Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,141
- 1,982
Salaam Wakuu,
Kumekuwa na mauaji ya kikatili ya polisi na raia. Mauaji haya yalianzia Tanga, Mwanza, Morogoro na kisha Pwani. Mauaji haya yametisha zaidi Mkoa wa Pwani na aghalabu huambatana na uporaji wa silaha.
Tarehe 13 Aprili askari polisi wanane waliuawa kikatili eneo la Jaribu Mpakani, Kibiti Pwani.Waliuawa na 'watu wasiojulikana' walioondoka na bunduki tisa zikiwa full magazine.
Februari mwaka huu 2017,OC CID wa Kibiti Pwani Peter Kubezya, Ofisa Misitu Peter Kitundu, na mlinzi Rashid Mgamba, waliuawa kwa kupigwa risasi kichwani na 'watu wasiojulikana'. Mwenyekiti wa kijiji cha Nyambunda, Said Mbwana, Ofisa Mtendaji wa Kijiji Ali Milandu na mfanyabiashara, Oswald Mrope wote walipigwa risasi na wasiojulikana. Vilevile iliripotiwa polisi kuwapiga risasi wanaume wawili waliovalia ushungi wakiwa kwenye pikipiki waliokataa kusimama, kutii amri ya polisi. Haya yametokea Lindi na Pwani.
Kwa nini wauwaji wanauwa
watendaji wa serikali za mitaa na polisi kisha kupora silaha? Mpaka sasa polisi hawajaweza kutegua kitendawili hiki.Uwezo wa polisi wetu kunusa taarifa za uhalifu na kuzuia mauwaji ni duni. Polisi wana uwezo mkubwa wa 'kiintelijensia' wa kubaini kuwa mikutano ya vyama vya upinzani na maandamano yao vitaleta vurugu. Hutumia nguvu kubwa inayosababisha hata vifo, ili kuizuia. Inawezekana kabisa kuwa mauaji ya polisi na watendaji wa serikali ni mwanzo wa ugaidi. Hata Boko Haram walianza hivi. Ni vizuri serikali ikapeleka polisi wetu kwa mafunzo nje ya nchi ili kujifunza namna bora ya kisasa ya kupambana na uhalifu.
Nawasilisha.