Matunda ya Tikiti kuoza yakiwa bado madogo

Mkuu kuoza kwa vitunda inaweza kuwa ni uwekaji dawa nyingi kama Dasban.

AU

Kuna wadudu wadogo ambao kienyeji huko mitaani wanaitwa inzi wa maembe hao huozesha hivyo vitunda vichanga vya tikiti. Kuna dawa nimesahau jina huwa unaweka kwenye vikopo unaweka sehemu nyingi shambani hao wadudu wanakimbia.

AU

Uchavushaji (pollination) sio mzuri kama alivyosema mdau ktk ile namba 1, nyuki wanaweza kuwa wengi lakini hawatui na kunyonya asali kwenye maua sababu ya harufu ya madawa. Kwa hivyo unatakiwa upulize dawa alfajiri au jioni karibu giza kabisa. Ikikulazimu punguza kiwango cha madawa makali.

NB: Watafute kilimomaarifa wana thread humu JF watakusaidia vizuri tu.
Kwa mimea inayotegemea uchavushaji wa wadudu ni vyema dawa apulize jioni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungeweka picha ya tunda lililoharibiwa ingekua rahisi kweli kweli walau ku suspect tatizo ni nini, ila kwa uzoefu wangu wa wakulima wenye case kama zako ni kuna wadudu wanaitwa Inzi wa matunda au kwa kimombo melon fly au wengine huita fruit flies. Ni wadudu waharibifu sana wa matunda hakuna mfano na kibaya zaidi hawafi kwa dawa za ku spray inabidi utafute dawa special ya kuua aina hiyo ya wadudu pekee ambayo hutundikwa shambani.
Nliekushauri ni mtaalam wa kilimo (afisa ugani).

Sent using Jamii Forums mobile app
Picha hizo hapa mkuu
 
Attachments

  • 20190112_165436.jpg
    20190112_165436.jpg
    256.5 KB · Views: 54
Nitafanya kilimo cha tikiti kama ziada nikiwa na vitu mbadala vya kunipa hela. Unateketeza 5m alafu ukute ndo umechukua mkopo saccos... Lazima uugue kwanza
 
Nitafanya kilimo cha tikiti kama ziada nikiwa na vitu mbadala vya kunipa hela. Unateketeza 5m alafu ukute ndo umechukua mkopo saccos... Lazima uugue kwanza

Hilo ni jambo muhimu sana inatakiwa watu walizingatie.

Kuna jamaa moja nilimkuta kwenye duka la pembejeo; nimkulima mzoefu wa matikiti, lakini ilifika na yeye yakagoma. alikuwa metumia pesa nyingi. kwa sababu alikuwa hana shughuli ya kumuingizia pesa ikabidi auze shamba ili aendlee kulima na kulipa madeni.
 
Watanzania wengi wanadanganywa na motivational speakers wanaokuja na maelezo matamu ya utajiri lakini hawana uhalisia
 
mkuu mimi lishawahi kutokea tatizo kama hilo ndan kulikuwa na funza.tatizo ni nn?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo ni inzi. kuna nzi fulani hutaga mayai kwenye tunda baada ya mda yale mayai yanakuwa funza amabao hutoboa tunda.
Suluhisho kila unapoona maua yametoa matunda inabidi upige dawa. Binafsi nime tumia dawa aina ya cutter na matokeo ni mazuri.

Ili kudhibiti hao inzi kuna vikopo fulani unaninginiza shamba kwa ajili ya kuwanasa hao inzi. nimefunga hivyo vikopo pia.
 
shukran mkuu....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom