Mauaji ya Kiongozi wa Walinzi PPF House

Ericus Kimasha

JF-Expert Member
Oct 27, 2006
488
470
Kumetokea mauaji ya Kiongozi wa Walinzi katika jengo la PPF House Samora. Mauaji haya yanakisiwa kutokea usiku wa kuamkia leo J3. Hakuna taarifa za kuaminika juu ya kusudio na wahusika wa mauaji haya. Polisi na vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi wa tukio hili.

Mauaji haya yamesababisha wafanyakazi wa ofisi zote zinazopanga katika jengo hili kuchelewa kuingia maofisini mpaka muda mchache uliopita. Hii ni kutokana na kuofia kuaribu ushahidi hasa alama za damu katika lifti na viashiria vingine vilivyopatikana katika eneo la maegesho ya magari (Underground Parking Yard)

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA

Nikiripoti kutoka ofisi za Jiji, ni Mimi
 
Asante kwa taarifa, nimeshangaa sana kuona watu wengi sana hapo PPF House, bt nikaendelea na safari Kuwahi kibaruani, Hali inatisha,
Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema,
 
RIP Kiongozi wa walinzi.

Tunatumaini polisi watawakamata na kuwawajibisha walioitoa roho yako.
 
RIP kiongozi wa walinzi, ni tunaliomba jeshi la polisi lifanye upelelezi wa kina hadi kuwapata wahusika.
 
Muiteni Leutenant General Shimbo akashughulikie tatizo hili maana yeye siku hizi anasimamia usalama wa raia.
 
Back
Top Bottom