Mauaji ya Muumini wa Waadventista Wasabato, watuhumiwa waomba upelelezi uharakishwe

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
UPANDE wa utetezi katika kesi ya mauaji inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itigi Wilaya ya Manyoni, Pius Luhende (54) na wenzake, umeomba kuharakishwa upepelezi wa shauri hilo.

Wakili wa mshatakiwa, Victoria Revocati, aliomba upande wa mashitaka uharakishe kumaliza upelelezi kwa sababu kesi hiyo haina dhamana.

Hata hivyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida, Consolata Singano, alisema kwa sasa ni mapema mno kulalamikia ukamilikaji wa upelelezi kwa kesi ya mauaji.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Rodey Elias (46), Makoye Steven, Silvanus Lungwisha (50), Elick Paul (31), Eliuta Agustino (43) na Yusuph Yohana (25).

Mapema jana, Wakili wa Serikali Mkuu, Michael Ng’hoboko, alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Consolata Singano, kwamba washitakiwa hao kwa pamoja, walitenda kosa hilo la kumuua mkulima, Isack Petro (28) mkazi wa Kijiji cha Kazikazi Tarafa ya Itigi, Februari 2 ndani ya kanisa.

Alidai walitenda kosa hilo katika Kata ya Kitaraka Tarafa ya Itigi.

Washitakiwa hao saba hawakutakiwa kujibu cho chote kwa vile mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 11.

-Mtanzania
 
ko mkurugenzi bado yumo ndani ama anapewa upendeleo wa kutoka nyumbani na kuhudhuria mahakama maana tz hakuna kishindikanacho
 
Huyu jamaa ndo alikuwa anamletea mademu boss mkuu siku za nyuma
 
Nilishangaa mtu anatoka mahakamani kwa kosa la mauaji alafu anapanda shangingi anarudi nyumbani badala ya gesti ya serikali (jela) only happen in Tanzania
 
Kuna ndgu yngu hapo alikuwa kavu sana na hakutegemea maisha yke yote kama itatokea kukaa ndani haya apambane na hali yake Mungu amsaidie angekuwa ukonga atlist ningempelekea chKula roho mbaya haijengi pole @roydene
 
Mkuu tusiombeane mabaya, case kama hizi unaweza shangaa anakaa ndani hata miaka mitano hukumu bado

Hakuna alie safe kiongozi, niliwah amka zangu ghetto mapema tu sina moja wala mbili, saa nne nikajikuta gest za serikal (lupango), ule usemi wa "Hakuna anae ijua hata sekunde moja ya maisha yake ijayo ndio niliuthibitisha hapo" nilijiuliza sana namna mambo yalivyo badilika haraka hadi najikuta ndani... unaweza shangaa hata wewe kesho vaap uko lupango

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heri wewe umesema!
 
Back
Top Bottom