Matumizi ya simu ndani ya benki

Matumizi ya simu ndani ya benki

ngonyango

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2017
Posts
1,887
Reaction score
1,623
Huwa sielewi mambo yafuatayo;

1. Mara nyingi walinzi wanatutolea macho tukiwa tunaongea na simu na hata muna makatazo juu ya matumizi ya simu (kuongea)ukiwa ndani ya benki....lakini bado unaweza ukawa unachat na kupiga hata picha ukiwa hapohapo ndani ila hilo halikatazwi....kwangu naona kuruhusu kuchat /text ni hatari zaidi kuliko kupiga/kupokea simu...mnalionaje hili wadau

2. Kuna mabenki hayatakiwi kabisa au yanatakiwa yabadili utaratibu huu wa kukataza watu kutumia simu sababu huduma zao ni slow kupita kiasi ikizingatiwa simu ndiyo jembe lenyewe kwa sisi wengine hivyo mnavyotukataza kutumia simu kwa zaidi ya saa moja mambo yanaharibika sana. Kwa mfano benki ya Equity pale Golden Jubilee Branch hata ukiwa peke yako lazima utumie si chini ya dk 20 kupata huduma.......

Sasa ukikuta kuna foleni ya watu wanne au zaidi kama umeingia saa tatu asubuhi basi huwezi toka chini ya saa sita/saba mchana...Tuachieni tutumie simu jamani hasa Equity Bank - Golden Jubilee...au tuwahame?


cc benki nyingine pia
 
wana maana mkuu kukwambia hvyo, hata picha wanakataza sema wengi wanapiga selfie mlinzi kujua ni ngumu
 
Wachora ramani wapo sharp sana kwa kutumia simu.

Benki nyingi haziruhusu hata kuchat ndo maana huwa kuna video ya kukupa burudani usahau uraibu wa simu kwa muda
 
Hamjanielewa...ni kwamba watu tunatumia simu sababu ya mlolongo mreefu tukiwa benki...sasa kukaa bila mawasiliano masaa mamatu au zaidi ni mateso
 
Back
Top Bottom