nessonlegend
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 1,698
- 1,512
Kwa utafiti huu serikali haina haja ya kufumba macho.
Wakuu salama.
Katika gazeti la Mwananchi tar 26-may-2017 ukurasa wa pili, kuna habari isemayo: HIKI NDICHO KIINI CHA MAUAJI PWANI. katika habari wameelezea kwa ufasaha ambao hata mtoto mdogo wa shule ya msingi hatopata tabu ya kuelewa ni nini kinaendelea huko Pwani.
Moja ya sababu ni; UONEVU NA DHURUMA ILIYOKITHIRI.
katika sababu hii wameelezea hali ya maisha ya wakazi wa Kilwa, mkuranga, kibiti na rufiji kuwa wengi ni masikini na elimu ni ndogo hivyo wengi huendesha maisha kwa kuvuna ama rasilimali za asili kama mbao na mkaa, lakini pia wamewekeza katika mazao ya mashambani. Lakini cha kushangaza ni namna wanavyokutana na changamoto hasa wakati wa usafirishaji wa bidhaa hizo wanazotokanazo kijijini kuleta mjini kuwa kumekuwa na urasimu mwingi hasa toka kwa wakaguzi wa maliasili ambao wamekuwa wakishirikiana na polisi ambapo inafika wakati wanadhurumiwa mali zao walizopambana kwa jasho huku jua likiwawakia. Na hata walipoenda kutoa taarifa kwa viongozi wa mitaa wamekuwa hawasaidiwi au kero zao hazitatuliwi bali wamekuwa wakipewa majibu ya kisiasa tu.
Lakini mwishoni na habari hii wameandika
USHAHIDI WA KUUNGA MKONO.
Kuuwawa kwa ofisa upelelezi wa wilaya ya kibiti (OC-CID) na maofisa wawili wa maliasili waliokuwa wakikusanya ushuru wa mazao katika kijiji cha jaribu wilayani kibiti. Kwamba kabla ya kuua kwa Risasi, waliteka kwanza. Kisha wakawaruhusu wananchi wa eneo hilo kuchukua mali zilizokuwa zimehifadhiwa katika Kituo hicho. Waliwateka watumishi waliokuwa zamu na kuwataka kukaa kimya kwasababu walikuwa na kazi ya kufanya kabla ya kwenda zao, kazi hiyo ndiyo ilikuwa ya kuruhusu wananchi kuchukua shehena za mkaa ili wapunguze ukali wa maisha na kweli bila kusita wananchi walihamasishana na kuanza kujibebea tu. Baada ya kufanya mauaji inasemekana waliacha majina ya viongozi wa mitaa ambao wangeshughulikiwa kwasababu ya kushindwa kuwasaidia wananchi.
Ukisoma kwa undani habari hii na ukatumia akili kufikilia utatambua kabisa ya kuwa Mauaji yanayoendelea kule ni chuki dhidi ya uongozi wa serikali za vijiji pamoja na maafiaa maliasili kwa kuendeleza udhalimu dhidi ya wananchi.
Tumeshuhudia wiki iliyopita jinsi waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba akitoa kauli tata ambayo kwa namna moja ama nyingine inaweza isizae matunda chanya bali ikazidisha uhasama katika ya vyombo vya dola na wananchi ambao wanadai haki zao kupitia mlango wa nyuma.
Kutokana na matukio haya kuna maswali ambayo tunatakiwa tujiulize kwa uyakinifu na uchanganuzi wa akili kabla ya kuchukua hatua pamoja na kwamba maswali haya alijiuliza Mh waziri lakini sidhani kama alichukulia kwa uzito na upana wake au aliongozwa na hisia za kisiasa kwasababu tu yeye ni kiongozi na ni mwanasiasa.
1) kwanini wanouwawa ni viongozi wa ccm ama watumishi ambao kwa namna moja ama nyingine wanauhusiano na ccm? (serikali)
2) kama wauaji wana nia mbaya na mkoa wa pwani au vijiji vya mkoa huo, ni kwanini baada ya kuteka kituo cha ukaguzi wakaruhusu Wananchi wachukue mali zilizokuwepo hapo?
3) ni kwanini wauaji hawatekelezi azma ya kuvamia makazi ya watu ama maduka na kufanya uhalifu kama huo badala yake wanawalenga viongozi na watumishi wengine wa serikali?
Kwa kujiuliza maswali haya na kuweza kupata majibu sahihi nadhani waziri angerudisha nyuma jeshi la polisi na kisha ufanyike uchunguzi makini wa bila kutumia silaha kwani kwa upande wangu naona mauaji haya kwa namna moja ama nyingine ni kisasi kwa wale amabo sauti zao zimezimwa na wale wanaowaongoza hivyo nguvu haitazaa matunda bali kuzidisha hasira zaidi kwani itafika siku jeshi la polisi litakamata watu wasio na hatia wakijua wakijua wamemaliza kazi kumbe watekelezaji wapo pembeni wanasoma mchezo na kusuka mkakati wa kufanya mashambulizi zaidi.
Peter Toshi, katika wimbo wake wa Equal right and Justice, anasema pasipo haki na usawa basi amani ni hakuna na kama ipo ni ya muda tu.
ZINGATIO: Habari hii nimeichukua katika gazeti la MWANANCHI Ijumaa 26-5-2017. Nimeongeza baadhi ya maneno na nimepunguza pia.