Mauaji ya Albino Tanzania na uongozi mpya

AZUSA STREET

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
2,007
1,893
Mwaka 2010 nilikuwa nchi fulani ya Ulaya nasoma, mmojawapo wa wanafunzi akajua mimi ni mtanzania akataka kuandika thesis kuhusu mauaji ya albino Tanzania. Iliniuma sana na almanusura niikane nchi yangu kwamba mimi sio mtanzania kule wanakoua albino.

Nikiwa hapa nyumbani, nilishuhudia mchungaji mmoja wa Vancouver Canada, baada ya kuona footage ya Vick Ntetema, alikuja Tanzania na kuanzisha "under the same sun" NGO. nimejiuliza maswali mengi sana. huyu mcanada amehangaika sana, na wanashirikiana na watanzania wenye albinism kusambaza uelewa na wanatafuta pesa hata za wahisani kusomesha watoto wenye albinism na kuwasaidia mambo mengine mbalimbali. (pitia website yao au google under the same sun).nimesoma historia yake yote na jinsi alivyopata shita kama ablino. maswali mengi hayajibiki:

1. hivi, serikali ya Tanzania imeshindwa kuwakamata na kuwaadhibu waganga wa kienyeji na matajiri/viongozi wanaonunua viungo vya albino hadi mtu wa canada aje kwa ndege garama zake kuja kutusaidia kupambana na mdudu huyu?

2. hivi, ni kwamba serikali haina nguvu katika hili, hata kusambaza awareness tu kwa raia ili waelewe kwamba mauaji dhidi ya albino ni myth?

3. hivi, hadi lini tutakumbatia na kuwapa vibali waganga wa kienyeji Tanzania? hawa ni wachawi tu, hawana maana yoyote, watumishi wa shetani wanaojifanya waganga. hakuna mganga mzuri kwasabbu hakuna mtumishi wa shetani mzuri, tangu lini shetani akawa mzuri? au kwasababu asilimia 90% ya viongizo au matajiri ni wateja wa waganga wa kienyeji hivyo wanaogopa wakiwatumbua watanyimwa ndumba?

4. hivi, serikali ya kikwete ilishindwa kabisa kuweka miundombinu ya kuwasaidia albino mfano: wanahitaji mafuta ya kupakaa ambayo ni garama, wanahitaji kusomeshwa bure kwenye shule maalumu zitakazowahakikishia usalama, wanahitaji chakula bora etc ijulikane most persons living with albinism wanatoka familia za kimasikini kupindukia hata kama wale wasio na albinism ni masikini lakini hawa wamezidi kwasababu ya kutengwa hawapatiwi hata kazi/ajira kirahisi na kuna matatizo mengi sana. serikali haiwasaidii hadi mtu wa nchi za nje aje?

5. serikali ya magufuli ina mpango gani, hata mpango wa kuongea tu basi ili tuwapime kama mna nia ya dhati kuwalinda, kuwainua watu wenye albinism. kama wanawake wasio na ulemavu wa macho au ngozi wanapewa kipaumbele cha kuinuliwa, kwanini hawa ndugu zetu wanaowindwa kama wanyama wasipewe kipaumbele?​

with respect, rafiki yangu Dr. Possi, naomba uongeze nguvu katika kazi yako, acha upole, najua hauwakilishi hawa ndugu zetu tu, unawakilisha wote lakini the most vulnarable group of all katika wizara unayowakilisha, ambao hawalali kwa amani wakiogopa kukatwa ni watu wanaoishi na albinism. sijaona ukiwa mstari wa mbele sana, tembelea vituo vya polisi upate report, hebu kuwa hata kama kina makonda hivi aisee uonekana ukifanya kitu, unawawakilisha watu wengi sana nyuma yako ujue.......sisemi kama haufanyi kazi, nakujua wewe ni mfanya kazi sana lakini ujue umeingia kwenye siasa, unahitaji publicity inayoonyesha unafanya kazi, unakemea waovu, unapambana na unawaweka watu kwenye acountability, sio kufungua tu maonyesho na matembezi, I wish ningekuwa kwenye position yako hiyo, survailance ambayo ningeiweka Tanzania nzima ingekuwa nzuri. hatuwezi kupinga kwamba, uliteuliwa kuwakilisha hawa ndugu zetu na unatakiwa uwawakilishe vizuri; sisemi kwamba hauna uwezo,una uwezo sana, ninakufahamu ulinizidi miaka miwili pale faculty of law udsm, mbona ulikuwa mbishi sanaaa na mpambanaji mwenye akili nyingi ambayo ni character ya mwanasheria...lakini nakuona kama mnyonge na mpole?...tafadhali kaka.....
 
ukiona kiongozi anashikilia waganga wa kienyeji na kuwapa vibali hao wapiga ramli, ujue yeye ni mteja wa wapiga ramli na hawezi kuwa kiongozi bila kuamini imani za kishirikina. ushetani umetawala sana Tanzania. mambo yaliyotabiriwa kwamba kutakuwa na biashara ya kuuza viongo vya binadamu leo yametokea Tanzania, siku za mwisho hizi.
 
Back
Top Bottom