Kuna taarifa kwamba kuna mauaji ya kutisha huko Nachingwea hadi kusababisha wanawake kuandamana kwenda kwa mkuu wa wilaya. Mwenye taarifa zaidi atuambie vizuri.
Ni kwanini binadamu anaweza kufanya unyama wa aina hii dhidi ya binadamu mwenzake? Hata simba hawezi kufanya hivyo. Baada ya hapo anakuwa na furaha gani duniani? Na yeye si kuna siku ataondoka? Inasikitisha sana na kuudhi sana. Zamani watu walikuwa wanajilinda dhidi ya wanyama wakali kama simba, chui na fisi. Leo binadamu anajilinda dhidi ya binadamu mwenzake! Ee Mungu uwape stahili yao watesaji na wauaji hao. RIP mama/dada!