Matumizi ya tumbaku yapungua duniani

Matumizi ya tumbaku yapungua duniani

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,359
Reaction score
4,814
Ripoti mpya ya kila mwaka ya Shirika la Afya Duniani WHO kuhusu tumbaku, inaonesha matumizi ya tumbaku kwa wanaume yameanza kupungua kwa mara ya kwanza.

Kwa mujibu wa shirika hilo idadi ya wanawake wanaotumia tumbaku imepungua kwa takribani milioni 100 kati ya 2000 na 2018, na kwa wanaume imeongezeka kwa kiasi ya watu milioni 40.

Shirika hili linakadiria kuwa idadi hiyo ya wanaume itapungua kwa watu milioni 2 katika mwaka ujao, na milioni 6 zaidi itakapofikia 2025. Hata hivyo ripoti ya WHO inaonesha pia wanawake wanaweza kukabiliana na uraibu wa tumbaku haraka ikilinganishwa na wanaume.

Kwa ujumla shirika hilo limesema idadi ya watumiaji wa tumbaku umepungua kutoka bilioni 1.4 kwa mwaka 2000 hadi kufikia bilioni 1.3 kwa mwaka 2018.
1576763416953.png

1576763452946.png
 
1576816009638.png

Matumizi ya tumbaku miongoni mwa wanaume yameanza kupungua kwa mara ya kwanza, kulingana na ripoti ya kila mwaka ya shirika la afya duniani WHO.

Idadi ya wawanake wanaotumia tumbaku ilipungua kwa karibu milioni 100 kati ya mwaka 2000 hadi 2018. Hata hivyo, wanawake wameendelea kupunguza matumizi ya uraibu wa Nikotini ukilinganisha na wanaume.

Mwaka 2000, karibu theluthi tatu ya watu duniani walio na umri wa miaka 15 na zaidi walikuwa wakitumia tumbaku, sigara na bidhaa nyingine za tumbaku. Kwa ujumla idadi ya watumiaji tumbaku imepungua duniani kote, kutokana na serikali kuwa na sheria kali dhidi ya uraibu huo.

Kila mwaka watu zaidi ya milioni nane hupoteza maisha kutokana na athari za tumbaku ikiwemo watu milioni 1.2 ambao si wavutaji lakini wakiathirika na moshi wa wavutaji. Mataifa yaliyo na kiwango kikubwa cha uvutaji tumbaku ni yale ya Kusini mwa Asia Mashariki.

Chanzo: DW Swahili
 
Ila kuna ukweli.. maana wakati sisi tukiwa wadogo tulikua tunatumwatumwa sana sigara na ndiko tulikojifunzia kuvuta. Pia tulikua tunawaona ma broo enzi izo wakivuta kwa kificho kule nyuma ya nyumba na vichochoroni. Zamani ilikua ni kawaida kukuta "ash tray" karibu kila mahali. Siku hizi ni nadra sana kumuona mtu anavuta sigara

Back
Top Bottom