikuwa kazini kwake, Hospitali ya Zakhem, Mbagala (Dar).
"WAONDOKA, WAACHA MANENO"
Jambo la ajabu, licha ya kumuua baba, waliendelea kufyatua risasi ndani. Lakini nje pia nilisikia milio ya risasi. Inaonekana nje ya geti kulikuwa na kundi kubwa la wenzao ambao pia walikuwa wakipiga risasi hovyo. Baada ya muda kukawa kimya, wale wa ndani waliondoka huku wakisema watarudi tena kwa ajili ya kuvamia nyumba nyingine iliyo jirani na yetu huku wakisema nchi itatikisika.
"KUMBE MAREHEMU ALIKUWA NA BASTOLA"
Baba alikuwa na bastola ndani lakini risasi zilikuwa mbali. Nafikiri alishindwa kujua kwa haraka alipoziweka lakini polisi walipofika walikuta risasi nje zilizofichwa. Mama alipata taarifa lakini alikutana na polisi wakiupeleka mwili wa baba Hospitali ya Temeke. Wahalifu hao walitoka na fedha lakini pia walifanikiwa kuondoka na simu saba.
"WALICHOSEMA MAJIRANIBaadhi ya majirani waliohojiwa na Uwazi kwa masharti ya kutotaja majina yao walisema kwamba watu hao baadhi yao walionekana wamezingira eneo hilo huku wakiwa na silaha nzito kwa ajili ya kulinda usalama wa wenzao waliokuwa ndani kwa marehemu.
POLISI WANASEMAJE?
Baadhi ya askari polisi waliohojiwa na Uwazi walisema maisha yao yako hatarini na kuiona kazi hiyo kwa sasa ni chungu kwao kutokana na kuvamiwa, kuuawa na kunyang'anywa silaha kila mara hali inayoifanya nchi itikisike."Kwa upande wetu polisi suala la ajira si kama zamani kwani vijana wamekuwa wakichukuliwa hovyo kujiunga chuoni bila kuzingatia sifa kama zamani. Kuna wahalifu wengi wameajiriwa na wanatumiwa kufanya ukachero kwa manufaa ya vikundi vya uhalifu.
MAREHEMU ALIKUWA DAR KWA AJILI YA KUTOA USHAHIDI
Marehemu alikuwa rafiki yangu na siku moja kabla ya tukio aliniambia ametoka Morogoro kuja Dar kikazi ambapo asubuhi ya Jumanne ya Agosti 4, (mwaka huu) alitakiwa kwenda kutoa ushahidi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kesi inayohusu kundi fulani. Polisi kitengo cha uchunguzi wasimame imara watabaini kitu.
NI MFULULIZO
Mauaji ya kamanda huyo ni mfululizo wa mauaji ya askari polisi nchini ambapo kwa kipindi kifupi tu, askari waliouawa wanafikia saba.
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, ACP Andrew Satta ambaye alikuwepo katika kuuaga mwili wa marehemu ASP Palangyo aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili kufanikisha kukamatwa kwa wahusika wote."Hili ni tukio la kinyama na hatuwezi kuvumilia hata kidogo. Tutahakikisha tunafanyakazi usiku na mchana na tutawakamata wote waliohusika na tukio hilo. Hakuna atakayepona. Naamini baadhi yao wako hapa wanatusikiliza," alisema kamanda huyo.
Mauaji ya Polisi sasa tishio | Global Publishers