buswelu moja
JF-Expert Member
- Aug 24, 2014
- 226
- 180
Ndugu wadau wa jukwaa hili kumekuwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za bindamu na matumizi mabaya ya pingu zinazotumiwa na askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha.
Baadhi ya polisi jijini Arusha wamegeuza pingu kuwa ndio mtaji wao wa kujipatia pesa katika masiaha yao kwa kuwa wakikukamata na kosa wanakwambia tunakutia pingu kama hutaki tupatie kati ya sh elfu 5 hadi 10 hii si sawa ndio maana tumeona tuliweke hapa ili na IGP MANGU alisikie hili pamoja na waziri wa mamabo ya ndani.
Kumekuwa na polisi wanaotumia pikipiki hapa jijini Arusha ambao wanatembea na pingu kila kona na hata kama huna kosa wakikukamata wanatishia kukutia pingu,kuna muda pingu zinatumika bila hata sababu kwa mfano wakifika kwenye tukio na kukuuliza kama shuhuda kabla ya kujieleza wanakutia pingu.
Mfano ni hawa askari wanaotumia pikipiki za PT 3491 na PT 3488 wamekuwa wakitumia vibaya pingu wanazotembea nazo tunaomba uchunguzi wa kina ufanyike juu ya hili kwa kuwa tumekosa majina yao lakini nambari zao za pikipiki tumezinadika mahala kwa kuwa wanapenda kutembelea maeneo ya Ngarenaro,Sakina na Matejoo ambapo ndio wanafanya matengenezo ya pikipiki zao.
Wito wangu kwa jeshi la polisi nchini chini ya IGP MWEMA pamoja na waziri wa mambo ya ndani tunaomba uchunguzi ufanyike juu ya hili kwa kuwa malalamiko yamekuwa ni mengi,asanteni
mdau wa jukwaa Arusha