Matumizi yasiyo Sahihi ya herufi ''L'' na ''R'' mitandaoni yananikera

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,488
Unakuta mtu badala aandike neno kwa usahihi analiandika katika matumizi ya herufi ambayo siyo na huku ni kuzuoesha wengine matamshi ambayo mwisho wa siku yatazidi kuharibu lugha ya kiswahili.

Mfano mtu anaandika neno ''kelo'' badala ya kero
''habali'' badala ya habari
''badara'' badala ya badala
''hasila'' badala ya hasira

Tujifunze matumizi sahihi ya herufi ndugu zangu, mazoea ni kilema. Hadi kwenye magazeti waliozoea kukosea matamshi haya huandika kwa kukosea pia.

Ahsanteni.
 
kuna sababu nyingi zinazosababisha watu kuchanganya matumizi ya maneno haya, eidha kwenye matamshi au kuyaandika,moja kubwa ni effect ya lugha ya awali au asili,kuna baadhi ya makabila yanasumbuliwa sana na matumizi ya maneno haya pamoja kwamba sitayataja makabila hayo.sababu nyingine ni uelewa,kuna uelewa wa aina tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine,wengine wana uelewa wa haraka na wengine taratibu,hata shuleni mnaweza kuwa wanafunzi 30 lakini akapatikana wa kwanza na wa mwisho miongoni mwenu.la muhimu ni kusahihishana bila kuaibishana au kudharauliana.
 
Wengine wanaokera ni wale wanaotumia herufi "h" pasipostahili, mfano:
hakamwambia=akamwambia,
hanakuja=anakuja, nk.

Wengine wanaochafua lugha ni wale wanaotumia neno "dhibitisha" au "dhibitika" badala ya neno sahihi "thibitisha" au "thibitika". Kwa kweli wabadilike.
 
Yule Mkuu wa Wilaya ya Iringa Jana amechanwa kwenye wall yake ya Facebook. Kaandika Cathoric badala ya Catholic, jamaa kamparamia kamchana vibaya! Mkuu wa Wilaya Mzima unafanya mambo ya kijinga namna hiyo?!!?
 
Kuna wengine sijui ni wavivu au kutokujua kutumia herufi ''h'' pale panapostahili?!
mfano;

Awezi = hawezi
Aamini = haamini
Alaf = halafu

Huwa najiuliza hivi hawa watu wa aina hii hata huko mashuleni kwao au wanapokua ofisini kikazi hutumia hii lugha?

Pia kuna wale wanaoiga Kiswahili cha Kenya,

Mfano;

1-Naenda kwa ofisi=naenda ofisini
2-Niko kwa barabara=nipo barabarani
3-Niko kwa Nyumba = nipo Nyumbani
 
Tatizo nyinyi watoto wa ki dar es saraama mnajifanya mnajuwa sana kufanya critic, mmesaau kuwa watu utofautihana ufaamu na mda mwengine ni makaso ya kibinadamu na wengine kiswahili sio lugha yao.
 
We bora R&L,Mimi A&H Mfano.hanalima badala ya analima,tatzo ili liko kwa wahaya na wangindo.
 
Unakuta mtu badala aandike neno kwa usahihi analiandika katika matumizi ya herufi ambayo siyo na huku ni kuzuoesha wengine matamshi ambayo mwisho wa siku yatazidi kuharibu lugha ya kiswahili.

Mfano mtu anaandika neno ''kelo'' badala ya kero
''habali'' badala ya habari
''badara'' badala ya badala
''hasila'' badala ya hasira

Tujifunze matumizi sahihi ya herufi ndugu zangu, mazoea ni kilema. Hadi kwenye magazeti waliozoea kukosea matamshi haya huandika kwa kukosea pia.

Ahsanteni.
Labda mtoa maada yanakela nini, ivi ukikuta sms kwenyesimu yako imeandikwa "Umepokea SHIRINGI 1'000'000 utakuwa bado hujahelewa.
 
Du, kaazi kweli kweli wa kwanza ku respond kaandika eidha badala ya aidha mi naona kama maana au ujumbe unafika tuache hivyo hivyo ! Mzungu mmoja alisema ukimpa nafasi mtz ajielezee kiswahili humuwezi ila mwambie aandike utachoka.
 
Nyinyi=Ninyi
Mmesaau= mmesahau
Utofautiana= Hutofautiana
Jindal singh kwa kiswahili hiki heri uandike Kihindi
 
Tatizo nyinyi watoto wa ki dar es saraama mnajifanya mnajuwa sana kufanya critic, mmesaau kuwa watu utofautihana ufaamu na mda mwengine ni makaso ya kibinadamu na wengine kiswahili sio lugha yao.
Hapo kwenye red,ndio wapi huko?!
 
Nyinyi=Ninyi
Mmesaau= mmesahau
Utofautiana= Hutofautiana
Jindal singh kwa kiswahili hiki heri uandike Kihindi
Ndugu mini hapa sijakuelewa kwa hili neno NINYI. Ninyi ni neno sahihi kabisa la kiswahili
 
Tatizo n shule na mazingira tuwashukuru hao wapo wengine hawajui kabisa eidha walim wao ndo chanzo
 
Mambo yakuandika Imla shuleni yalishapotea miaka mingi sana acha tu waendelee kukosea msingi ulishabomolewa. Mi nakumbuka kuandika maneno vizuri ilianzia kwenye Imla na Dictation shule ya msingi huko. Sina uhakika kama kizazi hiki hili suala bado lipo.
 
Tatizo nyinyi watoto wa ki dar es saraama mnajifanya mnajuwa sana kufanya critic, mmesaau kuwa watu utofautihana ufaamu na mda mwengine ni makaso ya kibinadamu na wengine kiswahili sio lugha yao.
Siyo suala la watoto wa Ki-Dar es Salaam. La hasha. Watu hawataki kujifunza. Wako wengine hata wakisahihishwa wanakuwa wakali na kudai eti walichoandika kinaeleweka. Wakati huo kaandika "asila" badala ya "hasira".
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Tatizo jingine ni punctuation jamani, na maana koma , vituo , mshangao nk . Unakuta mtu kaandika mnyororo wa maneno bila koma , kituo au alama nyingine za maandishi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom