Mauaji Kiteto yanawakera wananchi na viongozi

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
449
60
Kwa miaka kadhaa mauaji Kiteto yalianza kusahaulia, awali watu waliuana, ukiuliza sababu ya msingi ni kugombea ardhi. Baada ya kuingia utawala ya JPM mabadiliko makubwa yalifanyika kisha wananchi waliweza kuishi salama.

Sasa jinamizi kama alivyosema Mkuu wa Wilaya ya Kiteto TIMAINI MAGESSA, lilipita tena siku tatu zilizopita na kukwapua roho za watu kwa nguvu. Ilikuwa hivi kule Kijiji cha Kijungu mtu mmoja alionekana akikimbia kisha kuingia nyumbani kwa mtu, hapo wakapiga kelele na kufika kijana mmoja na kumtoa nje.

Mda mfupi wakati wanasumbuana Kijana huyo alichomoa kisu na mtu huyo na kupoteza maisha, jambo ambalo liliibua hisia mbaya kwa watu. Huwezi kuamini watu walianza kumkimbiza na kumkamata badala ya kumfikisha aKituo cha Polisi waliamua kumuua, Dah!

Kuacha huyo mwenyekiti wa kamati ya mazingira Kijiji cha Kinua aliuawa kikatili kwa kukatwa na shoka kichwani, Siku sio nyingi kana kwamba haitoshi. Kijana mmoja dereva wa bodaboda huko Kijiji cha Matui, Kiteto naye aliuawa siku hiyo hiyo na watu wasio julikana watu hao kutoweka na pikipiki yake.

Haya matukio yalisahaulika lakini yalikumbusha machungu ya watu hapo nyuma, nasema Mungu tuepusha haya.

Naomba viongozi wetu wadhibiti vitendo hivi kwani wananchi tuliishi salama kwa amani tukianza kusahamu yaliyopita sasa tunaanza kukumbushana, Dah! Hakika hakuna anayependa kupoteza uhai wake ama uhai wa ndugu yake kwaajili ya ardhi ama kitu kingine chochote BUSARA NA HAKI ITUMIKE.

Mungu bariki Tanzania Mungu Bariki Afrika Amina.
 
Back
Top Bottom