Matuta na vituo vya Mizani barabara za Bongo

Matuta na vituo vya Mizani barabara za Bongo

Wickama

Platinum Member
Joined
Mar 8, 2009
Posts
1,568
Reaction score
1,350
Wakuu, ndio kwanza narejea toka mikoa ya kanda ya ziwa kwa kupitia Kenya. Nilifuata barabara ya Tanga-Mombasa-Nairobi-Narok-Kisii-Tarime. Nilichojionea ni kama ifuatavyo;

  1. Matuta ya barabarani kwa upande wa Kenya ni machache sana. Kiasi kikubwa ni kuwa highway nzima inapitika bila matuta kasoro sehemu chache sana. Tena matuta yapo zaidi eneo la Kisii kwenye highway ya Sirari-Kisii kuelekea Kericho, sio kwenye highway ya Kisii-Narok.
  2. Mizani ya kupima magari uzito kwa njia nzima ipo Mombasa eneo jirani na Mariakani. Hii ina maana kwa kilometer zaidi ya 1000 ni mizani hii pekee niliyoiona.
  3. Magari ya abiria (mabasi) hayasimami mizani kupima uzito.

NAULIZA KWA NINI HAPA BONGO HALI NI TOFAUTI?
 
binafsi kinachokera si wingi wa matuta bali ni alama kuonyesha kua kuna tuta mbele, sehem nyingi sana tuta linawekwa bila alama kabisa imagine una drive mchana labda kwenda mwanza lazima utapanda matuta kadhaa kwa kuyaona gafla imagine sasa kama unasafir ucku chance ya kupata ajali ni kubwa sana! wengi tunaendesha hizi barabara za kwenda mikoani kwa kuzikariri kwamba sehem flan kuna kuaga na tuta unaanza kujiandaa kabla hujafika hilo eneo.

linalokela zaid ni size ya matuta, kuna matuta variety kadhaa tena kuna mengine hata ukipanda pole pole bado gari ina shake kama nn au mengine kama gari yako ni ya chini hata ujitahidi vp lazima itagusa chini tu!!
we need to even the size as well plus reducing some of them!!!
 
Na ht kwenye mizani,haya magari ya abiria hayapewi kipaumbele ni mwendo foleni tu. Basi ukute malori yameshika nafasi,abiria ndio mtakaaje kusubiria zamu yenu....
 
vipi kuhusu upande wa madereva kenya na tz? kufuata sheria na umakini, labda ndomaana kuna tofauti?
 
vipi kuhusu upande wa madereva kenya na tz? kufuata sheria na umakini, labda ndomaana kuna tofauti?

Kwa mabasi mengi yanayoenda masafa marefu nchini Kenya upo utaratibu wamadereva kubadilishana usukani baada ya mwendo fulani. Basi nililotumia (Otange Bus), dereva alipolifikisha Nairobi tokea Migori (371km) alikaa pembeni mwenzake akalichukua tokea Nairobi hadi Mombasa (483km). Hili basi lilikuwa na speed governor na halikuzidi 80km/hr. Nimeambiwa kuna mabasi (ili kuvutia abiria) yamejiwekea utaratibu huu wa kuthibiti mwendo kwa hiari.

cc lawmaina78
 
Last edited by a moderator:
Na ht kwenye mizani,haya magari ya abiria hayapewi kipaumbele ni mwendo foleni tu. Basi ukute malori yameshika nafasi,abiria ndio mtakaaje kusubiria zamu yenu....

Kinachokera kwa mabasi ni pale linapokaribia mizani halafu abiria walioko viti fulani vya nyuma mnaombwa kuhamia mbele ili uzito usizidi wakati wa kupimwa. Likishavuka mizani mnarudi kwenye viti vyenu. Haya nimeyashuhudia kila leo kwenye mabasi ya Tanga-Dar. Tanga-Dar (354 kms) basi linapita mizani 3 (tanga, wami, kibaha), kwenye siku mbaya mnahama mkikaribia kila mizani.
 
sio huko tu ht magari ya musoma, mwanza,shinyanga,nzega hadi dodoma mwendo ni huohuo......hadi inaboa sn kukaa seat za nyuma.
 
nadhani mengi yanawekwa kisiasa
 
binafsi kinachokera si wingi wa matuta bali ni alama kuonyesha kua kuna tuta mbele, sehem nyingi sana tuta linawekwa bila alama kabisa imagine una drive mchana labda kwenda mwanza lazima utapanda matuta kadhaa kwa kuyaona gafla imagine sasa kama unasafir ucku chance ya kupata ajali ni kubwa sana! wengi tunaendesha hizi barabara za kwenda mikoani kwa kuzikariri kwamba sehem flan kuna kuaga na tuta unaanza kujiandaa kabla hujafika hilo eneo.

linalokela zaid ni size ya matuta, kuna matuta variety kadhaa tena kuna mengine hata ukipanda pole pole bado gari ina shake kama nn au mengine kama gari yako ni ya chini hata ujitahidi vp lazima itagusa chini tu!!
we need to even the size as well plus reducing some of them!!!

Kila barabara ina matuta yake. Hayako standard kabisa.
 
Ukiambiwa na kondakta ondoka kwenye seat yako na wewe ukakubali maana yake unasaidia kutenda kosa. Mimi huwa nakataa kusimama na hawanifanyi chochote. Tujenge utamaduni wa kufuata sheria. Ila naomba Magufuli afute mzani wa morogoro ni kero. Haiingii akilini gari lipime mikese halafu lipime tena morogoro ni shida. Kama mzani wa moro ni muhimu uwepo basi wasubiri mpaka watakapojenga mzani mwingine upande wa pili.
 
Back
Top Bottom